HABARI NA HISTORIA YA WAMAKONDE


Image may contain: 1 personImage may contain: 2 people, people smiling





HABARI NA HISTORIA YA WAMAKONDE NA TAMADUNI ZA KUJICHORA, KUJITOBOA, KUJIKATA VIDELO NA KUCHONGA MENO.
Wamakonde ni moja ya kabila la kibantu linalopatikana kusini mwa nchi ya Tanzania na kaskazini mwa nchi ya Msumbiji. Lugha yao ya asili ni kimakonde ambacho chenyewe kina mgawanyiko wake kulingana na mazingira. Yaani kuna kimakonde cha Bara yaani kile kimakonde kilichochanganyika na Kiswahili, yaani Kimalaba.
Na kuna kimakonde cha ndanindani wanakiita Kimawia, hiki ndio kile kimakonde chenyewe kabisa cha asili, yaani mtu anaweza kuongea na usielewe kama wewe sio Mmakonde wa kundi hili. Ukiwa hapa Tanzania Wamakonde wanapaikana mkoa wa Mtwara, hasa hasa Mtwara Mjini. Lakini kutokana na mabadiliko ya maisha wamakonde ni moja ya watu wanaosambaa sana japo hawasambai maeneo ya mbali.
Kwa ufupi tu neno Wamakonde/konde›msitu/ linamaana ya Watu wa Msituni, na hili jina walilipata baada ya mapambano ya kivita yaliopata kutokea maeneo tajwa takribani miaka 500 iliopita. Na kabla ya watu hawa kuitwa jina hili moja la kikabila walikuwa wakiitwa majina ya koo kulinga na maeneo yao. Siku tukipata nafasi tutajadili asili ya majina ya koo za kiafrika hasahasa Wabantu.
kwa ujumla Wamakonde wana utamaduni wao ambao ni uchongaji na tamaduni zingine kama uchezaji wa ngoma ya Sindimba, Vyakula kama Chikandanga na Ming’oko, matambiko na ususi. Lakini kutokana na kabila la Wamakonde kuingiliana na makabila mengine, kumekuwa na tamaduni ambazo wamakonde wamakuwa nazo. Hivyo kwenye makala hii tutajadili mambo kama Kujichora, Kujitoboa, Kujikata Videlo Na Kuchonga Meno.
ILIKUWAJE MPAKA WAMAKONDE WAKAANZA, KUJICHORA, KUJICHANJA,KUCHONGA MENO NA KUKATA VIDOLE?
Inasimuliwa kuwa, Mnamo karne ya 16-19 yaani 1500-1800 biashara utumwa ilishamili sana maeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki. Kulingana na masimulizi na baadhi ya maandiko yanasema kuwa, huko kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji kulikuwa na njia ya misafara ya Utumwa aliokuwa ikisimamiwa na Wamakua na baadae Wayao(rejea historia ya Wamakua). Hivyo katika kutekeleza biashara hii kulikuwa na uhuitaji mkubwa sana wa watumwa kutoka sehemu hizi. Na moja ya Kabila ambalo lilikubwa na biashara hii ni Wamakonde.
Historia inasema hivi, Kabla ya biashara ya utumwa Wamakonde hawakuwa na utamaduni wa kujichora, kujitoboa, kujikata, wala kuchonga viungo vya miili yao, isipokuwa utamaduni wao ulikuwa ni uchongaji wa vinyago. Lakini kutokana na uwepo wa biashara ya utumwa ndipo Wamakonde walipoamua kutafuta njia ya kupambana na biashara hiyo. Inasimuliwa kuwa, sifa ya mtumwa ilikuwa ni kuwa na nguvu, kuwa na muonekanomzuri na asiwe na majelaa wala alama za aina zozote mwilini.
Sasa Wamakonde waliamua kukata baadhi ya vidole, kuchonga meno, kutoboa midomo kwa ajili ya kuweka ndonya ili wafanyabiashara watakapo kuja wasiwachukue. kwani mtumwa alitakiwa kukamilika viungo vyote vya mwili na bila kuwa na majeraa. Hivyo idadi kubwa ya watumwa wa Kimakonde walikuwa wakiachwa hapo hapo, kwani mtumwa aliyekuwa akisafirishwa kwenda Zanzibar alipaswa kuwa mtu mwenye viungo vilivyokamilika.
Na kila wakati Wafanyabiashara walipokuwa wanafika kwenye maeneo ya Kimakonde hawakuchukua watumwa. Kwani walidhani kuwa,watu hawa wana ugonjwa wenye kuwatoa mapele na alama mbalimbali mwilini. Ifahamike kuwa, sio kama wafanya biashara hao hawakujua kuwa Waafrika wana utamaduni wa kujichora, ila kwa Wamakonde ilikuwa taofauti. Kwani walikuwa hawachongi kama sehemu ya urembo, hivyo alama hazikuwa nzuri na wakati mwingine Vidonda vyenye kutisha.
Na mara baada ya kuonekana kuwa endapo ukijichora huchukuliwi Utumwa jambo hilo likaendelea na likawa kama sehemu ya maisha. Na mtu ambaye hakufanya hivyo alionekana kama mtumwa. Na kwa kuwa watu waliogopa kutengwa na kuchukuliwa utumwani kila familia ilibidi wafanye hivyo japo mambo yalikuwa magumu, kwa mfano suala la kuchonga meno lilikuwa ni la hatari sana namaumivu.
Historia inasema kuwa, mara baada ya biashara ya utumwa kuisha mnamo karne ya 19, Wamakonde wamejikuta wakiendeleza utamaduni wa kuchonga meno, kutoboa ndonya na kujichora michoro usoni kwa kisu cha jadi. Na mpaka kipindi cha ukoloni ambapo Tanganyika ilikuwa chini ya Ujerumani kuanzia miaka ya 1890 mpaka miaka ya 1919, bado Wamakonde waliendeleza tamaduni zao.
Na hata kipindi cha Waingereza yaani kuanzia miaka ya 1920-1960, bado mambo yalikuwa hivyo. Lakini kuna mabadiliko, Kwani mwanzo ilikuwa ni kuzuia utumwa, lakini kwa wakati ule ilikuwa sehemu ya Urembo. Na kama ni kijana hukuwa na chochote mwilini wewe ulionekana wa ajabu na sio mjanja wa mji. Na hauendani na wakati. Hivyo hata kukawa na wasanii maarumu wa kufanya kazi hizo kwa ubunifu na kwa gharama.
Kwa sasa tamaduni hizi za kujichora, kuchonga meno,kukata vidole na kutoboa midomo, zinaonekana kufa na ukiuliza sababu ya kufa ni kwamba, tamaduni hizo si sehemu ya Wamakonde, kwani zilianzishwa kutokana na utumwa na sasa utumwa haupo.
*Habari na historia hii ni sehemu ndogo sana ya historia ya kabila la Wamakonde. Hivyo mawazo yako yanahitajika sana katika kujengwa historia hii.
Powered by Blogger.