SIMULIZI:HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE
HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE
HAIKUWA rahisi kwa mume wangu kuamini kuwa mama yake ni mchawi tena ana uchawi wa kutisha. Ni mwanamke ambaye alikuwa akiwanga usiku kila chumba katika nyumba yetu iliyokuwa Metropol jijini Arusha.Nilikuwa naogopa kumuambia mume wangu kuhusu uchawi wa mama mkwe na tabia yake ya kutusotea usiku tukiwa tumelala.
Siku moja alikuja chumbani kwangu na kunishusha chini akidhani kuwa amenipumbaza kwa dawa zake alizomwaga lakini nilikuwa na akili timamu. Nilichukia sana baada ya kuona anataka kumfanyia kitu mbaya mume wangu ambaye ni mwanaye wa kumzaa.
Baada ya kunishusha juu ya kitanda na kunilaza kwenye zulia chumbani kwetu, mama mkwe alianza kumtambuka mume wangu akiwa kitandani, kisha kumvua bukta yake. Nilijisemea, �Nijifanye nimezinduka?�
Kutokana na kumuangalia mama mkwe wangu alivyokuwa akimfanyia mume wangu, moyo wangu ulikuwa ukidunda kama vile nimetoka kufanya pushap hamsini dakika chache.
Japoku kulikuwa na giza lakini mwanga wa �taa za ulinzi�, zilizokuwa zikiwaka nje, ziliniwezesha nione kila kitu alichokifanya mama mkwe dhidi ya mume wangu.
Je, mama huyo ni nani na anafanya nini? Msimualiaji pia ni nani na ametoka wapi? Pata majibu hayo itaendelea.

HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-2
Ni ajabu sana kuona mama mtu mzima akihangaika na mwanaye aliyemzaa na akawa anatembea naye huku nikimuona.
Uvumilivu uliniishia nikajifanya nanyoosha miguu huku nikikohoa. Haraka sana kama vile paka anavyomkamata panya, bi mkubwa yule aliruka kitandani na kusimama huku akiniangalia, nikajifanya sijazinduka usingizini.
Alitoka mbio na kwenda chumbani kwake huku akiniacha nikiwa bado chini kwenye zulia na mume wangu alikuwa yupo kitandani lakini alikuwa hajui lolote linaloendelea maana alikuwa hajitambui.
Sikujua nini alimfanyia mpaka akawa kama aliyezimia. Niliinuka pale chini na kuketi kitandani.
Ghafla mama mkwe akaingia tena chumbani humo huku akiwa na tunguri ndogo ambayo ilikuwa na shanga kibao kuzunguka mdomo wake na ilikuwa imepakwa mafuta.
Baada ya kuniona nikiwa nimekaa kitandani alipigwa na butwaa akashindwa kurudi nyuma kwa sababu aliingia akiwa na spidi kali.
�Mama kwa nini umeingia chumbani kwetu? Kuna nini?� Nilimuuliza.
Mama alipata kigugumizi cha miguu maana alishindwa kurudi alipotoka au kuingia ndani kabisa akawa kama bonge la chumvi lililoganda.
Akawa ananiangalia bila kusema chochote. Niliinuka na kuwasha taa, baada ya kuwasha taa ndipo alipoanza kutetemeka kama vile anaugua malaria kali.
�Mama umefuata nini humu chumbani kwetu?�
�Nime�.nime�..�
�Mbona mikononi una tunguri ni ya nini? Mama kumbe wewe ni mchawi? Unaturoga?�
�Sikiliza wewe mama Nachope� sitaki kusikia unasema jambo hili kwa mtu yeyote, umenielewa?� alifoka mama mkwe.
�Lakini mama kwa nini unatufanyia hivi, ina maana umeshindwa kwenda kwenye nyumba nyingine ukafanya upuuzi huu. Huyu ni mwanao, kwa nini umemvua bukta?� nilisema huku nikitetemeka kutokana na hasira.
�Narudia tena, sitaki kabisa kusikia hili jambo kwa mtu yeyote, ikivuja tu nakuumiza, nakuambia kweli,� alisema mama mkwe huku akionekana kujawa na hasira.
Wakati anasema hayo nilijitahidi kumuamsha mume wangu lakini alikuwa hajui kinachoendelea. Nilijitahidi kumtikisa lakini akawa haamki wala kusema lolote alibaki kukoroma.
Niliamua kumvalisha bukta yake huku mama yake akiangalia. Nilipandwa na hasira nikatamani nimrukie mama mkwe wangu lakini niliona uhai wa mume wangu ni muhimu zaidi, hivyo nikawa najitahidi kumtingisha huku nikimuita jina.
�Usijifanye kuwa na hasira nakuambia kitu kimoja. Sema hapa kwamba hutasema siri hii kwa watu la sivyo nitamuacha mumeo akiwa katika hali hiyo, tuone utaringia nini.�
Maneno hayo yalinifanya niamini kwamba mchawi huwa hana huruma. Kama mwanaye wa kumzaa anathubutu kusema atamuacha akiwa amezimia namna hii, je ningekuwa mimi si angeniacha nife kabisa?
�Mama tafadhali, mrudishie akili yake mume wangu.� Nilimsihi lakini yeye akawa hajali na badala yake alikuwa akisema kwa kunong�ona maneno ambayo sikuwa nafahamu maana yake kwa sababu hayakuwa ya Kiswahili.
Wakati akifanya hivyo ghafla giza lilitanda chumbani. Sikujua nani alizima taa, awali nilidhani Tanesco wamezima taa lakini niliamini ni mazingaombwe ya yule mama mkwe kwa sababu mwanga wa taa za nyumba ya jirani ulikuwa ukiingia katika nyumba yetu.
