Simulizi; "THE BLACK KILLER "

Simulizi; "THE BLACK KILLER "         (Muuaji mweusi)
      (muuaji mweusi)


Mtunzi; HAKIKA JONATHAN


Whatsup; 0629905923


*SEHEMU YA 07**


Kundi la simba wakali wa msitu wa Amazon, wanalivamia kundi la askari kwa ajili ya kujipatia kitoweo, ",Help me, please help me……",(Nisaidie tafadhali nisaidieni) mmoja wa askari wa kimarekani alipiga kelele kuomba msaada baada ya simba mkubwa kumkamata mguu na kuanza kutokomea naye porini huku likimburuza.",Pyuuu,pyuuu……pyuuu",,,Paaaah ……paaah……papaaah", milio ya bunduki za kivita za kila aina zilisikika,askari wa Kimarekani ambao walikuwa wakiongozwa na Waafrika watatu wakijalibu kumshambulia simba yule bila mafanikio.Ghafla kila askari alianza kujitetea kuokoa maisha yake kwani simba wengi walikuja kwa pamoja na kuvamia,hali iliyowafanya askari wengi kupoteza maisha na wengine kukimbia porini bila uelekeo maalumu."Help me,help… me"(nisaidieni nisa…idi…eni) sauti ya askari mmoja ilisikika ikiomba msaada huku ikiwa inapungua kadri muda ulivyozidi kwenda,joka kubwa ambalo haijulikani mahali lilipotokea lilimmeza askari yule na kuanza kumtafuna hali iliyopelekea askari wengi kutupa siraha zao na kukimbia na kuwaacha Waafrika watatu majasiri wakimpiga risasi nyoka yule na baadaye kufanikiwa kumuua.


…………………………………


Bomu lililotegwa na Paul Agustino kisiri katika nyumba ya mbao inayomilikiwa na daktari Benezeth,daktari aliyeibadirisha sura ya Paul kwa mara nyingine tena  linalipuka na kuua familia nzima ya dokta huyo."Hahaah…Sijawahi kushindwa na chochote,mimi ndio komando Paul…" Paul alicheka huku akiongea maneno ya kujisifu baada ya kuhakikisha hakuna mtu yeyote aliyekuwa amesalimika katika familia ya dokta Benezeth Christopher,na hatimaye alijihakikishia kurudi Tanzania kwani hakuna mtu yeyote ataweza kumfahamu.



"Pesa zangu zote,zililowa wakati napambana na nyoka mtoni zikiwa ndani ya begi,sitoweza kuishi huku Marekani …inabidi nirudi Tanzania " ,Paul aliongea huku akivaa miwani pamoja na suti yake nyeusi ,suti iliyomfanya kupewa jina la "THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi) kutokana na kupendelea kuivaa kila anapofanya mauaji na kisha kuanza kuitafuta njia ya kutoka msituni .

………………………………....…


Godfrey, Jonson pamoja na Jacline wanaponea chupuchupu mikononi mwa wanyama wakali wa msitu wa Amazon, huku askari wote wa Kimarekani wakipoteza maisha na wengine kukimbia. "Mmeusikia mlipuko huo wa bomu, twendeni tukashuhudie kilichotokea……tunaweza fahamu chochote ",Jonson aliwaeleza wenzake huku kila mmoja akijiweka tayali kwa mapambano muda wowote, kutokana na wanyama wakali kuwanyemelea kwa ajili ya kujipatia kitoweo


Godfrey na wenzake wanaelekea sehemu mlipuko wa bomu ulipotokea, na ghafla wanakutana na mzee aliyekuwa amevalia nguo pamoja na miwani ya Paul Agustino na kuwafanya wajulize maswali mengi, Lakini kwa upande wa Paul hakuonesha kushituka sana baada ya kuonana nao lakini alitumia lugha ya kingereza kujitetea ili asiweze kugundulika hasa pale ambapo angetumia Kiswahili.


"My name is mr Joseph, I came into this forest to conduct some research but suddenly the wild animals attacked me ……so i used bomb to kill them "(Jina langu naitwa mr Joseph, nilikuja ndani ya msitu huu kufanya utafiti … lakini ghafla nilivamiwa na wanyama wakali …kwahyo nilitumia bomu kuwaua) Paul alijitetea kwa kujiamini sana, hali iliyowafanya wakina Godfrey kushusha siraha zao walizokuwa wamemuwekea kichwani Paul na kisha kumruhusu kuendelea na safari yake.


"OK, but you have to leave from this forest, it is very dangerous " ,(sawa, lakini unatakiwa kuondoka ndani ya msitu huu, ni hatari sana) Jacline alimjibu Paul na kisha wakaanza kuelekea sehemu bomu lilipotokea kushuhudia, huku Paul yeye akitokomea na kupotea haraka sana baada ya kuruhusiwa kuondoka.  Jacline hakuweza kumtambua mzee yule kuwa ndiye Paul mwanaume pekee aliyempenda na kumpa penzi, bila kutambua kuwa aliweza kumpatia penzi muuaji bwana Paul Agustino.


"Mungu wangu, hawa wanyama aliowaua ndio hizi maiti za watu?  Na hii mashine ya upasuaji imefikaje hapa? ……Mmmh yule tuliyekutana naye atakua ndiye Paul mwenyewe kabadilishwa sura kwa mara nyingine tena, siunaona mashine hiyo ya upasuaji na pia si unaona kitambulisho chake hichi hapa kakisahau " ,Jacline msichana ambaye aliweza kuzitambua mashine za upasuaji kutokana na kupitia kozi mbalimbali za afya akiwa jeshini, aliongea huku akizitazama mashine hizo zikiwa zimeharibika kutokana na mlipuko uliokuwa umetokea …aliendelea kuwaeleza wenzake huku akionyesha kitambulisho cha Paul alichokiokota chini.


Paul anabahatisha mtumbwi uliokuwa umepaki ufukweni mwa mto Amazon, mto uliopita katikati ya msitu na kisha kuutumia mtumbwi huo kutoka ndani ya msitu huo, huku akifurahi na kujiona mshindi dhidi ya Godfrey na wenzake waliotumwa kumkamata.


*ITAENDELEA ***


Powered by Blogger.