Simulizi; "THE BLACK KILLER" (muuaji mweusi)
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 10**
Tetesi za Paul kurudi nchini Tanzania zinasambaa kila mahali katika jiji la Dar es salaam, huku barabara mbalimbali za mikoani zikifungwa na kisha kila gari lililoingia na kutoka katika jiji hilo liliweza kukaguliwa kwa umakini sana. "Hii ni taarifa ya habari kutoka ITV, jambazi Paul Agustino yasemekana karudi nchini Tanzania huku akiwa na sura nyingine kabisa baada ya kuibadilisha…na muonekano wake uko kama unavyoonekana katika picha ",mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, alitangaza habari iliyogusa hisia za wengi huku akiwasihi wananchi kutoa taarifa polisi mara watakapomuona popote pale. "Mungu wangu kumbe tunafuga jambazi, siku fahamu kama yule babu aliyekuja hapa jana ndio Paul Agustino …jambazi sugu ",meneja wa hoteli ya sea cleaf aliongea huku akibonyeza simu yake ya mezani kwa ajili ya kuwapigia polisi.
"Duuh tayali mambo yalishahalibika……",Paul aliongea baada ya kushtushwa na taarifa ya habari aliyoisikia, huku akijiandaa kwa ajili ya kutoweka haraka sana eneo lile. "Huyu mpuuzi bila Shaka analengo baya na mimi, kwanini kaja Tanzania bila kunipatia taarifa ",mfanyabiashara Benedict alilalamika baada ya kusikia taarifa ya habari, kuhusu ujio wa Paul katika nchi ya Tanzania na kumfanya kuutilia hofu ujio huo.
Godfrey na wenzake wanafika nchini Tanzania na bila kupumzika wanajikuta katika jukumu zito la kwenda kumkamata Paul, baada ya kupokea simu kwa siri kutoka katika hoteli ya kitalii ya Sea cleaf. ",Chukueni kila siraha mnayoona itawasaidia, lakini pia hakikisheni barabara zote za jiji la Dar es salaam zinafungwa na kukagua kila gari linalopita kwa umakini mkubwa ", raisi wa Tanzania alitoa amri kwa majeshi yake ya ulinzi, huku akiwapa majukumu askari watatu wakiongozwa na Godfrey kuhakikisha Paul asiweze kutoroka kwa mala nyingine tena.
Muda si mrefu Paul akiwa ndani ya chumba chake akitafakali namna ya kutoroka, ghafla alisikia sauti ya helikopta za kijeshi zikiizunguka hoteli na kumfanya kufanya maamuzi magumu. ",Duuh kumbe askari wameshaizunguka hoteli, nisipokuwa mjanja hapa nitakamatwa ", Paul aliongea maneno hayo baada ya kuchungulia dirishani, na kuona askari wengi wenye siraha nzito wakiwa wameizunguka hoteli. "Tayali nimeshapata njia ya kutoroka, sijawahi shindwa hata siku moja ",Paul alipata wazo namna ya kutoroka, baada ya kutafakari kwa muda mrefu. Haraka bila kupoteza muda alichukua bastora yake, pamoja na kisu chake na kisha kuanza kupanda juu kabisa ya hoteli.
"Pyuuu ……pyuuu ……pyuu ",Paul alimpiga risasi tatu askari aliyekuwa akija bila kuwa makini, na kisha kumvua nguo zake na kuzivaa yeye ,nguo zile zilimrahishia kutoroka kwani alifanana na askari wa jeshi la polisi. Paul kwa umakini mkubwa alitembea huku akiwa anaua askari kimya kimya na kisha kuifikia helikopta iliyokuwa imepaki juu kabisa ghorofa ya mwisho ikishusha askari polisi wengine kwa ajili ya kuongeza nguvu.
"Adui yuko juu, pandeni ngazi haraka sana ……tukamkamte",Godfrey aliongea huku akiwa anapandisha ngazi kuelekea juu, akiwa ameongozana na Jonson, Jacline pamoja na askari wengine.
"Mikono juu hapo ulipo, ukijitikisa nasambalatisha ubongo wako …",Paul aliongea huku akimnyoshea siraha rubani wa ndege ya kijeshi, baada ya kuwamaliza askari wengine. ",Nakuomba ondoa ndege hii, unipeleke sehemu ninayokuelekeza ",Paul aliendelea kuongea, huku dereva wa ndege akitii amri aliyopewa na kuipaisha ndege kutoka eneo lile.
Askari wanafika juu ya ghorofa na kushuhudia helikopta ikipaa kutoka eneo lile, huku maiti za askari zaidi ya mia moja zikiwa zimezagaa eneo lile. Pyuuuh …pyuuu…paah ……paah,, askari wakiongozwa na Godfrey, waliishambulia ndege iliyombeba Paul bila mafanikio, na kushuhudia Paul akifanikiwa kutoroka kwa mala nyingine tena.
…………………………………
Jacline anashindwa kuendelea na oparesheni kabambe ya kumtafuta Paul kutokana na ujauzito wake kuzidi kukua, hali ya afya yake inakua mbaya sana kutokana na kazi ngumu aliyokuwa akiifanya bila kujali ujauzito wake alionao. "Mgonjwa inatakiwa aongezewe damu, bila hivyo atapoteza maisha baada ya masaa ishirini na nne yajayo " ,daktari wa hospitali ya taifa ya muhimbili alizungumza na Jonson pamoja na Godfrey, akiwaelezea juu ya hali mbaya ya Jacline aliyonayo ,akiwa amefikishwa hospitalini muda mfupi tu baada ya kutoka kumkamata Paul bila mafanikio.
Kutokana na hali mbaya ya Jacline , mtu wa kumtolea damu yenye kuendana na grupu lake anakosekana miongoni mwa Jonson na Godfrey ,bila kutegemea anatokea mtu asiyetegemewa kabisa anajitolea damu na kuyaokoa maisha ya Jacline. "Tafadhali dokta, unaweza kutwambia mtu aliyeyaokoa maisha ya ndugu yetu ",Jonson aliomba kuambiwa mtu aliyemuongezea damu Jacline, lakini dokta aligoma katu katu kumweleza ."Muhusika kakataa kutajwa jina lake, na wala kuiweka wazi sura yake …hivyo basi maadili ya kidaktari hayaniruhusu kufanya hivyo kama muhusika alinikataza ",Dokta alizungumza huku akishikilia msimamo wake, wa kutomtaja mtu aliyeyaokoa maisha ya Jacline.
**ITAENDELEA **