Kufumba na kufumbua nikaona mbele yangu limesimama kundi la watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi yaani kaniki. Kila mmoja akiwa amepaka rangi nyeusi usoni na katika mikono yao walikuwa wameshika usinga.
Niliishiwa nguvu na kujikuta nikiwa nimeketi kitandani kando yangu akiwa mume wangu ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea.
Je, watu hao ni nani na huyo mumewe atapata fahamu au atakufa? Kujua hayo ungana nami Jumanne ijayo.

HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-3
Kufumba na kufumbua nikaona mbele yangu limesimama kundi la watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi yaani kaniki. Kila mmoja akiwa amepaka rangi nyeusi usoni na katika mikono yao walikuwa wameshika usinga.
Niliishiwa nguvu na kujikuta nikiwa nimeketi kitandani kando yangu akiwa mume wangu ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea.
PATA MAMBO...
Mama mkwe baada ya kuwaona watu wale ambao sikujua waliingilia wapi kwa kuwa milango na madirisha ilikuwa imefungwa, walianza kuimba polepole huku wakicheza.
Nilimwagiwa na mama mkwe unga fulani ulionifanya niishiwe nguvu na kujikuta nikimdondokea mume wangu ambaye alikuwa amelala fofofo.
Japokuwa nguvu ziliisha lakini ubongo wangu ulikuwa ukijua kila kilichokuwa kinaendelea pale. Nilifumba mambo kwa hofu kwamba nikiwaangalia wanaweza kuniangamiza kabisa au kunipa dawa zaidi ambazo zitaniumiza.
Nilitamani mume wangu naye apate fahamu ili ajionee mauzauza haya anayofanya mama yake na washirika wake kwa mambo ya ulozi.
Mzee mmoja ambaye sikuwa namjua jina nilimsikia akimuuliza mama mkwe.
"Tuambie, umetuitia nini?" Mama mkwe nilihisi alihama pale alipokuwa amesimama na sasa alikuwa karibu kabisa na pale tulipolala mimi na mume wangu kwa sababu nilihisi alikuwa akinipaka kitu mkononi. Akajibu.
"Huyu ni mkwe wangu. Amenigundua leo kuwa mimi ni mchawi, nikaona ni vema niwaiteni wenzangu mnishauri nifanye nini?"
Baada ya kusikia kilichowafanya wale wachawi waje pale, moyo wangu ulienda mbio nikajua kuwa siku ya mwisho wa maisha yangu imefika.
"Unataka tukuchagulie sisi cha kumfanya mkweo?" Mchawi mwingine aliuliza, nadhani alikuwa wa kike kutokana na sauti yake kuwa nyororo utadhani ni mwimbaji wa taarab.
"Hapana kwani kuomba ushauri kuna ubaya? Mimi nilijua kuwa mtapita hapa kunipitia nikaona ni vema niwaombe muingie humu ndani mnishauri."
"Sasa mbona unampaka dawa, ni ya nini?" Alidakia mwingine.
"Ahaa hii dawa ni ya kumfanya asizinduke sasa hivi mpaka tumalize mazungumzo yetu. Asijue mnashauri nini."
"Kwani mkweo anaitwa nani?"
"Jina lake ni Naomi Pirikisha, ni mkazi wa Ndanda ndiyo kwao," mama mkwe aliwajibu nikaona kama hivyo ndivyo basi wanataka kunimaliza.
"Je unataka huyu Naomi Pirikisha tumfanye zezeta?"
"Hapana. Kwa jinsi mwanangu anavyompenda, atapata shida sana kwani hatamuacha, atakuwa akimhudumia, sasa kwa kuwa huyu atakuwa hana akili, hatateseka, mwanangu ndiye atapata mateso."
"Sasa ni juu yako kuamua utamfanya nini mkweo kwa sababu kila tunachokuambia unajiwa na huruma, sasa uamuzi ni wako."
"Sawa niachieni nitajua la kifanya," alisema mama mkwe.
***
Nilishitukia asubuhi naitwa jina na mume wangu.
"Baby Naomi, mbona leo umechelewa kuamka?" amka basi," alisema mume wangu huku akinitikisa mguu.
Moyo wangu ulienda mbio baada ya kutikiswa mguu nilidhani bado ni usiku na nilikuwa natikiswa na wale wachawi walioalikwa na mama mkwe.
Nilipofumbua macho nilimuona mume wangu akiwa amesimama nyuma ya miguu yangu huku akiwa amefunga taulo kiunoni na mdomoni alikuwa na mswaki.
Nahisi ndiyo maana sikuweza kumtambua sauti wakati ananiita nikiwa usingizini kwa sababu mswaki ulimfanya asitoe sauti niliyoizoea.
Nilifikicha macho ili nimuone vizuri na kwa kuwa ndani ya chumba chetu cha kulala kuna saa niliiangalia na kuona kuwa ilikuwa saa 12.30 asubuhi na kweli muda huo mimi huwa nimeshaoga na kuanza kazi ndogondogo hapa nyumbani kwangu.
Niliamka na kuketi kitandani lakini ghafla nikakumbuka sakata la wachawi wa usiku na nikaanza kutokwa na machozi.
"Kwa nini unalia mke wangu?"
"Ni ….ni…" nilishindwa kujieleza kwa sababu nilifikiri sana na kujiambia kimoyomoyo kuwa nikisema mama mkwe alikuja chumbani usiku akafanya yale yasiyofaa kwa mume wangu na mimi pia sijui kama mwenzangu atanielewa.
Nilitafakari sana juu ya hilo, hivyo nikashindwa pa kuanzia badala yake machozi yakawa yanatiririka bila kujua niseme nini kwa mume wangu.
Itaendelea.......
,