Simulizi;"NABII WA UONGO"


Simulizi;"NABII WA UONGO"
*SEHEMU YA 07**

Watu walifurika kanisani kama kawaida, lakini siku hii ya jumapili,watu walikuwa wengi kuliko siku zote. Waandishi wa habari hawakutaka kupitwa na chochote kile, siku hii idadi yao iliongezeka tofauti na jumapili zilizopita.

Siku hii ilikuwa siku ambayo taarifa kuhusu Juliet kupotea, ilitakiwa kutangazwa huku mimi kama mchungaji nikielezea jinsi msichana huyu mrembo alivyopotea katika mazingira ya kutatanisha.

"Jumapili hii watu wamekua wengi sana ",

"Watu wanataka kusikia kilichotokea mpaka mtoto wa mzee wa kanisa akapotea !",

"Mimi siamini kama amepotea! binti yule ni msomi na tayali ni mtu mzima, hawezi kupotea kirahisi ",

"Ngoja tusubili kushuhudia mchungaji atasema nini! japo wengine wanasema  inawezekana kahusika kwa namna moja au nyingine! ",

Yalikuwa ni majibizano ya baadhi ya waumini waliokuwa karibu kabisa na meza yetu .Meza ambayo tulikuwa tumeketi viongozi wa kanisa.

"Waaoh!  today might be the blessed Sunday ever seen! (Waaooh! Leo inaweza kuwa jumapili ambayo imebarikiwa sana na haijawahi kuonekana), ilikuwa ni sauti kubwa ya mzungu mmoja, mzungu ambaye alionekana kutotambua chochote kuhusu wingi wa watu waliofurika kanisani siku hiyo.

"Mungu ni mwema leo, kesho na hata milele. Najua wengi wenu mnamfahamu Juliet, napenda kusema kuwa, mimi kama kiongozi wa kanisa sijafurahishwa na upoteaji wake. Mpaka sasa hatujui yuhai au amekufa, tunaomba kanisa zima tushirikiane bega kwa bega kumtafuta ",

"Mtoto wa jirani ni wa kwako pia, kazi ya kumtafuta Juliet siyo ya mchungaji, au wazazi wake peke yao! Hata wewe unaweza changia hata kwa maombi inatoshaa! ",

Makofi yalisikika, walikuwa ni waumini wakinipongeza kwa maneno mazuri niliyokuwa nikiongea. Hawakutambua siri nzito iliyokuwa kifuani kwangu, siri ambayo pengine muda wowote ingewekwa wazi na mzimu wake Juliet mala tu atakapokanyaga mguu wake kanisani kama jitihada za kumzuia zikigonga mwamba.

"Na…na…na taka nyama ya binadamu, nataka nyama! nataka chakula ",ilikuwa ni sauti ya nyoka wa ajabu, nyoka ambaye alikuwa na uwezo wa kuongea lugha yoyote ile. Maneno yake ya kutisha, yalinifanya nisitishe kabisa kuendelea kuongea.

Nilishangaa sana kwani baadhi ya watu waliokuwa wakinipigia makofi, walisitisha makofi yao baada ya kusikia sauti ya ajabu kutoka nyumbani kwangu.

"Mchungaji hapa kuna kitu sio bure, maombi ni siraha pekee ya kuitumia! ",alikuwa ni baba yake Juliet, mzee ambaye aliamini kabisa kuwa ipo siku ataweza kumuona tena mwanae. Alinyenyuka na kisha kuninongoneza maneno hayo, sikuwa na budi kukukubaliana naye ili wasiweze kugundua kuwa nilihusika asilimia mia moja na sauti za kutisha za kiumbe kilichokuwa kikisikika na kupiga kelele nyumbani kwangu.

"Hapana baba!, maombi yenu hayatasaidia chochote ,mimi nimekufa lakini kwa macho yenu hamtaweza kuamini!, mimi ni mzimu wa Juliet na wala sio Juliet,,, chanzo cha yoteee, ni mchungaji mnayemwona kama nabii kwenu, kanitoa sadaka kwa miungu yake ili aendelee kuwa tajiri, maarufu na kupata waumini wengi katika kanisa lake hili ,huyu sio mtumishi wa Mungu bali mpinga kristo!!! ",

Ilikuwa ni sauti ya Juliet aliyeingia kanisani akiongozana na wazazi wangu, na kuacha maswali mengi kwa umati wote uliokuwa kanisani kwangu.

Bagamoyo;
     Mganga pamoja na mzee Jabir hawakuamini kilichotokea, hawakuamini kama Juliet alifanikiwa kufika kanisani kwangu akiwa salama japokuwa walitumia uchawi wao wote kumzuia bila mafanikio.

Walituma radi, lakini radi ziliwarudia wao wenyewe na alimanusura ziwaue kabisa. Hawakukata tamaa, walijaribu kwa mala nyingine na kumtumia Juliet moto mkubwa na wa ajabu sana, lakini bila kutegemea moto ule uliweza kuwarudia tena na kuwaunguza wao japokuwa walifanikiwa kuuzima bila kupata majeraha yoyote. Japokuwa nguo walizovaa ziliteketea kwa moto huo, na kuwaacha wakiwa kama walivyozaliwa.

Juliet alikuwa na nguvu za ajabu, alifanikiwa kufika kanisani japo wazazi wangu walionekana kumuogopa sana tofauti na awali. Kwani walimshuhudia alivyokuwa akipambana na radi pamoja na moto uliotumwa kuwateketeza wakiwa ndani ya gari wakielekea kanisani kwangu. Waliamini kabisa Juliet hakuwa binadamu wa kawaida, na pengine alikuwa jini, lakini kilichowashangaza Juliet alikuwa ameshika biblia,jambo ambalo lisingewezekana kwa jini.Na kuwafanya waendelee kujiuliza maswali mengi bila majibu yoyote.

"Juliet ana nguvu kutushinda sisi,lakini Nyoka wetu ndiye mwenye uwezo wa kupambana naye!hatuna budi kusababisha ajari ili nyoka apate chakula na kumuongezea nguvu za kupambana na Juliet",mganga alitoa ushauri,ushauri ambao ulikubaliwa na mzee Jabir  kwa asilimia mia moja.

**ITAENDELEA**
Powered by Blogger.