HADITHI-THE WORLD OF MY OWN, _6

Image may contain: 2 people, people standing and text


(Ulimwengu wa ya kwangu) 
ILIPOISHIA.
Jenerali alimwachia akaita tena mabinti wengine wawili ndani, wakaja nao kwa haraka sana. Walikuwa ni wasichana waliokuwa wanavutia si haba. Baada ya kufika alitoa agizo huku machozi yakimtoka.
"Yule Mwananke wangu, naombeni mniandalie vizuri kwani nahitaji iwe starehe yangu kwa siku nzima ya leo, nampenda sana.
SONGA NAYO.
"Hapana waache tu, naomba warudi walikotoka!"
Baada ya kuyasikia maagizo ya Jenerali Yule Alisha alishituka sana, palepale akakataa na kuomba wale Mabinti wenzake warudi inje, alijua anaweza kusababisha mauaji mengine tena kwa wenzake bila kutarajia.
"Kwanini Mpenzi wangu!?"
Taratibu kabisa Jenarali aliuliza.
Alisha hakujibu kitu masikini, aliamua mwenyewe akalivua gauni lake, pamoja na nguo yake ya ndani, akabaki kama alivyozaliwa.
"Naomba uwatoe hawo inje tafadhali!"
Alisha kwa ulimi wake alitamka. Ilimbidi akubaliane na hali, mambo yalikuwa yashamuwia magumu kuona watu wakifa huku wakiwa hawana hatia yeyote.
"Tokeni ndani Mwangu! "
Jenerali aliamrisha, hata yeye hakutaka kumkwaza Alisha.
Baada ya kuwatoa Mabinti ndani ya nyumba yake, Bosi yule wa kikosi cha msituni alimsogelea alisha ambaye alikuwa amesimama kando ya kitanda, alipomkaribia alimpigia magoti kisha akakiegesha kichwa chake katika tumbo la Alisha. Alisha alishindwa kumzuia alibaki kusikilizia mwanaume yule atamfanyia nini, Bila kusubilia Mwanaume alianza kuuonesha utundu wake wa kibabe katika Mwili wa Alisha, hakutaka kubaka kama alivyokuwa amezoea kubaka tena kwa kuamrisha tu. Aliipikicha mikono yake kila sehemu ambayo inatakiwa kushikwa katika maungo ya mwanamke kama sehemu ya kumuweka tayari ili kulifaidi tunda la Roho. Ingawa alikuwa hakujipanga kwa kitendo hicho Alisha naye alikipokea na kuitikia Wito wa Jenerali yule aliyekuwa amepinda uso, kisha akaanza kuitika kwa miguno laini na hadimu kusikika holela isipokuwa sehemu nyeti hasa chumbani au sehemu Faragha yenye kufanyika tukio hilo. Ingawa Jenerali alikuwa mkorofi, lakini katika swala hilo alitumia ufundi wa hali ya Juu mpaka kumuweka Alisha katika hali sitahiki, alitumia dakika 20 kisha akaianza kazi ya kujipa burudani mwenyewe kwa kulizamisha jembe Ardhini. Kitendo hicho kilikuwa burudani pande zote mbili kwani maandalizi yalikuwa yakutosha, dakika tano tu jamaa alikuwa kaisha maliza tuta la kwanza analianza la pili. Wakiwa katika Shughuri yao nje ya Jumba msituni kuliskika milio ya Risasi na Miungurumo ya Herokopita ikipita Juu ya Anga lao, muda huo huo jenerali hakuendelea na zoezi nyeti alisitisha na kuikimbilia bunduki yake nzito na kutoka inje, tayari kikosi chake kilianza kushambuliwa na Jeshi la Kutoa msaada la Umoja wa Mataifa, wanajeshi wengi wa Jeshi la Msituni walipigwa risasi na kufa pale pale, wengine walianza kukimbia hovyo hovyo kukwepa kufa kizembe, hata Jenerali naye alipotoka hali ilimshinda hakuwa na uwezo wa kuwakusanya wanajeshi wake, alirudi ndani haraka. Ndani alimkuta Alisha kaisha vaa nguo zake naye akiwa katika hali ya maandalizi ya kutafuta pakutokea ili kukiepuka kifo. Jenerali yule mwenye maguvu alimshika mkono Alisha na kutoka naye inje na kuanza kukimbilia sehemu salama ili kukiepuka kifo, wakiwa katika mbio za kasi Mara Bomu lilirushwa karibu yao, mripuko wa Bomu hilo ulisababisha kila Mmoja kuruka na kuanguka upande wake. Jenerali ndiye alikuwa wa kwanza kuamka na kuanza kumtafuta tena Alisha, hakufanikiwa kumuona, ndipo yeye mwenyewe aliamua kukimbia na kumwacha Alisha upande mwingine