HISTORIA YA WANGONI: Sehemu ya 3
HISTORIA YA WANGONI: Sehemu ya 3
Leo nakuelezea uhamiaji wa wangoni nchini Tanzania .wangoni walihamia tanzaninia kwa makundi makundi na miaka tofauti tofauti kundi la kwanza lilihamia Tanzania mwaka 1820 hadi kundi la mwisho lilihamia mwaka 1840.
Kabila la wangoni mwanzo lilianzia nchini Afrika kusini . ktk kabila la wangoni kulikua na ukoo mbalimbali ukiwemo ukoo wa Zulu, ukoo wa Swazi,ukoo wa ndebeke, ukoo wa xhosa ukoo wa thembu, ukoo wa bomvana, ukoo wa mpindo, ukoo wa mpondomize, na kadhalika.
Wengine wanafikili zulu ni kabila hapana Zulu ni ukoo.
Wengine wanafikili zulu ni kabila hapana Zulu ni ukoo.
Sasa nakuambia historia ya ukoo wa zulu Zulu wa kwanza aliitwa Zulu kamalandela huyu Zulu alikua ni Mtoto wa mzee kamalandela. Zulu au izulu maana yake ni peponi kwahiyo mzee kamalandela alimbatiza mtoto wake jina la zulu maana yake mahala pema peponi sasa huyu zulu kamalandela alizaa watoto wawili mmoja aliitwa Qwabes, na mwingine alimlisisha jina la zulu . kwahiyo hawa watoto wawili baba yao alipo fariki waligombana sana kugombanea madaraka walipigana sana kwahiyo zulu alikimbilia kwake na familia yake kuanzisha ukoo wake na huyu qwabes alibaki pale kuanzisha na yeye ukoo wake. Kwa hiyo ukoo wa zulu ikapita miaka hadi alipo kuja kuzaliwa shaka zulu shaka zulu KWA lugha ya kingoni maanayake ni mdudu waliokuwa wakimtumia enzi hizo kuvuruga uzazi kwa akina mama kwahiyo mama alimpa mwanae jina la shaka zulu kwa sababu Mtoto wake shaka zulu alikataliwa na babayake alie lelewa na mama tu kwa hiyo shaka zulu alikua na hasira moyoni. Kwahiyo baada ya yeye kukua na kujiunga na jeshi akawa mpiganaji mzuri na kuteka koo zingine za wangoni. Koo zilizo pigwa zilikimbia na *kukimbilia Tanzania*, zambia,malawi,na msumbiji. Kumbuka kuwa shaka zulu alifukuzwa kwenye ukoo wa kina zulu akiwa mdogo akaenda kulelewa na ukoo wa mthethwa kwahiyo alipo pigana nao ni ndugu zake ambao ni ukoo wa zulu. Kwahiyo walio kimbilia hapa Tanzania ni ukoo wa zulu orijino lengo lake apigane nao ili ateke aje kiongozi wa ukoo wake wa zulu na alifanikiwa na kwa hapa Tanzania makao makuu ya ukoo wa Zulu wa kabila la wangoni ipo kijiji cha Maposeni peramiho. Maposeni ni jina la chifu wa wangoni walio tokea zambia aliitwa Mpeseni.
Naomba nikueleze jina la songea limepatekeneje* ipo hivi: huwezi kueleza na kukamilisha historia ya vita vya majimaji na ukombozi wa nchi ya Tanzania bila kumtaja shujaa wa kabila la wangoni aitwae Nduna Songea Mbano ambae jina lake lilipewa hadhi ya kuita mji wa Songea kutoka kwenye jina la Ndonde mwaka 1906 kiongozi huyo alikua ni miongoni mwa wasaidizi nduna 12 wa *chifu wa kabila la wangoni nkosi*chifu mputa bin gwezerapasi gama, wasaidizi wake wengine walikua ni mgendera mawaso gama, kohongo magagura,mputa mkuzo gama,magodi mbamba mbano, mtekateka muyamuya tawete, fratela fusi gama,manduna wengine ni Maji yakuhanga komba,zimani moto gama,mtepa hawaya gama, na nduna mkomanile ambaye alikua ni mwanamke pekee kuwa nduna.
Nazani hapo umenielewa kabla ya mwaka 1906 songea ilikua inaitwa Ndonde
Wafuatao ni wangoni wa Zulu waliopigwa na ndugu yao shaka zulu na wakaamua kukimbia na vikundi vyao . wa kwanza kupigwa ni zwangendaba . zwangendaba alipigwa mwaka 1819 na ndo mzulu wa kwanza kubadilisha jina kutoka Nguni hadi ngoni ikawa sasa wangoni badala ya wanguni.
Wakati yupo njiani na kikundi chake kuja Tanzania kumbuka hawakua na chakura na mahitaji mengine muhimu kwahiyo kila nch walio ingia walivamia na kupora vyakura na mahitaji mengine muhimu .
Kumbuka kikundi kilikua na wapiganaji wachache walio ongozwa na zwangendaba na walikua wanamafunzo ya kivita ya kizulu walikua wanashinda vita yoyote wakiwa njiani wanakuja Tanzania walikua wanateka hadi machifu wa makabila mengine wanayo kutana nayo kwenye nch mbalimbali na ilikua lazima kuzaa na wanawake wengi ili kuongeza jeshi . kwahiyo mngoni mmoja hata akiwa na watoto 50 kwa wakati huo ilikua ni nzuri sana yani sana.
Mwaka 1840 wangoni waliweka kambi hapo kati ya ziwa nyasa na ziwa Tanganyika walimkuta chifu wa wafipa ila huyu chifu wa wsafipa hakupigwa na wangoni sababu alikua mtiifu kwa wangoni .
