Simulizi; NABII WA UONGO

Simulizi; NABII WA UONGO
*SEHEMU YA 08**

Vyombo vya habari nchini Tanzania vilikuwa bize kutangaza kuhusu ajari ya meli iliyotokea mida ya saa nne ,siku ya jumapili.Kama ujuavyo Waswahili,huyu alisema vile na yule akasema hivi.Lakini mashuhuda wa ajari hii,walisema chanzo cha ajari hii ni wingi wa abiria na mizigo.Wingi huu ulisababisha uzito wa meli kuongezeka,na kupelekea meli ya Mv Unguja kuzama.Abiria wote zaidi ya mia mbili,walizama maji na hakuna mtu yeyote aliyeweza kupatikana akiwa hai au amekufa.Tanzania ilishangaa,Afrika na dunia nzima kwa ujumla.Hakuna ajari ambayo iliwahi kutokea huku wahanga wakishindwa kupatikana,jambo hili liliwafanya watu wengi kulihusisha tukio hili na ushirikina.

Kusema ukweli walikuwa sahihi!,mzee Jabir na mganga ndio chanzo cha ajari hii.Hawakuwa na njia nyingine ya kumshinda adui yao Juliet,msichana mrembo niliyemuua na kugeuka mzimu.Nguvu za nyoka wao,nyoka ambaye alitakiwa kupambana na Juliet,zilitegemea sana idadi ya watu ambao nyoka yule aliwameza.

"Hatimaye tumeshinda! Mkuu wetu Nyoka,nenda kamzuie Juliet asitoboe siri zetu",ilikua ni ombi kutoka kwa mzee Jabir na mganga,ombi ambalo lilitolewa baada ya mkuu wao Nyoka kumeza watu wengi sana,watu ambao walikuwemo ndani ya meli ya Mv Unguja,na kupotea katika mazingira ya kutatanisha bila kuonekana tena,mala baada ya meli kuzama.

"Sawa vijakazi wangu,nitamzuia binti  huyu asiweze kuwadhuru ",Nyoka yule wa ajabu, aliongea huku akipotea na kisha kutoweka kwenda kupambana na mzimu wa Juliet, mzimu ambao ulikuwa tayali umewasili kanisani kwangu.

……………………………

Kanisa langu lilikua kimya sana, hakuna aliyeamini maneno ambayo Juliet aliweza kuyaongea. Aliposema kuwa yeye ni mzimu, na mimi ndiye niliyemuua, hakuna aliyeweza kuamini maneno yake. Waumini wangu walibaki wakimtazama tu, bila kufanya jambo lolote lile. Lakini kwa upande wa wazazi wangu, walielekea kuamini kile ambacho mzimu wa Juliet uliweza kuongea kuhusu ubaya na maovu yangu yote ambayo nilikuwa nikiyatenda.

"Mwanangu mbona hakuelewi, ulikua wapi siku zote hizo ",mama yake Juliet, aliongea huku  akinyenyuka sehemu ambayo walikuwa wameketi wanawake, lakini cha kushangaza alipojaribu kumkumbatia mwanae. Hapo ndipo alipoamini maneno ambayo Juliet aliweza kuyaongea, kwani mikono yake ilipitiliza na kujikuta akikumbatia hewa tu. Hatimaye pilikapilika zikaanza, kila mtu aliyekuwepo kanisani pale alitaka kuiokoa nafsi yake baada ya kushuhudia jambo lile la ajabu.

"Mama mimi sina mwili tena, mimi ni mzimu, mchungaji kaniua na kunitoa sadaka ,huwezi kunikumbatia mama, mimi sio binadamu! ",Juliet alimaliza kuongea sentesi ndefu, na kusababisha watu wengi waweze kumuogopa.

"Mchungaji alitaka kuua mpaka wazazi wake, lakini kwa sababu mimi sio binadamu, niliweza kutambua mipango yake yote na kuwaokoa wazazi wake wasifike nyumbani kwake ",Juliet alizidi kuongea kila kitu ambacho alikifahamu kuhusu mimi, hatimaye siri haikuwa siri tena, nilibaki nimesimama tu huku wananchi wenye hasira kali wakitaka kunishambulia kwa kipigo.

"Mwanangu mbona umekua mnyama kiasi hiki, kwanini usitafute pesa kihalali na wala sio kwa njia hizi haramu za kumtumikia shetani ",mama alifoka!, maneno yake makali yaliugusa moyo wangu, lakini yalipita sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto.

Waandishi wa habari walikua makini kupiga picha, na kuchukua kila tukio ambalo lilikuwa likiendelea kanisani kwangu. Waliamini walifanikiwa kwa asilimia mia moja, kwani walipata taarifa nyingi na ushahidi wa kutosha kuweza kunichafua.

Ghafla nyoka wangu niliyekuwa nimemfungia katika chumba cha siri aliweza kuvunja mlango na kuingia kanisani. Alikuwa na njaa sana, na jambo la kwanza kulifanya, ni kuanza kummeza mwandishi wa habari mmoja aliyekuwa mlangoni akipiga picha za matukio yaliyokuwa yakiendelea. Kivumbi kikatimka upya!, kiwete aliyefata huduma ya maombezi, alitimka mbio ,mwenye mapepo alipata nafuu na kukimbia kuyaokoa maisha yake.

"Nifuateni mimi, kama unataka kuishi, kama hutaki kimbia sehemu ambayo unaijua wewe! ",Juliet aliongea huku wazazi wangu na wa kwake wakimfuata kila alipokuwa akienda, na kuwaongoza kutoka nje. Kila mtu aliyejaribu kupita njia tofauti na maelekezo yake aliishia kumezwa na nyoka yule niliyekuwa nikiishi naye.

Hatimaye radi zilipiga!, tetemeko la ardhi likapita kwa dakika kadhaa, ulikua ni ujio wa mkuu wa chama cha kishetani, chama cha wapinga kristo. Nyoka huyu mwenye vichwa vingi alifika kunipatia msaada, japo alikuwa amechelewa sana.

Camera mbalimbali zilikanyagwa na nyoka yule kufuta ushahidi ili nisiweze kuchafuliwa, lakini pia waumini wote walifutwa kumbukumbu kichwani na kusahau kila kitu ambacho waliweza kushuhudia. Isipokuwa watu wachache ambao waliwahi kutoka kanisani mapema, wakiwemo wazazi wake Juliet, pamoja na wazazi wangu.
"Kidogo nimejalibu kukusaidia, kazi iliyobakia ni kuua kila mtu ambaye alishuhudia, na kuamini maneno ya Juliet kisha kutoka kanisani mwanzoni kabisa! ",Joka lile kubwa liliongea, huku kanisani kukiwa kumebaki kweupe, huku viti vikiwa vimevunjika vipande vipande mithili ya mchanga, kwani vurugu za watu kuyaokoa maisha yao hazikuwa za kawaida.

"Sawa mkuu! ",niliongea bila wasiwasi huku joka lile likipotea kama upepo, huku likizindikizwa na radi nyingi pamoja na ngurumo za kutisha!, mimi niliongozana na nyoka wangu kuelekea ndani, nyoka ambaye tayali alipata chakula, japo hakuwa na nguvu nyingi kunilinda, kwani hakuweza kuwala wazazi wangu, watu pekee ambao nilitakiwa niwatoe kwake kama sadaka ili kumuongezea nguvu.


**ITAENDELEA **
Powered by Blogger.