Simulizi; ",NABII WA UONGO ", *SEHEMU YA 04**
Simulizi; ",NABII WA UONGO ",
*SEHEMU YA 04**
Bagamoyo;
Mganga alichoka! sauti zile za ajabu zilimfanya achanganyikiwe, kwani alitumia utaalamu wake wote kumgundua mtu aliyekuwa akimtisha lakini alishindwa.
"Wewe ni nani uliyekuja kunitisha katika himaya yangu?, naomba ujitokeze ",mganga aliamua awe mpole tu, kwani kila utundu alioufanya ilikuwa ni sawa na bure. Mala achukue kibuyu ateme mate ndani yake kisha akipulize, na hakuishia hapo akachukua tunguli moja iliyokuwa karibu naye na kuiweka ndani ya kibuyu na kisha kuendelea kukipuliza bila mafanikio. Sauti zile aliendelea kuzisikia, huku akiwa hamtambui muhusika aliyekuwa akimtisha na kuamua kumuomba aweze kujitokeza.
"Lazima nitawaua, kama nyinyi mlivyoua watu wengi wasiokuwa na hatia... ",sauti ile nzuri ambayo ilionekana kuwa ya msichana mrembo, iliendelea kumtisha mganga yule, mganga aliyekuwa amekalia joka lile la kutisha ambalo lilikuwa limejiviringisha na kutulia tuli! Kama maji ya mtungini.
"Ohooo! Kumbe ni wewe, tayali umeshaliwa na nyoka wetu, halafu wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kupambana na sisi ",mganga aliongea huku akiwa ameshika tunguli zake, na kumzuia Juliet asiweze kumsogelea baada ya kujitokeza. Lakini kwa wakati ule joka la ajabu lilikuwa limelala, kwani mganga hakutaka kuliamsha liweze kumsaidia, aliona tatizo lilikuwa dogo sana kwake na angeweza kulimudu.
"Muda ukifika, utajuwa kama mimi ni mtoto mdogo au laaa! mzimu wa Juliet uliongea huku ukitabasamu, tabasamu ambalo lilionesha kutowaogopa adui zake na kisha kutoweka mahali pale kama upepo huku mwanga mkali ukimsindikiza, hali hii ilimfanya mganga aweze kutambua kuwa lolote baya linaweza kuwatokea, yeye na wanachama wake wote japopokuwa alikuwa akimdharau Juliet.
"Huyu binti kawa mzimu!!, ngoja tuone kama ataweza kupambana na sisi ",mganga aliongea huku akishusha pumzi ndefu, na kujifuta kijasho ambacho kilikuwa kinatiririka katika mwili wake.
Dar es salaam;
Nikiwa nimeketi sebuleni Kwangu nikimtafakali Juliet, huku nikiwa sitambui kama aliweza kufika mpaka Bagamoyo usiku ule ule alipotoka nyumbani kwangu na kwenda kumpatia vitisho vikali mganga, wazo jipya liliweza kunijia kuhusu wazazi wangu.
"Mungu wangu! mpaka sasa hawajafika, nini kimewatokea! ",nilishtuka ghafla kwani nilikuwa tayali nimesahau kuwa wazazi wangu walikua safarini kwa usafiri wa ndege kuja kunitembelea.
"Wameanza safari saa kumi na moja, bila shaka!mpaka sasa saa tatu usiku tayali wangekuwa wameshaikanyaga Dar es salaam ",nilizungumza bila kutambua kuwa simu yangu ilikua na missed call zaidi ya nane, huku nikiwa nimepigiwa bila kusikia simu yangu kama iliweza kuita.
"Potelea mbali!, lazima watakua salama tu, ngoja nichukue biblia nifanye kukalili mistari, sunajua tena kesho jumapili ………!",niliongea huku sauti mbili zikipingana katika fikra zangu, sauti moja ikiniambia nitazame simu yangu huku sauti nyingine ikiniambia niweze kuchukua biblia.
*******
Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu hivi,ndege ndogo ya kubeba abiria takribani sitini, iliweza kutua katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere.
"Mke wangu hapa ndo Dar, bongo bahati mbayaa! najua umezoea kusalimia mwidiwe kule kwetu kila mtu unayekutana naye njiani, lakini hapa sio Kigoma! naomba zungumza kiswahili, staki kuaibishwa ohoooo ",ilikuwa ni sauti ya mzee mjanja sana, mzee aliyezaliwa na kukulia mtaa wa Bangwe Kigoma mjini. Mzee huyu alitegemea uvuvi wa samaki katika ziwa Tanganyika, shughuli pekee ambayo ilimuingizia kipato na kuitunza familia yake. Hivyo haikuwa mala yake ya kwanza kufika Dar es salaam, kwani siku zote alisafilisha migebuka kutoka Kigoma hadi Dar es salaam.
"Sawa mme wangu, ndategeje! ",ilikuwa ni sauti ya mama yangu kipenzi, mama ambaye alinikataza nisije Dar es salaam, lakini mimi sikuweza kukubaliana naye nilifunga safari kwa lazima, huku nikiwa nimeruhusiwa na baba yangu kipenzi mzee Hamenyimana. Mzee ambaye alikuwa kama kijana, kutokana na tabia zake za kitoto alizokuwa nazo,na kujikuta akipatiwa jina la mzee mjanja na wavuvi wenzake.
"Nimetumwa na mtoto wenu nije kuwapokea …",ilikua ni sauti ya Juliet, msichana ambaye alikuwa amegeuka mzimu mala tu baada ya mimi kumuua na kisha kumtoa sadaka.Sauti ile iliweza kuwashtua wazazi wangu ambao walikuwa wanaangaza huku na kule katika eneo lote la kupokelea wageni bila kuniona, lakini baba aliweza kushauri watoke nje na kisha kuchukua taksi ili waweze kuja nyumbani kwangu kwani nilikuwa nimeshamwambia mtaa niliokuwa nikiishi.
"Mbona hakuna taksi hata moja!!, "ilikuwa ni sauti ya mzee wangu, kwani alionekana kushangaa kutokuta hata taksi ya kubeba wageni eneo nyeti kama hilo, tena katika uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa bila kutambua kuwa kulikuwa na mkono wa mtu ukisababisha yote hayo.
"Sawaa! bila shaka wewe ndiye mama mchungaji hahaa! lakini mwanzoni tumeangaza kila sehemu hatujaona taksi mahali hapa, lakini nashangaa baada ya muda mfupi tu ulipotuita na kugeuka ,tunashangaa kuona taksi kibao mahali hapa!",mzee wangu aliongea huku akiamini Juliet atakuwa mke wangu, japokuwa alionekana kushangazwa na kile alichokiona mahali pale.
"Msijali twendeni mahali salama",mzimu wa Juliet uliongea na kisha kumfanya mzee ajiulize maswali, labda kulikuwa na hatari yoyote imeweza kumtokea mwanae, hasa baada ya kukumbuka kuwa aliweza kunipigia mala tisa simu bila kupokelewa, huku mimi kipindi simu inapigwa nilikuwa nawaza maajabu ya kumuona Juliet kageuka mzimu na kisha kunitokea.
"Dereva tupeleke Mbagala kuu, "Juliet aliyekuwa amevaa gauni zuri, huku kovu la kisu likionekana kwa mbali shingoni kwake japokuwa halikuweza kuzuia uzuri wake usiweze kuonekana, alimuelekeza dereva taksi sehemu ya kuwapeleka huku mzee akionekana kutoshtukia chochote kile, kwani Juliet hakutisha hata kidogo!, alikuwa na mwonekano wa kawaida kabisa.
**ITAENDELEA **