Kwahiyo zwangendaba alijenga mji wake hapo aliuita *mapupo* maana yake ndoto. Baada ya miaka miwili ya kukaa kwa wafipa kwa amani sasa wakaona wakavamie kwa wasukuma, na kwa wasafwa . wasafwa na wasukuma wote walipigwa na wangoni na wote hao wakawa chini ya utawala wa wangoni ikawa ngome ya wangoni . wangoni wakazaa na wasukuma ila watoto wengi wakaachwa hapo wakaendelea kuitwa wasukuma hivyo hivyo ila ilikua damu ya kingoni ilipo fika mwaka 1845 zwangendaba alifariki hapo kwenye mji wa mapupo kwa wafipa . hawakutaka wamzike hapo walibeba mwili wa marehemu zwangendaba hadi kwenye maficho ya eneo la *chapota* jirani na mto nyinaruzi .
Kwahiyo zwangendaba alijenga mji wake hapo aliuita *mapupo* maana yake ndoto. Baada ya miaka miwili ya kukaa kwa wafipa kwa amani sasa wakaona wakavamie kwa wasukuma, na kwa wasafwa . wasafwa na wasukuma wote walipigwa na wangoni na wote hao wakawa chini ya utawala wa wangoni ikawa ngome ya wangoni . wangoni wakazaa na wasukuma ila watoto wengi wakaachwa hapo wakaendelea kuitwa wasukuma hivyo hivyo ila ilikua damu ya kingoni ilipo fika mwaka 1845 zwangendaba alifariki hapo kwenye mji wa mapupo kwa wafipa . hawakutaka wamzike hapo walibeba mwili wa marehemu zwangendaba hadi kwenye maficho ya eneo la *chapota* jirani na mto nyinaruzi .
Baada ya mzee kufariki ikatokea tafurani wakagawanyika makundi matano makundi matatu wakaamua kwenda Malawi, na zambia kwenda kuwa wafugaji. Makundi mawili wakaamua kwenda kaskazini maeneo ya ziwa viktoria wakakuta waarabu wanafanya biashara ya utumwa wananunua watu. Kwahiyo wangoni wakawa wanateka watu wanaenda kuwauzia waarabu.
Mafahari wawili hawakai zizi moja wakaanza kuchapana tena wangoni kwa wangoni walio shindwa walikimbia wakakimbilia morogoro na mbeya wengine walikimbilia kaskazini waliko toka mwanzo kupitia njia ya wafipa. Kwahiyo wangoni wenye nguvu ndo wamebaki hadi leo mkoa wa ruvuma na makao makuu ya wangoni yapo peramiho kijiji cha maposeni.
Hadi hapo sema *"shikamoo wangoni"*
kosa walilo fanya wangoni kule kaskazini* wakawafundisha watu wa nyanda ya ziwa mbinu za kivita .
kosa walilo fanya wangoni kule kaskazini* wakawafundisha watu wa nyanda ya ziwa mbinu za kivita .
Baadae watu wa kanda ya ziwa walichoka utumwa wa kingoni wakaanzisha vita KWA mbinu zilezile za kingoni wangoni wakatawanyika sehemu tofauti tofauti wengine walishuka hadi kusini ( songea) na kote waliko ingia hawakujitambulisha kuwa ni wangoni wakawa wanajiita kwa kabila wanalo likuta hapo na majina yao wakaanza kubadilisha na kujiita majina ya wanyama mbalimbali wanao patikana tanzania kama sungura,mbawala,ngolombo,punda,nyani, kifaru, nakadhalika.
Sasa kikundi cha kwanza cha kingoni kiliingia Songea kutoka kaskazini kikafika Songea na kuanzisha makazi ya kudumu wengine walijichanganya na makabila mengine baada ya kukaa songea ( songea) KWA mda kikaja kikundi kingine cha wangoni kikitokea upande wa kusini kikiongozwa na Maseko kikakutana songea wakakaribishwa vizuri sana na wangoni wenzao wakakaa hapo songea maeneo ya Peramiho.
Kwa kuongezea makabila mengi hapa Tanzania yanadamu ya kingoni baazi ya makabila hayo yaliyo zaa sana na wangoni ni wasukuma,wanyakyusa,wanyasa,wamatengo, na wamanda hadi leo wangoni wanaendelea kusambaza damu ya kingoni kwa makabila mengine ila miaka hii wangoni wanatumia ustaaeabu wanabembeleza sana zamani ilikua ni lazima sio Hiyari.
Niliongelea kundi la kwanza kupigwa na kukimbia kutoka Afrika kusini ni kundi la zwangendaba lakini pia kuna makundi mengine mawili yalifuatia kundi la pili ni kundi la maseko mputa, na kundi la tatu ni la Zulu gama na mbonane tawete . kundi la Zwangwendaba lilipitia kwa wafipa,kama nilivyo sema kwenda hadi kondo,tabora,mwanza,na maeneo ya ukanda wa ziwa baadae kushuka hadi kusini . kundi la pili la maseko liliingilia kusini mwa tanzania kupitia kwa wayao tunduru kuja songea . na kundi la tatu ni la zulu gama lilipitia kusini hadi songea kwa hiyo baada ya kuchapana na wangoni kwa wangoni kundi lililo shinda ni kundi la Zulu gama.
Na niwajuze, babayake Zulu anaitwa Njeru alifia njiani wakati wa kwenda zambia waliachana njia na mwanae. Na baba yake Zwangwendaba anaitwa Mshopi, alifia njiani wakiwa wanaenda Zambia pia . ujue kabisa mizunguko hiyo yooote hawa wangoni walikua wanatembea kwa miguu.