HISTORIA YA WASUKUMA

HISTORIA YA WASUKUMA
Na jaji BULIMBO MNENE
Wasukuma limetokana na neno SUKUMA(KASIKAZINI).
Hivyo Msukuma ni mtu wa Kasikazini.
lakini Wasukuma haimaanishi tu watu wa kaskazini bali wanajumuishwa pia watu wa
1.Mashariki(Bhanakiya:Ntuzu):Mkoa wa Simiyu.
2.Kusini(Wadakama,hawa wanaweza kuwa Shinyanga ama Tabora kutegemeana upo wapi).
Msukuma wa Mwanza yeye ndio anaona yupo kaskazini hasa kuliko wote kwa hiyo akiwaita watu wa Shinyanga ni wa Kusini(Wadakama) hawezi kuwa amekosea.Japo ukiwa Shinyanga napo utawasikia watu wa Shinyanga wakisema wao wapo kaskazini hivyo ni wasukuma na kusini yao ndio kuna wadakama(Mkoa wa Tabora ndio upo kusini). Inajulikana zaidi kuwa Wenyeji wa Tabora ni Wanyamwezi.Usukumani hakuna kabila la Wanyamwezi bali wanaitwa Wadakama. Japo ukifika Tabora wilaya ya Sikonge na Urambo hasa yenye Wanyamwezi huku wilaya zingine zikiwa kwa kiasi kikubwa zimekaliwa na wasukuma waliotokea Shinyanga na Mwanza miaka mingi iliyopita.
3.Magharibi(Bhanang'weli). Huku utakutana na Wasumva/Wasumbwa. Hawa ndio wanachukua sehemu ya watu wa Magharibi.
Wasumbwa kama ilivyo kwa Wanyamwezi wao wanaonekana kama si sehemu ya Wasukuma lakini ni sehemu ya wasukuma na karibu kila kitu kinafanana kuanzia lugha,mila na desturi na utamaduni wao.
4.Kaskazini(Wasukuma).
Kwa hiyo Wasukuma wamegawanyika katika pande kuu nne za dunia na jina la pande moja ya Kaskazini ndio lililochukua nafasi ya pande zingine zote.
Kabila la wasukuma linapatikana mikoa mitano Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu na Tabora.
Japo wanyamwezi asili kabisa ni wachache na wanachukua wilaya ya Sikonge na Mirambo, wilaya zingine zikikaliwa na Wasukuma kuanzia Igunga na Nzega ama mchanganyiko kama Uyui.
hii ni mikoa asili ambayo wasukuma wanatokea.
Wasukuma wengi pia wanapatikana katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Morogoro.Ambapo wamehamia huko kwa ajili ya kufata kilimo na malisho ya mifugo.
Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi nchini Tanzania likifuatiwa na Kabila la Wahaya na baadae Wachagga
MILA NA DESTURI.
Kama ilivyo makabila mengine ya Kiafrika wasukuma wana mila zao na tamaduni zao.Mila za wasukuma zimegawanyika sehemu mbili.
1.Mila za koo ama familia.Hizi hazifanani kabisa kati ya koo na koo.
2.Mila za jumuiya. Hizi zinafana na zinajulikana kwa wanajumuiya/wanachama bila kujali ni wasukuma wa Mwanza,Simiyu(Ntuzu),Tabora(Wanyamwezi),Shinyanga ama wamagharibi(bhanang'weli=wasumbwa).
Jumuiya za mila zipo mbili.
(i)Bhakango,hawa wanafanya kitu kinaitwa bhukango.
Mila hizi zinahusu wazazi na watoto wa aina:-
kwanza watoto mapacha.
Ukizaa watoto mapacha ni mkosi hivyo lazima ufanye bhukango kuondoa mikosi.wa pili ni watoto waliozaliwa wametanguliza miguu(Kashinje/kashindye).
Mtoto akitanguliza miguu kwa maana ya kuzaliwa kinyumenyume huo ni mkosi na lazima ufanye bhukango.Wazazi wa mtoto ama watoto mapacha hupelekwa kufanyiwa matambiko maeneo kama mtoni na huko wao watakuwa uchi kabisa huku wakifanyiwa hayo matambiko na wanajumuiya wenzao.
