Simulizi; "NABII WA UONGO"
*SEHEMU YA PILI *
Dar es salaam;
Ilikua jumapili moja tulivu sana, kama kawaida ya Dar es salaam, joto ndio kama mahali pake. Maelfu ya watu wakiwa wamefurika kanisani kwangu ,kanisa kubwa ambalo nililianzisha mtaa wa Mtoni kijichi _mbagala kuu.,walikanyagana na pengine wengine walisukumana ili wapate nafasi ya kuniona, na kupokea uponyaji.
Kwa upande wangu, joto sikulihisi kabisa, kwani nilikuwa nimevalia suti nzuri sana na ghali zaidi duniani. Suti hii ilikuwa na air condition ndani yake,na pia ilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi, si nyingine bali ni suti aina ya Diamond Armor. Jina ambalo limetokana na madini ya almasi ambayo yamenakishiwa kwenye suti hiyo, na kuifanya iwe ya kupendeza sana.
"Karibuni wote katika kanisa langu la Hakika worshiping center …",nilizungumza kwa sauti yenye kujiamini, huku kila mtu aliyekuwepo mahali pale akipiga makofi mengi sana, makofi yaliyonivimbisha kichwa na kujiona kama mungu mtu kwa wakati ule.
Kama kawaida yangu siku zote, niliangaza kila kona ndani ya kanisa langu kubwa.Ilikuwa ni kawaida yangu kutazama wanawake wazuri waliofika kanisani kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za maombezi, lakini huduma hiyo niliyoitoa mimi ilikuwa tofauti kabisa na jinsi walivyokuwa wakinifikilia.
"Na leo watanitambua!, kwa jinsi nilivyopendeza, ndoano lazima inase zaidi ya samaki kumi kwa mpigo hahaahaa ",niliongea moyoni huku nikishika suti yangu na kujishangaa, kusema ukweli suti yangu niliyoinunua kwa dola za kimarekani 3.2M ilinipendeza sanaa na kuonesha utofauti mkubwa uliopo kati yangu mimi na walalahoi waliopata pesa kwa jasho lao, na kuja kunitolea mimi kwani nilionekana kama mtatuzi wa matatizo yao.
"Swatzirlend wanajua!!, hatimae leo wamenitengenezea suti ya kujidai na kunipa masifaaa",nilizidi kuongea maneno ya kejeli moyoni, huku nikilifumba jicho langu la kushoto.Ama kweli duniani kuna mambo!, nilimkonyeza dada mmoja aliyekuwa mrembo sana. Weupe wake, umbo lake zuri pamoja na nywele zake nzuri alizosuka kwa mtindo wa kipekee, ni baadhi ya mambo yaliyonifanya niipeleke puta ibada ya siku hiyo, ili tu niweze kupata nafasi ya kuongea nae.
Kutokana na pesa nyingi nilizokuwa nazo, nilikuwa na uwezo wa kutembea na mwanamke yoyote niliyemtaka ndani ya kanisa langu. Na pengine mume wake akingudua, nilimtupia mamilioni ya pesa mezani na kumziba mdomo, kusema ukweli siri ikabaki kuwa siri, na uaminifu wangu ukazidi kuongezeka.
Na pia mwanamke yoyote aliyejifanya kushika dini, na kutotaka kumsaliti mume wake, alijikuta analainika pale tu alipokanyaga ndani ya nyumba yangu, nyumba ambayo niliitengeneza pembeni tu ya kanisa langu. Asikwambie mtu! nyumba yangu ilikua ni nzuri sana, japo ilikuwa ni ya ghorofa moja tu lakini madini mbalimbali yaliyotumika kuipamba, yaliifanya ing'are na kupendeza.
Lakini pia, wale wanawake waliopenda wanaume wenye magari tena mazuri ,ndio wengi ambao niliowakamata, na wakakamatika kwelikweli. Kwani parking yangu ilijaa magari ya kifahari zaidi ya matano, likiwemo gari zuri aina ya bugatti ambalo mchezaji maarufu wa mpira duniani Christian Ronaldo kalinunua majuzi tu.
