Simulizi; "THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi)



Simulizi; "THE BLACK KILLER "          (muuaji mweusi)



 Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU YA 15**


Baada ya Paul kuitupa ndani ya maji ndege ya kijeshi alipokuwa akitoroka,kwani alishindwa kuiongoza vema kutokana na maumivu ya miguu baada ya kupigwa risasi.Maisha yake yanazidi kuwa hatarini, kwani Samaki mkubwa aina ya papa, akiwa mwenye njaa kali anakutana uso kwa uso na Paul akijitahidi kuogelea bila mafanikio. "Oooh ……aim dead! Aim not able to run away "(ooh……nimekufa!  Sina uwezo wa kukimbia)  ,Paul alizungumza kwa huzuni akiwa amekata tamaa ya kupona kutoka mikononi mwa samaki yule, samaki ambaye alikuwa akija kwa kasi kubwa uelekeo ambao Paul alikuwepo ili kumlalua na kujipatia chakula.


Lakini bila kutegemea, Paul alishangaa kuona papa yule akishambuliwa kwa mishale pamoja na siraha nyingi za kijadi, na kumfanya kugeuka kutazama watu walioweza kufanya hivyo bila mafanikio, kwani nguvu zilikua zimeshamuishia kabisa na kujikuta akipoteza fahamu. "Haraka shukeni kwenye meli mkamkomboe, mkichelewa atazama na kupoteza maisha ",kundi kubwa la wavuvi ambao haikujulikana wametokea wapi, waliamrishwa na bosi wao kujitupa ndani ya maji na kisha kumuokoa Paul,
aliyeonekana kabisa angeweza kupoteza maisha asipopata msaada, na kisha kuanza safari ya kuelekea bara akapatiwe matibabu haraka sana ili kuyaokoa maisha yake.


Kundi la wavuvi wa Kitanzania waliomuokoa Paul, wanafika pwani ya Bahari ya Hindi na kuamua kutoa taarifa  kituo cha polisi, na kisha kujipatia mamilioni ya pesa kutoka kwa raisi wa Tanzania, kwani Paul aliweza kutafutwa muda mrefu na serikali bila mafanikio. Lakini kipindi yote hayo yanatokea, wavuvi wale hawakuweza kuamini kama waliyemuokoa na kumripoti kituo cha polisi ndiye jambazi aliyekuwa akitafutwa duniani kote.


………………………………


"Samahani Godfrey na serikali Tanzania, pamoja na serikali yangu ya Afrika kusini, nilipokea madini mengi sana kutoka kwa Paul na kumuacha akitoroka huku mimi nikijichoma kisu, nisiweze kugundulika ",Jonson alizungumza kwa huzuni sana huku machozi yakimtoka,akiwa kitandani akijuta kwa kujichoma kisu, kwani kiliathiri ini lake na hivyo angeweza kupoteza maisha muda wowote. "Usilie ndugu yangu, yote ni mipango ya Mungu ",Godfrey alizungumza na kumfuta machozi Jonson, huku akipokea madini yale tayali kwa ajili ya kwenda kuikabidhi serikali, madini ambayo yaliweza kuuzwa na kuwalipa fidia wahanga wa mlipuko ulioua maelfu ya raia.


…………………………………


Mahakama ya hakimu mkazi kisutu inafurika maelfu ya watu wakishuhudia hukumu ya jambazi sugu Paul ikitolewa, watu wakiwa na hasira kali wanamtukana Paul huku wengine wakimpiga na viatu vyao, alipokuwa akiingia mahakamani. "Asipohukumiwa kifo, tutamuua wenyewe kwa mikono yetu, "raia mmoja aliongea kwa hasira na kumpiga Paul kwa kiatu chake kichwani,na kusababisha damu nyingi kumvuja kwani ngozi yake ilikuwa laini sana sababu ya maradhi ya kansa aliyonayo.


"Baba kwanini ulikuwa muuaji kiasi hiki, nikikua nitahakikisha nakuwa askari mwema, nipambane na waovu kama wewe na kulipa wema kwa mabaya yote uliyowatendea walimwengu " ,mtoto mdogo wa Paul na Jacline, anazungumza kwa huzuni akiwa mahakamani akishuhudia hukumu ya baba yake ikitolewa, baada ya kuelezwa kila kitu na Godfrey japo alikuwa na umri wa miaka saba tu.



"Mahakama inatoa hukumu ya kunyongwa mpaka kifo kwa Paul Agustino, na iwe fundisho kwa wengine ",jaji alisikika akitoa hukumu kwa Paul, ambaye alikuwa amenyongonyea sana kwa wakati ule kutokana na kansa iliyoiharibu vibaya sura yake kwa vidonda ,lakini kwa upande wa wananchi, walishangilia kwa furaha baada ya kusikia hukumu ikitolewa.


"Tha…nk you Go…d, i can die now (asa…nte mun…gu, ninaweza kufa sasa) Jonson akiwa hospitalini amelala kitandani akishuhudia hukumu ya Paul ikitolewa na kurushwa katika televisheni, anatabasamu baada ya kufurahishwa na hukumu ile, huku roho yake ikiuacha mwili na kupoteza maisha.



"Mwanangu nitakukumbuka sana, ishi vizuri na walimwengu na usiwe kama mimi baba yako ",Paul akiwa amemkumbatia mwanaye, analia kwa uchungu na kumpati wosia kabla ya kwenda kunyongwa mpaka kifo. "Usjali baba yangu, nakuahidi sitakuwa kama wewe ",mtoto wa Paul alimwitikia baba yake kwa uchungu huku akiishika sura ya baba yake, iliyokuwa imeharibika vibaya sana.



*MWISHO ***

"Kila jambo baya au zuri, lina malipo yake "


*simulizi hii ni ya kutunga na yenye visa vya kubuni, haina ukweli wowote*

Powered by Blogger.