simulizi; THE BLACK KILLER (Muuaji mweusi)







simulizi; THE BLACK KILLER
   (Muuaji mweusi)
Mwandishi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU 02**
Upelelezi unaanza huku afande Godfrey Manumbu akiongoza kundi hilo lenye watu watatu. "Twanzie kwa ukaguzi wa cctv camera ……twaeza gundua kajambo "askari wa kike kutoka Afrika kusini aliyeitwa Jacline aliwashauli wenzake huku akijitahidi kuongea kwa kiswahili, "Ndio hilo ni wazo zuri " Jonson alimjibu Jacline kwa kiswahili kilichonyooka na kumfanya Godfrey kushangaa sana.."Kumbe mnafahamu Kiswahili …naamini itaturahisia kazi "Godfrey aliongea huku akitabasamu,na kuwafanya wote wacheke kwa furaha. "Hahaahaa ……tumekuja mara nyingi sana kwa Afrika Mashariki kwahiyo Kiswahili tunaongea pia, na ni moja ya sababu iliyotufanya tuchaguliwe kuja huku "…Jacline alimjibu Godfrey huku wakikagua baadhi ya cctv camera zilizoko uwanja wa taifa, mahali mlipuko ulipotokea.


"Njooni muone hii camera  ,mfumo wake haukuharibiwa na bomu "Godfrey aliwaita wenzake baada ya kuhangaika muda mrefu kukagua camera iliyokuwa bado nzima, kwani camera nyingi ziliweza kuharibiwa na bomu vibaya sana.

"Waooh …this can help us "(waooh ……hii inaweza kutusaidia) Jonson aliongea huku akiitazama na kuikagua vizuri camera ile.

…………………………………

Sura ya Askari aliyewahi kuwa komando wa Tanzania inaonekana ikipandikiza bomu kubwa sana lenye uzito wa kilo tano, bomu hilo lilitegwa huku likiwa limetengenezwa kwa mfano wa mdoli wa kuchezea mtoto. Kutokana na muonekano huo ilikua vigumu mtu yoyote kulitambua  bali baadhi ya watoto walionekana wakicheza nalo kutokana na muonekano wake kuwavutia.

"mmmh mbona inaonesha ni komando Paul Agustino, haiwezi kuwa kweli ……siamini macho yangu Paul kashakufa miaka mitano iliyopita kwa ajari ya ndege akiwa anaelekea nchini Canada katika shughuri za kijeshi "……Afande Godfrey alishangaa baada ya cctv camera kuonesha kila kitu ilipounganishwa na kompyuta, huku maelezo ya muhusika na historia yake ikionekana kwenye kompyuta hiyo. "Hapa kutakua kuna siri nzito,, kama muhusika inasemekana kafa na alikua ni askari wa Tanzania ……hapa kuna mkono wa mtu "Jonson aliongea huku akionekana kuchanganywa sana na maneno aliyoyaongea Godfrey.

"We should go to the area where he was buried … we can find something to help us "(tunapaswa kwenda eneo alipozikwa …tunaweza pata kitu cha kutusaidia ) Jacline aliongea maneno yaliyokubaliwa na wenzake na haraka sana walifunga safari kuelekea  mahakamani ili kupewa kibali cha kufukua kaburi ambalo ilisemekana komando Paul Agustino aliweza kuzikwa.


"Aliyezikwa hapa ni mtu feki, kutokana na dokomenti zilizopo …Paul alikua na damu grupu O …lakini vipimo vyangu vinaonyesha kua mtu huyu kabla ya kupoteza maisha, alikuwa na damu grupu AB huku fuvu lake likiwa na tundu la risasi kichwani  jambo ambalo linaonesha maiti hii siyo sahihi " daktari alitoa ripoti baada ya kukamilisha uchunguzi wa maiti iliyokuwa ikisemekana ni ya Paul Agustino.

"Hapa sasa nimeshapata jibu, twendeni uwanja wa ndege tukachunguze camera za watu walioingia nchini na kutoka kabla na baada ya tukio ",Godfrey alizungumza jambo ambalo halikupingwa na mtu yeyote na haraka sana waliondoka katika makaburi ya manispaa ya Kinondoni kuelekea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.


