MJUE NOAM CHOMSKY
Chomsky ni nani?? Ni mwanasarufi maarufu aliyefanikiwa kuhusisha Sarufi ya Lugha na Ubongo wa binadamu na mwili..
Nadharia ya Chomsky maarufu kama Transformational grammar ilielezea namna mtoto yeyote kwenye Lugha yeyote anavyoweza kutumia kanuni/sheria za lugha kuunda sentensi na kuwasiliana na jamii, na pia kuunda sentensi mpya bila ukomo.
Chomsky aliendelea kudai pia Kanuni zinazotawala lugha ni maalumu na huwa ni za kibailojia.Kupitia theory hii aliweza kuhusisha Sarufi na Elimu nyingine kama Saikolojia,Bailojia,Filosofia,Anthropology n.k....Toka hapa sasa Sarufi ikaanzwa kutazamwa kama elimu ya kisayansi zaidi.
Wanaofuata Mtazamo wa Chomsky huitwa Chomskyan..
Bahati mbaya siwezi kuweka kila kitu ila kwa hitimisho niseme ''Chomsky believes that the structure of language is determined by the structure of the human mind and that the universality of certain properties characteristics of language is evidence that at least this part of human nature is common to all members of species, regardless of their race or class....''
Mchango mkuu wa Chomsky kwanza ni katika isimu kwa jumla na halafu ktk taaluma ya Kiswahili. Ktk isimu kwa jumla ni kuibua swali hili: Watoto wanawezaje kujifunza lugha tunavyowaona ktk muda mfupi sana, bila kufundishwa sarufi, na kwa hatua zile zile katika kila lugha? Jibu lake ni katika nadharia tete kwamba tumeumbwa na lugha. Lugha iko katika mfumo wetu wa utambuzi. Hii inaitwa sarufi bia. Toka hapo, wanasarufi wengi wanajishughulisha na kujaribu kugundua kanuni, sheria, na ruwaza ambazo tunaweza kuziita sarufi bia na pia kwa kuangalia tofauti za lugha zinatokana na nini hasa. Chomsky aliweka kiunzi kikuu cha nadharia ya isimu ni kuweza kutoa majibu kwa swali hilo la sarufi bia kwa namna ambayo inaonesha jinsi watoto wanavyojifunza lugha kwa urahisi.
Kiswahili ni lugha moja ambazo zimechunguzwa mintarafu masuala kadha ya sarufi bia. Chomsky mwenyewe hakukichunguza Kiswahili. Wako watu kadha washirika wake na wanaofuata mkabala wake ambao wameangazia mambo kadha katika Kiswahili. Sehemu kubwa ni katika kujaribu kuangalia ni kanuni gani zinazohusika katika uundaji wa maneno. Kuna wanaosema kwamba kanuni za uundaji wa virai na sentensi ndizo pia zinatumika katika kuunda maneno. Mfano mkubwa ni jinsi tunavyoweza kuunda sentensi kwa kutumia neno moja tu la kitenzi. Basi wanaisimu wanaangazia unyambulishaji na uambishaji, nk