"Ndugu mzee wangu wa kanisa, naomba kaniitie yule dada, nina mazungumzo nae katika ofisi ya mchungaji ",yalikuwa ni maneno yangu niliyoyazungumza baada ya ibada kuisha, niliamua kumtuma mzee ambaye alinisaidia katika kazi mbalimbali kanisani kwa moyo wote bila kutambua undani kuhusu maisha yangu na kazi ya unabii.
"Sawa mtumishi wa Mungu, tangulia ofisini atakukuta huko " ,mzee yule alinijibu kwa heshima zote, huku mimi nikimpatia noti kadhaa za shilingi elfu kumi kumi na kisha kuelekea katika ofisi yangu kumsubili dada yule, dada ambaye nilimfanyia kitendo kibaya ambacho mpaka leo ninakikumbuka na kujutia.
********
Jua kali lilizidi kuwaka na kuwakera watu wengi sana,na msichana mrembo Juliet ni mmoja kati ya watu ambao walionekana kukerwa na jua hilo na kuzidi kuongeza joto.
"Mchungaji ofisi yako ni nzuri sana, nimeingia humu ndani lakini mwili wangu umepoa ghafla ",msichana mrembo Juliet, msichana aliyenifanya nimkumbuke milele kwani ndiye msichana pekee aliyeyabadilisha maisha yangu, aliongea huku akitabasamu mala baada ya kuingia katika ofisi yangu.
"Karibu uketi, na ujiskie uko huru, usiniite mchungaji, niite tu Hakika inatosha, sio lazima uweke na cheo changu, mimi ni kijana mwenzako bwanaaa ",niliongea huku nikimtazama msichana yule machoni, na kumfanya ashindwe kujiamini.
"Kwa nini sasa hutaki kuitwa hivyo, wewe si mchunga………!!",
Alitaka kumalizia, lakini mimi nilimkatisha kauli yake kwani niliona kama inanipunguzia maksi za kummiliki msichana yule, aliyesababisha mpaka nikatishe ibada mapema sana kwa ajili yake.
"Anyway! tuyaache hayo, umeolewa? nilimuuliza swali kwa kumtega kwani kwa wakati huu nilimkazia macho, na kumfanya ashindwe kabisa kujiamini, na kubaki akinishangaa tu, hakuamini kama maswali yale yalikuwa yakitoka kwa mchungaji, tena mtu aliyeniamini sana.
"Hapana sijaolewa, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka huu wa 2017,lakini mungu akipenda labda nitafanikiwa kuolewa mwakani ",msichana yule alizungumza huku kidole chake cha kushoto akiwa amekiweka mdomoni, na macho yake yakirembua kwani aliweza kuhisi kile kilichokuwa moyoni mwangu.
"OK…!,nakukaribisha nyumbani kwangu, muda wowote tupate chakula pamoja, na kutafakali maneno ya Mungu, "nilizungumza huku tayali Juliet akiwa ameshika kitasa cha mlango, na kujiweka tayali kwa ajili ya kuwahi nyumbani, kuwapikia chakula cha mchana wazazi wake.
********
Nikiwa nimeketi nyumbani kwangu, jioni ya siku hiyo. Pombe kali za kila aina zikiwa juu ya meza yangu, bila kupoteza muda nilinyenyuka na kuelekea kwenye friji na kuchukua chupa kubwa ya lita moja, chupa ya maji ya Kilimanjaro.
Mziki mnene uliendelea kupiga, tena haukua mwingine, ulikua ni wimbo wa,sorry! wimbo ulioimbwa na mwanamziki wa kiume kutoka Marekani ,Justin Bieber.
Taratibu nilitikisa kichwa changu kufuatisha mapigo ya mziki huo, huku nikishangaa jinsi wadada wazuri wa kizungu walivyokuwa wakiucheza na kutikisa makalio yao na kuzidi kunipagawisha.
Siku zote raha jipe mwenyewe! taratibu msemo huo ulipita katika fikra zangu, na kunifanya nizidi kuwa na uchu wa kuifurahia siku ile ya jumapili,kwa kufanya anasa tofauti na jinsi ilivyokuwa ikitakiwa.
Nilifungua kizibo cha konyagi na kisha kumimina katika grasi, lakini nilipotaka kuchukua chupa ya maji niweze kuchanganya, ghafla nilisikia kengele ikilia, kengele ile iliashiria kulikuwa na ujio wa mgeni nyumbani kwangu.
