Simulizi; THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi)
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU YA 13**
Kifo cha Jacline kinakuwa gumzo sana nchini Tanzania, huku taratibu za kumuaga kijeshi zikifanyika katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, kwa ajili ya kuisafirisha maiti nchini kwao Afrika ya Kusini. Jonson kwa huzuni alimuaga mwenzake, huku akiapa kulipiza kisasi kwa kuhakikisha Paul anawajibishwa kwani yeye ndiye alikuwa chanzo cha matatizo yote yaliyotokea huku akimtazama mtoto mchanga wa Jacline aliyekabidhiwa na serikali kuishi naye na kumlea.
Paul akiwa na huzuni na kukosa cha kufanya baada ya kufika katika kisiwa kidogo, mahali alipoificha helikopta na ghafla kupokea ujumbe kuhusu kifo cha Jacline kupitia redio ya kijeshi iliyokuwa ndani ya ndege ile baada ya kuiwasha. "Ni nani atakuwa amepewa jukumu la kumlea mwanangu?," Paul aliongea huku akiwa na mawazo mengi juu ya kifo cha Jacline, huku akifikilia mahali mwanaye atakuwepo, ili akamchukue kwa siri na kisha kumlea mwenyewe.
Ghafla Paul anajikuta akitekwa na kundi kubwa la magaidi, bila shaka alifikilia ni maharamia kutoka Somaria kutokana na mavazi yao pamoja na siraha walizokuwa nazo, lakini alishangazwa baada ya kukutanisha macho uso kwa uso, na kiongozi wa kundi lile la kigaidi. "Paul kijana wangu, sura yako umeibadilisha lakini huwezi nidanganya mtu kama mimi ninayekufahamu vizuri, ukishavaa miwani yako tu tayali nakufahamu kwani ni miwani pekee duniani " ,Waziri Sarehe aliyesemekana amekufa kwa sumu, sumu iliyowekwa na Benedict kwenye chakula chake alipowapatia rushwa askari magereza aliongea huku akimtazama Paul kwa furaha sana. "Ndiyo nafahamu, miwani hii tulimnyanganya mtoto wa malikia wa Uingereza baada ya kumvamia na kuwapiga walinzi wake na kutokomea nayo alipokuja Tanzania kuupanda mlima Kilimanjaro, Lakini imekuaje mpaka ukawa hai wakati niliskia ulikufa kwa sumu ",Paul aliongea huku akimtazama aliyekuwa waziri wa ulinzi Sarehe Athuman, aliyeonekana kumiliki kundi kubwa la kigaidi kwa ajili ya kujalibu kuipindua nchi ya Tanzania kwa mara nyingine tena. "Siwezi kuuawa kirahisi na mtoto mdogo kama yule, nilimpatia pesa daktari na kutoa ripoti ya uongo na kutengeneza maiti yangu feki iliyobadilishiwa sura na kufanana na mimi " ,Sarehe aliongea huku akifurahi kukutana na Paul kwa mara nyingine tena, kwani alimuamini sana katika shuguli zake.
"Nakuomba tuungane kwa mara nyingine tena, tutimize malengo yetu "mzee Sarehe aliongea huku akiamrisha jeshi lake kushusha siraha zao, kwani walikuwa bado wamemteka Paul na kumnyoshea siraha zao kichwani kwake ili atakapo leta fujo wasambaratishe kichwa chake. Lakini kwa wakati wote ambao Sarehe aliyazungumza hayo, Paul alikua amesimama akiwa amepigwa na butwaa akimtazama waziri yule kwani hakuamini alichokuwa anakiona mbele ya macho yake kuwa mzee Sarehe alikuwa bado hai.
"Inabidi nimkubalie, lakini nitamuua muda wowote haraka sana na mimi niwe kiongozi wa kundi hili …mzee huyu ni msaliti hawezi kutunza siri, mambo yakiwa mabaya anataja taja tu ilimradi awe huru " Paul alizungumza maneno yake ambayo aliyatambua yeye mwenyewe, huku akitikisa kichwa kuonesha ishara ya kukubaliana na ombi la waziri muasi bwana Sarehe Athuman.
Muda siyo mrefu, kundi dogo la kigaidi linalongozwa na Mzee Sarehe, waliongozana na Paul mpaka kwenye kambi yao iliyokuwa ndani ya mahandaki makubwa katika kisiwa ambacho Paul alienda kujificha. "Hapa ndipo mafichoni kwetu, ulipofika mara ya kwanza na helikopta tulikusikia kutokana na mtikisiko, ikabidi tutoke ndani ya mahandaki yetu kwani tulifikili tumevamiwa na askari wa Tanzania, bila kutegemea tulikuta ndege imefichwa kwa majani huku muhusika katoweka, ikabidi tuwe tunafanya dolia kila siku katika eneo lile ili tumtambue mtu aliyeweza kuficha helikopta katika himaya yetu ",mzee Sarehe aliongea maelezo marefu sana, huku akimkalibisha Paul ndani ya mapango waliyoyatumia kwa ajili ya kujificha dhidi ya maadui. "Duuu, Asante sana mkuu ,naamini kila kitu kitakwenda sawa " Paul aliongea huku akiwaza na kuwazua namna ya kumuua Sarehe ili yeye ndo awe kiongozi mkuu wa himaya ile.
Siku moja Paul akiwa anafanya mazoezi peke yake nje ya mahandaki yao, katikati ya msitu ulioko ndani ya kisiwa kidogo kilichopo katika bahari ya Hindi.Ghafla Paul alikutanisha macho uso kwa uso na joka kubwa aina ya "black mamba "(koboko), likiwa limeinua kichwa juu na kisha kusimama tayali kwa ajili ya kumlukia na kumshambulia Paul. "Hapa nijifanye sijaliona, kutokana na njaa zake ,likinilukia tu nitalikata kichwa haraka sana ",Paul aliwaza kichwani haraka sana kama umeme, na kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha nyoka yule baada ya nyoka kuluka hewani kwa ajili ya kumuangamiza ."Hapa tayali, Sarehe hana jipya mbele yangu mimi ndo muuaji mweusi kama navyofahamika ,mimi Siyo Benedict sitoshindwa kumuua",Paul aliongea huku akikamua sumu ya nyoka yule na kuiweka katika kichupa kidogo cha maji ya kunywa, huku akifurahi sana kwani aliamini mzee Sarehe hatoweza kuepuka kifo, kwani sumu ya nyoka huyo aina ya koboko ndo sumu kali sana kuliko nyoka wote ulimwenguni na huua kabla ya masaa ishirini na nne baada ya kuingia katika mfumo wa damu.
"Kuanzia leo mimi ndiyo kiongozi wenu ,"Paul alitoa amri mbele ya kundi kubwa la jeshi la mzee Sarehe, baada ya kuwatandika na kuwajeruhi vibaya huku wengine wakipoteza maisha, baada ya kutaka kumpinga na kulipiza kisasi walipongundua Paul kahusika na mauaji ya mkuu wao mzee Sarehe, kwa kutumia sumu ya nyoka iliyowekwa ndani ya maji ya kunywa na kisha kumpatia mzee Sarehe. "Ndiyo mkuu ",sauti kubwa yenye unyonge, hasira na chuki ilisikika ikitamka maneno ya kukubaliana na uongozi mpya wa bwana Paul Agustino.
**ITAENDELEA *
"Hakika ninaweza, na wewe pia unayesoma simulizi hii unaweza …kamwe usikubali kukata tamaa bali jiamini kama Paul anavyojiamini, lakini pia usikubali kushinda katika mambo mabaya, bali imani yako iwe katika kutoshindwa katika mema ",