Simulizi ;"THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi)



Simulizi ;"THE BLACK KILLER "
       (muuaji mweusi)
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 06**
Paul Agustino anaitelekeza pikipiki yake barabarani, na kutokomea ndani ya msitu wa Amazon. Msitu mkubwa nchini Marekani unaosifika kwa kuwa na wanyama wengi wakali, hakuna binadamu yeyote aliyefanikiwa kutoka salama baada ya kuingia katika msitu huo. Paul akiwa ameshikilia bastora yake pamoja na kisu kikali cha kijeshi mikononi mwake, aliendelea kuingia kabisa katikati ya msitu, bila kuogopa kitu chochote kutokana na ujasiri aliokuwa nao.


Ghafla Paul anajikuta katika wakati mgumu baada ya joka kubwa aina  ya chatu lililokuwa juu ya mti, kumdondokea na kisha kujiviringisha katika mwili wa Paul tayali kwa ajili ya kummeza. "Shenzi wewe, umeingia choo cha kike ",Paul alizungumza maneno ya kejeli kwa joka lile kubwa huku akipambana nalo ili kujikomboa. Bila kutegemea joka lile linamtupa Paul ndani ya maporomoko ya maji ya mto Amazon, mto ambao ulikuwa umejaa mamba wengi sana wenye njaa kali, na kumfanya Paul kuwa katika wakati mgumu kupambana na joka lile kubwa pamoja na mamba waliokuwa wanaonekana kuwa na njaa kali kwa muda mrefu.


"Paaah ……paaah ……paah "milio ya risasi ilisikika pamoja na mishale mingi ,iikitokea katikati ya msitu na kushambulia mamba  pamoja na joka lile kumbwa ambalo lilikuwa tayali limemshinda nguvu Paul na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili. "Pole sana baba, nitakusaidia kukutibu "mzee wa makamo alimpa pole Paul, huku vijana walio onekana kuwa ni watoto wa mzee yule wakimkokota Paul na kumtoa ndani ya maji huku akiwa amejeruhiwa vibaya sana. "Asante sana mzee wangu, ilikuwaje mpaka ukafahamu kuongea lugha ya Kiswahili, na kwanini unaishi ndani ya msitu huu ambao ni hatari sana ……"Paul alimuulza mzee yule swali, huku akionekana kushangazwa sana na mzee yule aliyemsaidia, mzee ambaye alikuwa amevalia ngozi ya mamba pamoja na vijana wake.

"Utafahamu kila kitu, tuondoke eneo hili tuelekea kwenye kambi yetu...…eneo hili ni hatari sana kwa wakati huu kwani wanyama wakali wanapenda kuja kunywa maji hapa mtoni, lakini tukifika kambini nitakuelezea kila kitu ",mzee yule alimjibu Paul huku wakiondoka sana eneo lile, lakini kwa upande wa Paul, mawazo mengi yalizidi kumtawala na woga kumtawala kwani alimuona mzee yule hakuwa mtu wa kawaida kutokana na muonekano wake na  njinsi alivyomuokoa kutoka kwa wanyama wakali.
…………………………………
Camera mbalimbali zilizoko kila kona ya barabara katika nchi ya Marekani, zinakaguliwa na askari na kisha kugundua sehemu ambayo Paul Agustino aliweza kuelekea. Jeshi kubwa la nchi ya Marekani likiongozwa na vijana watatu wa Kiafrika, wanajikuta wakiingia katika msitu wa Amazon kumtafuta Paul, baada ya kuikuta pikipiki aliyoitumia kutoroka ikiwa imetelekezwa barabarani. "Huyu mshenzi nikimkamata nitahakikisha na mkata kata vipande vipande, hawezi kuisumbua dunia kiasi hiki ",Godfrey alizungumza kwa hasira sana huku akitumia panga lake kukata matawi ya vichaka, ili kutengeneza njia ya kupita na kuingia ndani kabisa ya msitu.  "Nina hasira naye sanye sana, huu ni mwezi wa sita niko mbali na familia yangu nikiteseka kumtafuta mpuuzi huyu, lazima atalipia tu siku nikimkamata, nina hasira naye sana "Jonson aliongea pia kwa hasira maneno ambayo yaliyodhibitisha kuwa alichoshwa na kazi  nzito ya kumtafuta bwana Paul Agustino.