akiwa anagagaa kwa maumivu makari aliyokuwa akiyapata baada ya kuanguka chini. Muda huo huo kikosi cha wanajeshi wa kutoa msaada kutoka Umoja wa mataifa kililitawala eneo zima la msitu, kazi iliokuwa inafuata pale ni kuwakusanya watu ambao waliwahofia kuwa Bado ni wazima, bahati nzuri waliwakuta baadhi ya watu waliokuwa wametekwa pamoja na Alisha kutoka mipakani mwa inchi hizo mbili wakiwa wazima halafu wamejikusanya sehemu ambayo walikuwa wamewekwa kama mateka. Kikosi hicho kilizidi kutafuta maeneo hayo ya Msituni, upande mwingine walimkuta Alisha akiwa bado anaangaika kunyanyuka, walimbeba na kumuweka pamoja na wengine, kwakuwa alikuwa na majeraha usoni na miguuni Dkt wakike aliyekuwa ameandamana na kikosi hicho cha umoja wa Mataifa, alianza kumpa huduma ya kwanza. Baada ya kumaliza zoezi hilo waliwakusanya watu wote pamoja kisha wakaanza kuwaongoza kutoka katika Msitu huo kuelekea katika eneo la wazi kwa ajili ya usafiri ili kuwapereka sehemu ya makazi salama. Walitumia saa zima kabisa kuwavusha Raia wale kutoka eneo la hatari mpaka sehemu ambayo usafiri ulikuwa ameandaliwa, kulikuwa na maroli makubwa ya kijeshi yameandaliwa tayari kwa kuwabeba, Alisha akiwa miongoni mwao walibebwa wote wakaeneo katika magari mawili ambayo yalikuwa makubwa, kisha safari ya kuwapereka sehemu salama ikaanza huku wakisindikizwa na wanajeshi wa Umoja wa mataifa. Safari yao ilifikia kikomo katika kambi kubwa ya wakimbizi ya Nyarugusu Iliyoko Kasuru Mkowani kigoma. Hapo ndipo makazi mapya ya muda kwa Raia wale yalianza upya kama wakimbizi wa kivita kutoka Kongo.
*******
Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Uzuni sana kwa Alisha, akili zake zote zilibadilika na kuwa za kioga, aliyahofia maisha yake, alikuwa amekaa pembeni kabisa akiwaza, matukio yaliyomkuta yote yalianza kujirudia kichwani mwake, hakuwaza kingine zaidi ya vifo vya wazazi wake, ambavyo vilikuwa vya udhalilishaji, bado mdogo wake naye haijulikani kama ni marehemu au Raha, wakati huo huo matukio ya kubakwa nayo yalizidi kumfuata, kitendo cha kuwaona mabinti wawili wanapigwa risasi mbele yake nayo yalikuwa yakijirudia kichwani mwa Alisha kwa kipindi hicho, wakati wote machozi yalikuwa yakimmiminika kwa wingi, hakuwepo Mtu wa kumliwaza kambini pale, alikuwa yeye kama yeye akijiliwaza na mawazo yake. Majeraha ya kuanguka kutokana na mripuko wa bomu yalikuwa yamejichora usoni mwake pamoja na miguuni. Kwa wakati huo upweke ndio ulikuwa faraja moyoni Mwake.
Akiwa amekaa hivyo hivyo akiendelea kuwaza , huku hana hili wala lile, Alisha alishituka na kugeuka haraka baada ya kuguswa mabegani. Macho yake yalikutana na kijana mtanashati kweli kweli. Kijana yule alikuwa amevalia suti nzuri ya mvuto, huku akionekana si miongoni mwa watu masikini.
"Pole!"
Sauti nzuri ya mvuto wa kitanashati ilimtoka kijana Yule.
Alisha hakuijibu badala yake aliona kuwa kuna usumbufu ndani yake, au huyo kijana huwenda akawa ni Mmoja wa watu wabaya ambao wametumwa kumuua kabisa. Hapo hapo alitaka kuzipiga hatua ili kumuepuka kijana yule, lakini kabla hata mguu wake wa kwanza haujatua chini baada ya kuurusha kama tambo ya kwanza ya kupiga hatua, kijana yule alimshika mkono.
Kitendo kile kilisababisha alisha kumuhofia zaidi kijana yule, hapo akaifungua midomo yake tayari kupiga kelele, kabla hata sauti haijamtoka Alisha, kiganja cha kijana yule kilikuwa tayari kimeufikia mdomo wake na kuuziba.
"Tafafhali naomba usipige kelele, mimi ni Mtu mwema kwako!"
Kijana yule alisema, alionekana ni shapu kweli kweli.
Baada ya kusema hivyo alilazimika kumuachia Alisha akawa huru.
