Simulizi; "THE BLACK KILLER" (muuaji mweusi)
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 14**
"Samani mkuu, tumeweza kupata mawasiliano ya ndege yetu iliyotekwa na Paul, kompyuta inaonesha ndege yetu iko katika kisiwa kidogo ndani ya bahari ya Hindi, bila shaka mtuhumiwa atakuwepo mahali hapo " ,mmoja wa askari katika kitengo cha mawasiliano, alitoa ripoti yake ya uchunguzi kwa kiongozi wao bwana Godfrey. "Inatakiwa tuvamie eneo hilo kwa siri, haitakiwi umwambie mtu yeyote, tutatangulia wawili tu mimi na Jonson, lakini nyie mtakuja baadaye " ,Godfrey alimjibu askari yule aliyempatia taarifa hiyo, huku akijiandaa kwa ajili ya kuelekea katika kisiwa hicho haraka sana.
Kwa upande wake Paul, ngome yake iliendelea kuwa tajiri, kwani walizivamia meli za abiria na mizigo katika eneo lote la bahari ya Hindi, na kupora mali mbalimbali pamoja na vito vya thamani na kisha kuua abiria waliokuwa ndani ya meli hizo. Bila kutambulika, waliweza kuendelea na shughuli zao za kikatili huku wakitumia rushwa kama moja ya siraha za kujilinda. "Meli yetu moja ya mizigo imetekwa na maharamia baharini, wameiba kila kitu na kisha kuua watu wote waliokuwa ndani ya meli hiyo ", kiongozi mmoja wa ngazi za juu katika serikali ya Kenya, alisikika akitoa taarifa mbaya kuhusu upotevu wa nyara za serikali zilizoibiwa huku wahusika wakitokomea bila kufanikiwa kukamatwa, na kuomba askari wake kuweka ulinzi imara ili kupambana na maharamia wanaoteka meli zao.
…………………………………
Godfrey na Jonson wanafanikiwa kufika katika kisiwa kidogo kwa kutumia meli ya kijeshi inayosafiri ndani ya maji aina ya Nyambizi (submarine), na kisha kuingia ndani ya kisiwa ,kisiwa ambacho yalikuwa maficho ya Siri ya Paul bila kugundulika na mtu yeyote. "Tunatakiwa tuue kimya kimya, tukitumia bunduki tutawashitua, na bila shaka kazi itakua ngumu zaidi ",Jonson aliongea huku akitumia mikono yake kunyonga baadhi ya walinzi katika ngome ya Paul, na kisha kusonga mbele lakini bila kutegemea walijikuta wakizunguka eneo lote la kisiwa bila kugundua chochote zaidi ya kukutana na magaidi wachache wa jeshi la Paul, na kisha kuwaua. "Nasikia muungurumo wa mashine mbalimbali pamoja na magari chini ya ardhi, bila shaka kambi yao iko chini ya ardhi ",Godfrey aliongea na Jonson, huku wakiitafuta njia ya kuingia ndani ya mahandaki kwa ajili ya kumkamata Paul Agustino. "Hawa washenzi wananifatilia sana, leo ndo mwisho wao ",Paul aliongea huku akiliongoza jeshi lake kutoka nje haraka sana kwa ajili ya kupambana na askari ambao tayali wamekwishavamia eneo lao.
"Piga mpuuzi huyooo, muue kabisa ",Godfrey aliongea, baada ya Paul kukutana na mateke mawili mfululizo na kumfanya kuweweseka baada ya kutoa kichwa chake nje ya ardhi, kipigo kizito akichopigwa na Jonson. "Kila mmoja apambane kwa ajili ya kujinusuru yeye mwenyewe, pamoja na kambi kwa ujumla ",Paul alisikika akitoa amri huku vijana wake wakiwashambulia askari wawili bila mafanikio, kwani waliuawa kwa wingi bila huruma na kumfanya Paul kutafakari namna ya kutoroka eneo lile haraka sana kwani dalili ya kushindwa ilionekana wazi wazi.
"Kula naye sahani moja mpuuzi huyo, mkimbize asikuache ",Godfrey alimsihi Jonson kumfatilia Paul, baada ya kutimua mbio kuelekea mahali helikopta ilipokua imepaki huku yeye akiendelea kukata vichwa vya askari wa Paul, ambao walionekana kuwa na mbinu duni za kupambana bila kutumia siraha.
"Usi…niue, usinika…mate, naomba uch…ukue madini haya na kisha uniruhusu nitoroke ",Paul aliongea kwa maumivu makali baada ya kupigwa risasi za miguuni na Jonson, alipoonekana kukimbia sana na kutaka kutokomea hali iliyomfanya Jonson kutumia bastora yake kumtandika risasi, ili asiweze kutoroka. "Chu…kua, utakua bilion…ea mkubwa wewe usiwe mjinga, unafanya kazi kubwa lakini unalipwa pesa ya mchicha hah…aaha usichezee utajiri kijana",Paul aliendelea kumsisitiza Jonson kukubali rushwa ile,huku akimkejeli kwa maneno makali na mazito sana.
"Haraka sana potea eneo hili na uende mbali sana ",Jonson alimruhusu Paul kuondoka huku akipokea madini ya almasi pamoja na dhahabu yaliyokuwa ndani ya kimfuko kidogo na kisha kuyaficha. Huku Godfrey akiwa anakuja anakimbia haraka sana ili kumsaidia Jonson kumkamata Paul,lakin hakuamini alichokiona.
Paul alitembea kwa kujivuta haraka sana na kujitupa ndani ya helikopta, baada ya kupigwa risasi mguuni huku maumivu makali akiyasikia na kisha kuipaisha ndege kutoweka eneo lile. "Yalaa ……nakufaa ,msaada jamani ",Jonson alipiga kelele za uchungu baada ya kujichoma kisu, njia ambayo aliitumia kumdanganya Godfrey asiweze kugundua chochote kuhusu kukubali rushwa na kushindwa kumkamata jambazi katili aliyeua maelfu ya watu.
"Pole sana jikaze, usichomoe kisu kwanza mpaka madaktari wa huduma ya kwanza wafike",Godfrey alimweleza Jonson baada ya kufika eneo lile na kushuhudia kisu kikiwa tumboni mwake ,huku Paul akitokomea na ndege eneo lile,na kuamini kuwa Paul ndiye aliyehusika kumchoma kisu bwana Jonson,askari kutoka Afrika kusini.
Kutokana na Paul kuugulia maumivu,anajikuta akishindwa kuongoza ndege vizuri na kuamua kuitupa baharini,ili kuokoa maisha yake."Haya maboya ya kuogelea yatanisaidia,nisipofanya hivi ndege hii italipuka na kuniangamiza kwani imeshaanza kupoteza uelekeo",Paul aliendelea kuzungumza huku akiishusha helikopta chini tayali kwa ajili ya kuitupia baharini .
…………………………………
Ugonjwa wa kansa unaanza kuibuka usoni kwa jambazi Paul,kansa ambayo inasababishwa na upasuaji alioufanya mara mbili mfululizo kuibadilisha sura yake.Vipele vidogo vidogo vinatokea usoni kwake ,huku ngozi ya uso wake ikibadilika na kuwa nyekundu sana ……
**ITAENDELEA**
"Rushwa ni adui wa haki,piga vita rushwa"