Kwa upande wake Jacline aliumia sana kila aliposikia maneno yaliyohusu adhabu kari atakayopatiwa Paul, mara baada ya kutiwa mikononi. "Nakupenda sana, lakini nitahakikisha nakuua kwa mikono yangu mwenyewe kutokana na mauaji ya kikatiri unayoyafanya kila kukicha ……na sitajali kuhusu kiumbe kilichoko tumboni mwangu kukosa baba ",Jacline aliongea kwa uchungu mkubwa na kwa sauti ya chini, huku machozi yakimtoka. Jacline alizidi kusonga mbele msituni na askari wenzake, bila kumwambia mtu yeyote siri aliyonayo baada ya kugundua kuwa na ujauzito wa bwana Paul Agustino, jambazi sugu lililoitikisa dunia kutokana na habari zake kusambaa duniani kote.


…………………………………


"Mimi naitwa daktari Benezeth Christopher kutoka Tanzania, ndege yetu ilipata ajari miaka hamsini iliyopita tukiwa tunaelekea visiwa vya Haiti kwa ajili ya kutibu wahanga wa vita. Ndege yetu ilikuwa na jumla ya abiria kumi, nane walifariki dunia huku wawili tukitoka salama mimi nikiwa kama daktari mkuu pamoja na nesi wangu. Kutokana na msitu huu kuwa na wanyama wakali, tulishindwa kutoka ndani ya msitu na kujikuta tukianzisha makazi katikati ya msitu huu na kuishi kama mke na mme " Daktari yule alimuelezea Paul, historia ya maisha yake huku Paul akiwa makini kuisikiliza kwani ilimvutia sana. "Vipi kuhusu historia yako kijana wangu, inaonekana wewe ni askari kutokana na jinsi nilivyokuona ukipambana na joka lile kubwa, na pia inaonekana una siri nzito moyoni mwako kwani muda mwingi nakuona ukiwa na mawazo…niambie tu siri hiyo nitakusaidia "Mzee yule aliyeonekana kuwa na busara nyingi huku uso wake ukionekana kuwa ni mtu mwenye huruma sana alimuulza Paul yaliyomsibu, na kumwomba amwambie ili aweze kumsaidia.


Paul Agustino bila kutegemea anajikuta anamwamini mzee yule, na kumwelezea kila kitu kuhusu historia na siri nzito ya maisha yake, "Nisaidie mzee, sina msaada mwingine zaidi yako ……sasa hivi nimebadilika sio mtu yule wa zamani ",Paul aliongea maneno kwa hisia kali huku machozi yakimtoka, hali iliyomfanya mzee yule akubali kumsaidia.


"Nitaibadilisha sura yako kwa mara nyingine, lakini usithubutu kunifanyia chochote kama ulivyomfanyia dokta Benny, mimi hutoniweza, mimi ni mtu hatari sana zaidi ya unavyofikiria ",mzee yule alimweleza Paul maneno ya kukubali kumsaidia, huku akimuonya asithubutu kumuua kwani asingeweza kufaulu kama  alivyofanya kwa dokta Benny.


Kwa mara nyingine upasuaji wa kubadilisha sura ya Paul unafanikiwa, kwa kutumia vifaa vya kidaktari ambavyo havikuharibika baada ya ndege kudondoka. Kutokana na ujuzi wa mzee yule kuwa ni wa zamani sana, huku akitumia vifaa vya kizamani vya kufanyia upasuaji, Paul Agustino alionekana kuwa na sura ya kizee baada ya kufanyiwa upasuaji ule. "Bila shaka, sitoweza gundulika ……nakushukuru sana mzee wangu ",Paul aliongea kwa furaha sana na kumshukuru mzee yule, huku moyoni akiwaza kumuua na kisha kutoroka eneo lile.

Powered by Blogger.