Katika matambiko haya matusi yote husemwa na ndio lugha rasmi inayotumika hata kama wakiwa njiani wanarudi.Matusi ya kutaja majina viungo vya siri hutamkwa bila aibu yoyote mwanzo mwisho.
Kwa wasioshuhudia siku ukibahatika kukutana nao barabarani wanatukana matusi makubwamakubwa njia nzima wala usishangae.
Kwa kawaida kama si mwanajumuiya wa Bhukango hata ukizaa mapacha ama kashinje mila hii hufanyi.
Labda mpaka upate mikosi ama matatizo na uelekezwe na wataalamu wa mila kuwa hao mapacha ama huyo kashinje ndio tatizo basi utalazimika na wewe kuwa mwanachama/mwanajumuiya.
Ili uwe mwanachama sharti uzae mapacha,kashinje,ama wewe ni pacha,ama waliokutangulia ni mapacha mfano ni Shija ambaye huzaliwa baada ya mapacha naye ana sifa ya kuwa mkango.
(ii)Bhasweji, hili ni kundi la pili la wanamila wa kisukuma.
Kundi hili ndio hushughulika na matambiko ya kila aina iwe ni kuondoa mikosi,neema n.k
Hapa si lazima uwe mwanachama wa moja kwa moja kufanya matambiko haya. Ukipata mikosi,laana nk na njia pekee ni ya kuondoa mikosi hiyo ni matambiko basi hawa mabwana watakuja kukufanyia hata kama si mwanachama.Ila matambiko na ngoma watacheza na kufanyia kwako.
Chakula chao hawali kitu kingine zaidi nyama. Fanya ufanyavyo nyama isikosekane. Kama unapika ugali mboga ni nyama. Kama wali mboga ni nyama.Na wanatabia huwa hawaondoki na wanaweza kukaa kwako hata mwezi wanatambika tu.Usipopika nyama siku hiyohiyo wanaondoka.
WASUKUMA NA NDOA.
Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitaala(mke zaidi ya mmoja).
Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahali ya ng'ombe kati ya ng'ombe 7 mpaka 20. hii ni kawaida.lakini mahali inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 kutegemeana na mazingira ya anaeolewa na muoaji.Lakini kubwa kuliko yote ni uzuri na tabia nzuri ya mwanamke.
wasukuma huzaa watoto wengi. Kwa wastani watoto kati ya 6 mpaka 8 ama zaidi na hao ni wa mama mmoja
WASUKUMA NA WANAWAKE WEUPE.
Ni kweli wasukuma wanapenda wanawake weupe ila weupe natural.
Lakini hili la wanawake weupe si la Wasukuma peke yake bali ukweli ni asimilia kubwa ya wanaume wa makabila yote wanapenda wanawake weupe ila wasukuma ndo wanasingiziwa zaidi utazani wengine hawawapendi wanawake weupe
NGOMA.
Wasukuma wana aina ya ngoma za burudani zaidi ya 15.
USHAMBA WA WASUKUMA.
Kuna mambo mawili hapa.
1.Wasukuma wana watani wao.
Ushamba wa msukuma umejengwa juu ya watani wa msukuma. Ambapo ni kawaida sana kwa makabila watani wa msukuma kumtania msukuma japo utani unaweza kuwa unabeba sehemu ya ukweli kwa anaetaniwa ila haimaanishi ndo wasukuma wote wapo hivyo.
Nje ya makabila watani wa msukuma hata makabila mengine yanatania wasukuma hasa kutokana na ukweli kuwa msukuma kwa kiasi kikubwa hanaga tatizo na jamii yoyote ukiacha wamasai waliokuwa wanatuibia ng'ombe zetu enzi na enzi japo hili sasa ni kama halipo.
2.Maisha ya kijijini. Kama ilivyo makabila mengine wasukuma wengi zaidi wanaishi vijijini na maisha ya vijijini yanafanana kwa karibu makabila yote nchini. kama ni uduni wa mavazi na malazi yanafanana na watu wa vijijini katika jamii zingine,Kama ni kutoyafahamu vyema maisha ya mjini basi ni sawa na watu wa vijijini katika makabila mengine hata kwa watani zetu wagogo.kwa hiyo ieleweke kuwa kila kabila lina washamba na wasio washamba kutegemeana na aina ya ushamba na mazingira ya huyo mshamba
Powered by Blogger.