"Mimi ninaitwa Rameck Mtatiro, ni mfanya biashara mkubwa sana katika taifa hili la Tanzania, huwa ni kawaida yangu kufika hapa katika kituo hiki mara kwa mara kwa ajili ya kutoa misaada na kuwapa pole Watu wote hapa, kama unavyoona kule yale ni magari ambayo yamebeba mizigo kama chakula, nguo kwa ajili ya watu wa hapa"
Kijana yule alisema huku akionesha upande wa pili ambako kulikuwa kuna Magari mawili makubwa aina ya fuso yaliyokuwa yamebeba shehena ya vitu huku utingo wakiwa wanavipakuwa. Pembeni yake kulikuwa na Gari moja ndogo nzuri aina ya Range rover sport iliyokuwa na rangi nyeusi.
"Lile Jeusi ni gari langu..........labda nikupe pole kwa yaliyokukuta, haya majeraha, hayakuumizi?"
Yule kijana alisema huku akiipereka mikono yake katika uso wa Alisha. Alisha aliukwepesha uso wake huku akionekana kuchukizwa na kauli ya kijana huyo, kwani aliona kabisa ni majeraha halafu anauliza tena kuwa majeraha hayaumizi. Alisha alianza kuzipiga tena hatua ili kuondoka.
"Samahani naomba nikujue?"
Sauti ya kijana yule ilisikika ikisema. Alikuwa ni kijana mdogo mdogo tu, umri wake ulikuwa uzidi umri wa miaka 24.
Alisha alimgeukia lakini hakumjibu chochote.
"I am the son of president in this country (mimi ni kijana wa Rais katika taifa hili"
Kijana yule aliyejitamhulisha kwa jina la Rameck alisema.
"So"(kwahio)
Alisha alisema. Aliijua na kuielewa lugha kingereza vizuri.
"I will help you"(nitakusaidia)
"For what?"(kwa lipi?)
"You will see when you are accepting my request to leave with you here"(utaona utakapokubali ombi langu la kuondoka nawe hapa)
"The son of president! Bado hutonibeba!"
Alisha alisema.
"Unakijua kishwahili"
"Hiyo ni Lugha ya Africa mashariki na kati"
Alisha alimjibu Rameck, alikuwa anazungumza kishwahili pia tena kilikuwa kimenyooka vizuri sana.
"Poa, lakini uliwahi kufika Tanzania hapo Kabla"
"Ndiyo, nilifika na Baba yangu, tulikaa wiki mbili kabisa, kipindi hicho tulikuwa kwenye mapumziko katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti"
"Mwaka gani ilikuwa?"
"Ilikuwa Mwaka 2003 nilikuwa na umri wa miaka kumi, halafu Mdogo.........! "
Hata hakuimalizia kauli yake machozi yalimdondoka pale pale, na kushindwa kuendelea kuzungumza. Kitendo cha kumtamka mdogo wake ilikuwa kama kayakumbushia machungu.
"Naomba usilie, najua lazima kuna makubwa ambayo yamekukuta, tena yanaumiza sana, lakini hupaswi kuyaweka kichwani mwako mpaka sasa, jaribu kuyasahau hayo"
Rameck alisema tena, wakati huo alimsogelea Alisha na kumkumbatia, tayari hata yeye alishajua kabisa kuwa lazima ndugu zake Alisha pamoja na wazazi wake Alisha walikuwa wameuawa katika mapigano yaliyokuwa yanaendelea katika mataifa ya Congo, Muda huo Bado Alisha alikuwa ajajitambulisha kwa kijana yule.
"Naomba nikusaidie tafadhali kama upo tayari, mimi niko tayari kukutorosha hapa kambini, halafu nitakupereka Hospitali, utatibiwa haya majeraha yako, kisha nitajitahidi kuirudisha furaha yako"
Rameck alisema. Maneno yake hayakuwa na ushawishi wowote kwa Alisha, kwani matukio ambayo yalikuwa yashamkuta yeye aliona kuwa hasitahili kumpa Moyo wake Mtu mwingine, alikuwa kaisha dhalilishwa kwa kubakwa halafu sasa umri wake ulikuwa ni mdogo bado ulikuwa hujafaa kujihusisha na maswala ya kujamiana, halafu kilicho muumiza zaidi ni kuhitaji kulipa kisasi, kwahio kukubali kwenda na Rameck yeye aliona kama ni sehemu ya kukwamisha makusudio yake. Kwa kipindi hicho alikuwa anawaza atoroke arudi tena kongo katika jeshi la Msituni akajifunze kuua na Jinsi ya kuitumia bunduki ili iwe rahisi kwake kwenda kukilipa kisasi kwa Rais wa Inchi yake Cardin Solomon. Alikuwa tayari akaishi kama mpenzi wa Jenerali Kabanga lakini ajue namna ya kuua, ila si kuishi Maisha tofauti na kuua.
ITAENDELEA. 
Powered by Blogger.