"Mungu wangu !,leo nimeumbuka ",nilizungumza maneno huku nikiwa nina hofu sana, na bila kupoteza muda nilizima tv yangu kubwa ya ukutani, na kutoa frash ya miziki na kuchomeka frash ya nyimbo za kwaya na kisha kuwasha tv kwa mala nyingine tena.
Baada ya hapo, nilitoa chupa zote za pombe zilizokuwa mezani na kisha kuweka chupa kadhaa za soda, halafu nikaenda kufungua mlango wa nyumba yangu.
"Jumba lote hili, huogopi kukaa peke yako, yaani mnaishi wawili na mlinzi wa getini kama vile wafungwa, "Juliet aliongea huku akiwa ameshika biblia, lakini mimi nilitabasamu kuficha hofu yangu kwani nilisahau kutoa grasi yenye konyagi mezani.
"Nimeaga nyumbani naenda kwenye maombi, tutafakali maneno ya mungu, halafu nirudi nyumbani haraka mchungaji siunajua ni usiku ,lakini ninakiu sana ………haya maji si ninaweza kunywa?, naona wewe umejaza soda tu mezani ",Juliet aliongea baada ya kuketi kwenye sofa, huku akitazama wimbo wa nibebe!, ulioimbwa na mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Rose Muhando.
"Hapana usinywe! ngoja nikakuchukulie maji masafi ya baridi siunaona joto ",nilimnyanganya grasi yenye konyagi haraka sana na kisha kuelekea sehemu ambayo friji ilikuwepo, pale pale sebuleni.
Nilitembea haraka sana!,kwani huo ndio ulikuwa wakati pekee wa kufanya ukatili wangu. Nilichukua unga kama watu wengi wa kizazi hiki cha Makonda wanavyouita, na kunyanganya na maji kwenye grasi bila Juliet kuniona na kisha nikampelekea.
"Tusome za …bu… rii zabu…rii "zaburi haikusomeka tena!, kwani kabla Juliet hajamalzia kusoma biblia kitabu cha Zaburi, ili tuweze kutafakali. Nguvu zilimuishia na kisha kujilaza katika kochi lile, huku kitabu kitakatifu cha Mungu kikidondoka chini.
"Tayali dawa imefanya kazi, utajuta kunywa maji yangu leo ",nilizungumza huku nikimnyanyua Juliet, msichana mweupe, mrefu na mrembo sana na kisha kumpeleka chumbani kwangu.
"Hakika, Hakika Hakikaaa!, usiku huu wa saa sita utakua usiku wa mwisho kwa utajiri wako, maisha yako na umaarufu wako, tangu uingie kwenye chama chetu hujatoa sadaka kwa nyoka wetu, tumekutalifu mala nyingi lakini hutaki kutii amli yetu ",ilikua ni sauti nzito iliyosikika chumbani kwangu, na kusababisha nyumba yote kutetemeka. Mala tu baada ya kumfikisha Juliet katika chumba changu, na kisha kuvua nguo zangu, lakini kabla sijamfanya chochote ndipo nikasikia sauti ya kutisha bila kujua ilitokea wapi.
"Sawa mkuu, leo nitatii amli yenu, ",nilizungumza kwa ujasili huku nikivaa nguo zangu, na kujiweka tayali kwa ajili ya kumtoa sadaka Juliet. Kwani ili sadaka isiwe haramu, haikutakiwa nimuingilie kimwili, kwani sadaka hiyo ingekuwa najisi kwa mizimu.
Nilielekea katika kabati la vyombo, nilipojalibu kuangalia saa yangu, ilikuwa bado mapema, tena saa mbili usiku. Lakini nilikuwa na mambo mengi ya kufanya, ili sadaka iweze kukamilika, ningefanya mzaha, saa sita ingefika huku sijakamilisha hatua zote za kutoa sadaka.
"Nisamehe sana Juliet, sina jinsi ",niliongea huku nikiwa nimejifunga kitambaa chekundu kichwani, na kumchinja Juliet kama vile kuku huku damu yake ikitapakaa kila sehemu ndani ya chumba cha siri, chumba ambacho kilitofautiana na vyumba vingine, kwani kilipambwa kwa mashuka ya rangi nyeusi, nyekundu na cheupe kiasi kwamba ukuta ulikuwa hauonekani.
*ITAENDELEA *