HISTORIA ILIYOFICHIKA JUU YA VITA VYA MAJI MAJI VILIVYOPIGANIWA KWENYE ARDHI YA TANZANIA KATIKA MIAKA YA 1905-1907




Image may contain: 4 people
HISTORIA ILIYOFICHIKA JUU YA VITA VYA MAJI MAJI VILIVYOPIGANIWA KWENYE ARDHI YA TANZANIA KATIKA MIAKA YA 1905-1907.
Asilimia kubwa ya watanzania wanajua historia ya vita hivi ambavyo vimehusisha makabila mengi ya hapa nchini mafano, wangoni, wapogoro, wazaramo, wafipa, wabena na wandamba, ili kupinga Ukoloni wa Mjerumani ulioanzishwa hapa Tanzania katika miaka ya 1890’s. Jina la vita hii lilitokana na maji ya kimiujiza yaliyotumiwa kama dawa ya kukinga risasi. Historia inasema kuwa maji hayo ya Baraka yalichotwa katika mto Ngarambe unaopatikana kusini mwa Tanzania.watu walikuwa hawanywi maji hayo, bali waganga wa kila kabila walipewa na kuwanyunyuzia wapiganaji.aliyekuja na wazo hili la kimiujiza alijulikana kama bwana Rajabu ari maarufu kama Kinjekitile Ngware. Kwa namna hiyo kila waganga wa kabila walipewa na kuwanyunyuzia wapiganaji. Lakini dawa ilipofika kwa wangoni walipinga na kuikataa . Walipinga kwani wangoni walikuwa na njia ya kutambua ushindi katika vita. Wangoni walitumia mzizi ambao wakiurusha juu, kama ukianguka ni ishara ya kushindwa na kama ukiganda ni ishara ya kushinda. Hivyo mzizi uiporushwa ulianguka, hivyo wangoni walijua kuwa kwenye vita hivi hawatashinda.kwa kuwa makabila mengi yaliamini maji hayo, wangoni walibidi wafanye majario juu ya maji hayo.jaribio la kwanza walifanya kwa Mbwa, walimnyunyuzia Mbwa na wakampiga risasi,na mbwa akafa palepale, ndipo wangoni wakasema maji hayafai, lakini waganga wengine wakasema dawa hii inafanya kazi kwa binadamu na sio kwa mnyama. Na ndipo wangoni wakamchukua Mfungwa wakafanya hivyo hivyo na mwisho mfungwa akafa.wangoni wakazidi kugoma, ila waganga wakasema dawa hii inafanya kazi kwa wanajeshi wanaopiga vita. Hivyo wangoni hawakuwa na la kusema ilibidi waende vitani. Na mwisho watanzania wakapigwa na kuuwawa na wajerumani kushindwa vita.watanganyika wengi hawakufa kwa kupigwa risasi kama wengi wanavyofahamu, bali watu wengi walikufa kwa njaa, baada ya wajerumani kuzidiwa waliamua kuchoma moto vyakula vyote.
Powered by Blogger.