HISTORIA YA WASANGU

Daaa asante kwa historia hii ya wasangu Wa usangu

Image may contain: one or more people, people standing, outdoor and nature



JE UNAZIJUA MILA NA TAMADUNI ZA KABILA LA WASANGU ZILIZOPO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA.
KUNA hazina nyingi za mila na tamaduni za wasangu zimeachwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya baadhi ya vijiji vikiwemo vya Upagama,Idunda,ukwaheri na Msangaji kuhamishwa kupisha hifadhi ya Taifa ya Ruaha 2007-2008 na iwapo kumbukumbu hizo za asili zikihifadhiwa zinaweza kuwa kivutio kikubwa kwa wageni.
Muonekano wa Bonde la Usangu ni kama Bakuli, na ndani ya bonde hilo kuna mlima mrefu kiasi na uliochongoka kwa juu unaofahamika kwa jina la NDATAMBULWA.
Asili ya jina mlima huo linatokana na mtemi wa kabila la Wasangu aliyefahamika kwa jina la ZAKARIA MERERE (NDATAMBULWA) ambaye alikuwa mtawala msaidizi upande wa kaskazini mashariki mwa Bonde la Usangu (Unyamande) katika Vijiji vya Utuya,Ulanga,Mawale, Upagama,Chankonde na aliishi na kufia katika kijiji cha Upagama kata ya msangaji wilaya ya Mbarali-mbeya (Usangu).
Wakati akipambana na maadui zake wakiwemo wahehe na wakoloni wa Kijerumani alikuwa na kawaida ya kukimbilia katika mlima huo uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa lengo la kuwaona maadui kwa Urahisi zaidi na ukiwa juu ya Mlima huo utaweza kuliona bonde la Usangu kwa uzuri sana na kuna ambo yanayosadikiwa kuwa ya kimiujiza katika mlima Ndatambulwa .
Na kuna mlima mdogo unaofahamika kwa jina la KITUNDAKULU ndani ya hifadhi hiyo ambapo kuna shina la tumbaaku(lipo mpaka sasa) inayoaminiwa kuwa ni la kale sana na halijawahi kukauka na lilikuwa ikitumiwa na watemi wa Kisangu na baada ya hapo wananchi wakawaida hususani wawindaji na walina asali wanaovuta tumbaaku walikuwa wakitumia kabla ya eneo hilo kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha(sharti ni lazima uvute bila ya kuondoka na kipisi au jani la tumbaku).
Pia katika eneo hilo kuna kete za bao(mchezo wa bao) ambazo zipo mpaka sasa na zilikuwa zikitumiwa na watemi enzi za zamani na kwa miaka kadhaa iliyopita kabla ya eneo hilo kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha wawindaji na walina asali walikuwa wanatumia vitu hivyo wanapokuwa wamechoka na sharti kubwa hupaswi kuondoka na vitu hivyo baada ya kutumia.
Mpaka sasa wazee hao jamii ya Kisangu wapo tayari kutoa ushirikiano kwa Mamlaka husika ili kuhakikisha maeneo hayo yanahifadhiwa na kuheshimiwa na wanaweka wazi kuwa kuna mambo mengi sana ya mhimu na ya kijadi likiwemo bwawa la ajabu lenye samaki ambalo lilikuwa likitumiwa na wawindaji wakikosa wanyama ( ambapo samaki huvuliwa kwa maombi na mahitaji maalum) na katika eneo la bwawa hilo kuna kuku weupe ambao huonekana kwa nadra.
Wazee hao wanaweka wazi kuwa ndani ya hifadhi hiyo kuna mlima mdogo wenye pango na ndani ya pango hilo kuna bunduki inayoonekana,lakini sirahisi kuichukua na pia kuna nyuki ya Muda mrefu ambapo walina asali walikuwa wakitumia kulina pindi wanapozidiwa na njaa na kabla ya kulina asali maombi ya kijadi hutangulizwa na hivyo kumwezesha mlina asali kulina bila kuumwa na nyuki(na asali inayolinwa ni lazima itumike kuliwa katika eneo hilo bila ya kuondoka nayo).
Na katika eneo la Wimbe wakati unaelekea kilichokuwa Kijiji cha Msangaji ndani ya hifadhi ya Ruaha kuna jiwe ambapo ambapo juu ya jiwe hilo kuna Unyayo wa binadamu anayesadikiwa kuwa ni wa kale sana(mguu wa kushoto).
Pia kuna eneo maalum kwajili ya maombi ya kimila( matambiko) lililopo katika eneo la Ngelyama ndani ya Hifadhi hiyo ya Ruaha kando kidogo ya Mto wa Ruaha mkuu ambapo watemi wote wa kabila la wasangu waliowahi kutawala katika bonde la Usangu wamekuwa wakilitumia kwa ajili ya maombi ya kimila.
Aidha karibu na eneo hilo la Matambiko (Ngelyama) ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuna Bwawa kubwa kiasi ambalo lipo hadi sasa lilikuwa linakaliwa na viboko wengi, ambapo zamani inasadikiwa kuwa jaamii ya kabila la Wasangu walikuwa wakienda katika bwawa hilo na kumfunga Kiboko kwa kamba na kumtoa nje ya maji kwa ajili ya Kitoweo bila ya kudhuliwa na mnyama huyo.
:Baadhi ya watemi wa Kabila la Wasangu waliowahi kutawala.
1834 - 1860 Mui'Gumbi Merere I
1860 - 1893 Tovelamahamba Merere II
1893 Mugandilwa Merere III (1st time)
1893 - 1896 -
1896 - 1906 Mugandilwa Merere III (2nd time)
1906 - 1950 Mxabuwoga Merere IV
1950 - 1953 Myotishuma
1953 - 1962 Alfeo Mgandilwa Merere V (miaka 38years)
1962 - 1988 -
1988 - c.1989 Yusuf Merere VI (1st time)
1989 - c.2002 Ahmed Merere VII
2002 - 2003 Yusuf Merere VI (2nd time)
2003 - Salehe Alfeo Merere VIII
Picha chini ni ya Chifu Zakaria Merere (Ndatambulwa) picha ilipigwa miaka ya 1967 na picha inayofuata ni chifu wa sasa wa kabila la wasangu Salehe Alfeo Merere VIII(bado kijana) na picha ya tatu ni boma la Chifu Merere eneo la Utengule-Usangu.
Taifa lisilo na utamaduni ni Taifa lililokufa. (a nation without culture is a lost nation).

Powered by Blogger.