Simulizi; "THE BLACK KILLER "
    (Muuaji mweusi)


Mwandishi; HAKIKA JONATHAN


Whatsup; 0629905923


**SEHEMU 05**


Jacline alirudisha kitambulisho kile haraka sana baada ya kusikia mlango wa bafuni ukifunguliwa, huku Paul akitoka na kuhisi hali isiyo ya kawaida kwani Jacline alionekana kutojiamini kama awali huku wasiwasi na woga ukiionekana wazi katika sura yake. "Vipi mpenzi, kuna tatizo lolote "Paul alimuulza Jacline huku akijifuta vizuri mwili wake kwa taulo na kukausha maji yaliyokuwa yakitililika mwilini. "Hapana mpenzi niko sawa,ondoa hofu kabisa "Jacline aliongea kwa sauti nzuri iliyomfanya Paul kupotezea swala lile.


…………………………………


"Kuna jambo nataka niwafahamishe, kuna kijana nimekutana naye ……inaonekana anafahamiana na Paul Agustino, kijana huyu nilikagua suruali yake alipokuwa ameenda kuoga na bila kutarajia nilikuta kitambulisho cha jeshi cha Paul. " Jacline aliwafamisha wenzake baada ya kutoka chumbani kwa Paul na kugundua jambo ambalo alishindwa kulihifadhi moyoni, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Paul kwani hisia za mapenzi zilimsumbua na kumtaka asitoe siri ile kwani angemuweka mahali pabaya Paul ambaye yeye alimfahamu kama mr Pius. "Kijana huyo anaitwa nani?……na umefahamiana naye kivipi " Jonson alimuulza swali Jacline, huku Godfrey akiwa makini kusikiliza mazungumzo hayo.



"Kijana huyo anaitwa mr Pius, nilikutana naye nje ya hoteli jana baada ya kusikia akiongea Kiswahili, kutokana na kuniambia anatokea Tanzania nilijikuta nikiwa rafiki yake " Jacline alimjibu Jonson huku akionekana kuchoshwa na maswali mengi aliyokuwa akiulizwa. "Mi nakuomba endelea kuwa karibu naye na uzidi kumchunguza zaidi, lazma atakuwa anafahamu kitu "Godfrey askari aliyekuwa na busara sana katika kila maamuzi aliyoyachukua, alimsihi Jacline aendelee kuwa karibu na Paul, bila kutambua madhara makubwa yatakayotokea mbeleni.


"Mimi pia, naona hilo ndo jambo sahihi nalotakiwa kulifanya ……"Jacline aliongea huku akitabasamu kwa furaha baada ya kuruhusiwa kuwa karibu na Paul, hali iliyowashangaza Jonson na Godfrey kwani hawakufahamu chochote kuhusu furaha hiyo.


…………………………………

Paul Agustino akiwa chumbani kwake anajiandaa na kutafakari namna ya kumuua  Benny Hanson, daktari aliyemfanyia upasuaji na kuibadilisha sura yake. "Nikifanikiwa kumuua Benny, angalau nitaishi kwa amani kwani ndio mtu pekee anayefahamu siri hii ya mimi kubadili sura yangu "Paul aliongea huku akiisafisha bastora yake na kuiondolea mfumo wa sauti na kuwa na uwezo wa kuua bila kutoa mlio (silent). "Hello doctor, aim very sick …just come to help me "(haloo daktari, naumwa sana njoo unisaidie) Paul Agustino alimpigia simu Benny Hanson kwa sauti ya unyonge sana na kujifanya anaumwa ili aweze kufika haraka na kumuua.


Muda si mrefu dokta Benny aliwasili kwani aliyaamini maneno aliyozungumza na Paul kwenye simu, kwani haikuwa kawaida ya Paul kuongea naye kwa sauti ya kinyonge kiasi kile. "Ndiii…ndiiiii ……ndiii…ndiii" mlio wa kengele ulisikika na kumfanya Paul kuikoki bastora yake, kwani kengele hiyo iliashilia dokta Benny alikuwa tayali a
Powered by Blogger.