"Mhhh mhusika anaonekana hakua anaishi Tanzania kama inavyoonekana ……aliingia nchini siku mbili kabla ya tukio "Godfrey aliongea huku wakiwa makini na wenzake kufuatilia cctv camera iliyokuwa ikionesha matukio yaliyopita uwanjani hapo.

"What !!………waziri wa ulinzi atakua anahusika kwa namna moja au nyingine kwanini alienda kumpokea uwanja wa ndege " ,bwana Godfrey aliongea huku wakishuhudia mheshimiwa  Sarehe Athuman ambaye ni waziri wa ulinzi wa Tanzania akimpokea mtuhumiwa aliyekuwa akionekana kutokea Canada kutokana na taarifa zilizotolewa na wahudumu wa usafiri wa anga.

"Our cctv camera system was hacked the next day after  explosion ……I think the suspected person disappeared on that day "(mfumo wetu wa cctv camera ulihakiwa siku iliyofuata baada ya kutokea mlipuko ……nafikiri mtuhumiwa alitoweka siku hiyo) mhudumu wa kizungu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere aliongea hasa baada ya taarifa za kutoka nchini mtuhumiwa zikiwa hazionekani kwenye kompyuta.

"What you are saying can be right, if not!  Still the suspect might be here in Tanzania ……"(unachokisema kinaweza kuwa sahihi, kama siyo sahihi! Mtuhumiwa atakua bado yuko Tanzania) Jacline alizungumza maneno yaliyoungwa mkono na kila mmoja.

"Mi naona waziri wa ulinzi akamatwe ahojiwe, atakuwa anafahamu kila kitu kuhusu mlipuko huu na mahali muhusika alipo. "Jonson alishauri jambo ambalo liliweza kuleta manufaa katika upelelezi na kutambua ukweli kuhusu kifo cha Paul Agustino, mmoja kati ya makomando kumi pekee wa jeshi la Tanzania.


"Kuanzia leo natengua uteuzi wa waziri wa ulinzi mheshimiwa Sarehe Athuman kutokana na tuhuma nzito alizonazo za kuhusika na mauaji yaliyotokea, na akamatwe haraka iwezekanavyo kwa mahojiano………" Raisi alitoa amri iliyoungwa mkono na viongozi mbalimbali wa nchi ya Tanzania huku, wananchi wakipiga kelele za shangwe kufurahia maamuzi hayo ya raisi yaliyokuwa yakirushwa hewani kupitia redio na televisheni zote nchini.


…………………………………

"Yalaaa………mnisamehe jamani …nakufa mimi …Msiniue nitasema kila kitu, Paul Agustino yuko hai na ndio kahusika na shambulio la kigaidi lililotokea kwa ajili ya kumuua raisi ili mimi niweze kuipindua serikali iliyoko madarakani ….na niweze kuwa raisi wa Tanzania ………Paul hakufa kama ilivyokua inafahamika bali tulifanya mpango wa kulidanganya taifa kuhusu kifo chake ili tuweze kumtumia katika shughuri zetu kulingana na uhodari na ushujaa alionao katika masuala ya kivita ",waziri wa ulinzi aliongea kwa maumivu makali baada ya mateso ya siku mbili mfululizo bila kula chakula cha aina yoyote ile, huku akipigwa bila huruma na kundi la askari watatu wakiongozwa na afande Godfrey Manumbu.

"Paaaah ……" mlio wa kitako cha bunduki ulisikika na kufanya kichwa cha bwana Sarehe kuvuja damu, "Sema mpuuzi wewe, mtuhumiwa yuko wapi ……" Jonson aliongea kwa hasira huku akikumbuka kifo cha raisi wao wa Afrika Kusini kilichosababishwa   na mlipuko huo huku bwana Sarehe akiwa muhusika namba moja wa tukio hilo …….."ooooh !!…msiniue tafadhali ……nitasema ukweli  mtuhumiwa kakimbilia nchini Marekani katika jiji la Newyork ……" Bwana Sarehe aliongea kwa maumivu makali huku akitoboa siri nzito iliyokuwa imefichika.
***ITAENDELEA *
Powered by Blogger.