Simulizi; NABII WA UONGO


Simulizi; NABII WA UONGO
*SEHEMU YA 12**

Hali ya wasiwasi iliwakumba wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet. Wakiwa bado na majonzi, kwani waliamini mtoto wao alikwisha kufa, na karudi duniani kama mzimu kwa ajili ya kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani. Waliamua kumuachia Mungu, kwani yeye ndiye mwenye kuhukumu, na hawakua na budi kunisamehe kwa yote niliyoyatenda na kumtoa kafara binti yao kipenzi.

"Msameheni kijana wetu, hakujua alitendalo " ,wazazi wangu waliongea kwa uchungu, huku wakiwakumbatia wazazi wake Juliet. Kwa wakati huo, mama yake Juliet alikuwa akilia tu, kwani hakuamini kama nilikuwa mchungaji mnyama na katili kiasi kile, japo kwa mwonekano wa nje nilionekana mpole na mwenye roho nzuri sana.

"Msiwe na shaka, nyie ni wazazi wenzetu, kijana wenu hafanyi haya yote kwa kupenda, inabidi tuombe sana kwa Mungu ili mzimu wake Juliet ufanikiwe kumkomboa ",yalikuwa ni maneno ya busara kutoka kwa baba yake Juliet, maneno ambayo yalikuwa ya hekima na ujumbe mzito ndani yake. Hawakutambua  mzimu wa Juliet ulikuwa umefungiwa katika gereza lililoko kuzimu, huku nyoka wakimlinda asiweze kutoroka na kuendeleza harakati zake za kunikomboa.

"Lakini tangu aondoke hapa jana asubuhi, bado hajarudi, sijui atafanikiwa? Lakini naamini ananguvu za kutosha, kwani sio binadamu wa kawaida, bila shaka atafanikiwa kumkomboa mchungaji kutoka utumwani ",baba yake Juliet, aliendelea kuongea huku akionekana kama vile hakuguswa na kifo cha binti yake, aliona kama vile yalikuwa mapenzi ya Mungu, Juliet aweze kufa na kuokoa vifo vya watu wengi ambavyo ningeendelea kuvisababisha kanisani kwangu, kwa kuwatoa waumini kafara.

…………………………………

Hatimaye baada ya kumaliza shughuli iliyotupeleka kuzimu, tulishikana mikono na kutengeneza duara dogo kama awali. Tulifumba macho, kisha upepo mkali sana, upepo ambao ulikuwa na kasi kupita ule wa awali, ulianza kutusafirisha kwa kupitia shimo kama lile tulilolitumia kusafiria wakati tukielekea kuzimu.

Safari ilikua ndefu, lakini baada ya masaa kadhaa tuliweza kutokea nyumbani kwangu. Katika chumba cha siri ambacho ndiyo sehemu ambayo safari ya kuelekea kuzimu, ilipo anzia.

"Fumbueni macho tumefika duniani ",

"Ooooh, duniani ni mbali kiasi hiki, nimefumba macho hadi nimechoka!! ",

"Ndio ni mbali sana, lakini wewe ni mzoefu wa safari hizi, ilitakiwa mchungaji Hakika,  ndiye alipaswa kuchoka zaidi kuliko wewe ",

"Sawa!, tuyaache hayo, inabidi sisi tuondoke kuelekea Bagamoyo, mchungaji abaki aendelee na majukumu yake ya kujenga chama chetu ",

"Sawa mkuu, naamini hatotuangusha ",

Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mganga, pamoja na mkuu wetu nyoka. Lakini wakati mazungumzo yakiendelea, mimi pamoja na mzee Jabir tulikua kimya tukisikiliza kwa makini mazungumzo yao, huku tukitabasamu.

Radi zilipiga mfululizo, sauti nzito za kutisha zilisikika ndani ya chumba changu cha siri. Baada ya sekunde takribani tano nilijikuta nikiwa peke yangu.Kwani kipindi radi zikipiga,ndipo mzee Jabir,mganga,pamoja na mkuu wetu nyoka,waliweza kutoweka na kurudi Bagamoyo.

Nilibaki nikishangaa tu,na kutabasamu,kwani niliamini walimwengu ni watu wenye siri nzito,hasa baada ya kumfikilia mzee Jabir.Maisha yake ya nje alionekana mstaarabu,na mwenye utajiri mkubwa sana.Lakini nyuma ya pazia,alikuwa mshirikina,muuaji na mwenye roho mbaya kupita kiasi.Japo nilijiunga na chama chao niweze kuwa tajiri,lakini kwa wakati mwingine roho ilinisuta na kujiona mwenye makosa makubwa mbele za Mungu.

…………………………………

Wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, wakiwa wameketi sebuleni wakati wa usiku, walishangazwa na kiumbe cha ajabu ambacho kiliwatokea na kuwapatia ujumbe uliowashtua sana.

"Msiogope,msikimbie! Juliet alikufa na kisha kurudi duniani kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya watu wabaya,na kisha kimuokoa Hakika kutoka katika utumwa wa shetan..Lakini kakamatwa na kufungwa kuzimu na watu wabaya,asiweze kutimiza malengo yake..Mnachotakiwa kufanya,ni kufunga na kuomba kwa siku mbili,ili nguvu zake ziweze kurudi",yalikuwa ni maelezo marefu kutoka kwa mwanaumwe aliyewatokea wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet sebuleni,mwanaume huyo alikuwa na sura ya upole huku akiwa amevalia mavazi meupe yaliyong'aa sana.Hofu iliwatawala sana, kwani binadamu yule hakuwa wa kawaida na alileta taarifa ambayo iliweza kuwashtua sana.

"Wewe ni nani,! " Lilikuwa ni swali kutoka kwa baba yangu, mzee ambaye siku zote alikuwa jasiri, kwani kupitia shughuli zake za uvuvi katika ziwa Tanganyika. Mala nyingi sana alishuhudia mambo ya ajabu,kiasi kwamba uoga ukaweza kutoweka kabisa katika nafsi yake.

"Hilo swali, muulize Juliet atakapo kamilisha kazi iliyomrudisha duniani, siku ambayo atawaaga kwa huzuni, huku nyie mkilia kwa majonzi kwani itakua ndio siku ya mwisho ya nyie kumuona mbele ya macho yenu ",mwanaume yule aliongea na kisha kupotea mbele ya macho ya wazazi wangu, huku baba yake Juliet akiangaza huku na kule kuhakikisha kama kweli kiumbe yule aliweza kutoweka.

**ITAENDELEA **
Powered by Blogger.