HISTORIA YA UHUSIANO WA MAKABILA YA WAMATUMBI NA WANDENGEREKO
HISTORIA YA UHUSIANO WA MAKABILA YA WAMATUMBI NA WANDENGEREKO
Kabla sijaanza kuwaletea historia yao ya makabila haya mawili,
Ikumbukwe wamatumbi wanapatikana katika wilaya ya Kilwa haswa kwenye tarafa ya kipatimu na tarafa ya Miteja.
Wandengereko wanapatikana wilaya ya Rufiji ila kwa sasa tunaweza kusema wanapatikana wilaya ya Rufiji, Kibiti na pia Mkuranga.
Sasa tuendelee na historia yetu,
Hapo zamani inasemekana wamatumbi na wandengereko walikuwa wakiishi sehemu za KICHI
Kutokana na ukame na shida za hapa na pale ikabidi waitishe kukao juu ya stakabali la suala hili.
Ndipo walipowatuma makundi mawili yazunguke wakiangalia wapi wanaweza kwenda.
Makundi haya yalipotumwa , yakaenda km walivyoagizwa na waliporudi kila kundi lilirudi na sifa mbalimbali.
Kundi la kwanza lilikuwa limetoka milimani na kusema ya kuwa twendeni huku maana tumeona maji yakiteremka toka milimani na tutalima na kufanya mambo mbalimbali.
Kundi la pili lilitoka bondeni na hawa walikuja na sifa ya kuwa huko bondeni kuna mto wenye maji mengi na samaki wa kutosha.
Kundi kubwa lilielekea bondeni na baadhi walielekea milimani.
Hawa wa milimani waliitwa watu wa milimani au kwa lugha ni wamatumbi.
Waliolekea bondeni waliitwa "WANDENGEREKO"
Hapo ndipo mgawanyiko ulipotokea.
UTHIBITISHO WA MGAWANYIKO
Tunathibitisha kwa kutumia:-
1. Koo zao zinafanana
~Mbonde
~Mketo
~Mpili
~ Mkumba
~ Mkinga
Tunathibitisha kwa kutumia:-
1. Koo zao zinafanana
~Mbonde
~Mketo
~Mpili
~ Mkumba
~ Mkinga
2. Lugha yao ni moja
Wote wakiongea wanaelewana japo kutokana na kijiografia itawapa ugumu kuelewana.
Wote wakiongea wanaelewana japo kutokana na kijiografia itawapa ugumu kuelewana.
3. Mila na desturi zao ni moja
4. Watani wao ni wamakonde na wangindo