Simulizi; "THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi)


Simulizi; "THE BLACK KILLER "         (Muuaji mweusi)




Mtunzi ; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 09**

Safari inakua ngumu sana katika mto wa Amazon, Godfrey na wenzake wanajikuta katika wakati mgumu baada ya upepo mkali kuvuma na kusababisha mawimbi makubwa kuupiga na kuusambalatisha mtumbwi waliokuwa wameupanda.."Vuta pumzi… jitahidi, ukikata tamaa utasombwa na maji „" Godfrey alimtia moyo Jacline aliyekuwa anaonekana kuzidiwa na mawimbi, hali ambayo ingepelekea Jacline kuzama kama angeishiwa pumzi kabisa na kushindwa kuogelea.Japokuwa wote walikua hodari sana katika kuogelea, lakini walijikuta wakizidiwa na nguvu ya mawimbi huku kila mmoja akitafuta njia ya kuokoa maisha yake.


Paul Agustino jambazi la kimataifa, anafanikiwa kuwazidi nguvu askari wa malikia wa eneo lile la kisiwa kilicho katika nchi ya Mexico, baada ya mapambano makali kutokea na kisha askari wengi wa malikia kupoteza maisha huku Paul akitoroka na dhahabu nyingi zilizokuwa zikimilikiwa na jamii ile. "Siku sote mimi ni mshindi, Hahaha ",Paul aliongea kwa sauti huku akicheka kwa furaha na kuwafanya watu waliokuwa karibu naye kumshangaa, kwani walimuona kama kichaa kutokana na yeye kuongea peke yake.


"Give me ten billions, ",(Nipatieni bilioni kumi), Paul alitaja kiasi cha pesa alichokitaka, baada ya kwenda kuuza dhahabu alizoziiba katika sehemu ya kuuzia vito vya thamani iliyopo katika jiji la Mexiko„kutokana na dhahabu alizokuwa nazo kuwa na thamani kubwa zaidi ya pesa aliyoitaja, alilipwa pesa hiyo haraka sana na kisha aliweza kutoweka eneo lile. Bila kupoteza muda, Paul alielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mexiko, tayali kwa ajili ya kusafili kurudi Tanzania siku iliyofuata.


Malikia wa eneo la kisiwa kilichoko Ufukweni katika nchi ya Mexiko, anawakuta vijana watatu ufukweni wakiwa wamepoteza fahamu ,akiwa ameenda kuvua samaki kama kawaida yake. Kutokana na hasira aliyokuwa nayo, baada ya kuibiwa dhahabu zake huku vijana wake wengi wakijeruhiwa na wengine kupoteza maisha, hakuwa na huruma na kina Godfrey bali aliwakamata na kisha kuwafunga katika gereza lake. Huruma na uaminifu wa malikia yule kwa vijana wale watatu, unazidi kupotea baada ya kugundua walikuwa na siraha pamoja na baadhi ya nyaraka za kijeshi zilizokuwa zimelowa maji baada ya kuwakagua katika mifuko yao.


"What do you want in this land, are you spies? ",(mnataka nini katika ardhi hii, nynyi ni wapelelezi?) Malikia yule aliuliza swali kwa hasira, huku jeshi lake likiwa limewanyoshea siraha wakina Jonson, Godfrey pamoja na Jacline. ",We are soldiers from Tanzania, we are here looking for the killer, who killed thousands of people in our country ",(sisi ni askari kutoka Tanzania, tuko hapa kwa ajili ya kumtafuta muuaji aliyeua maelfu ya watu katika nchi yetu) Godfrey alijibu swali la malikia yule, jibu ambalo lilimfanya malikia yule kukumbuka mauaji aliyoyafanya Paul katika ardhi yake na kuamini kweli alikuwa ni jambazi. "There is an old man from Tanzania, has killed my people and has disappeared with my gords …",(kuna mzee kutokea Tanzania, kaua watu wangu na kutoweka na dhahabu zangu) malikia yule aliongea huku akiamini kuwa mtu aliyehusika na wizi wa dhahabu zake, ndo yule aliyekuwa akitafutwa kwa tuhuma za mauaji. ",Where do you think ,he has gone? "(Unafikilia kaenda wapi?) Jonson alimuulza malikia yule, huku askari wa malikia wakiwafungua kamba na kuwatoa katika gereza lao baada ya kujiaminisha kuwa sio watu wabaya. ",He told me, he want to go back Tanzania …",(aliniambia, anataka kurudi Tanzania)  malikia yule aliongea huku akiamuru chakula kizuri kuletwa, kwa ajili ya Godfrey na wenzake.



Jua kali liliwaka huku moshi wa viwanda mbalimbali vikilipamba anga la jiji la Dar es salaam, ndege kubwa aina ya Boeing 777,Ndege ambayo Paul alipenda kuitumia katika safari zake, iliikanyaga ardhi ya Tanzania. "Nafurahi kurudi nyumbani, ni miaka miwili tu lakini nchi imeendelea sana ",Paul aliongea huku akishangaa uwanja mzuri wa ndege wa mwalimu Nyerere ukiwa unapendeza sana baada ya kufanyiwa marekebisho. Paul bila kupoteza muda anachukua taksi na kisha kuelekea katika hoteli ya kitarii ya sea cliff, hoteli ambayo aliiona nzuri kwake bila kujali gharama kubwa za mahali pale.


godfrey na wenzake wanafanya mawasiliano na serikali ya Tanzania, baada ya kufika katika jiji la Mexiko lililopo katika nchi ya Mexiko wakitokea katika kisiwa kilichoko ufukweni mwa nchi hiyo, kisiwa kilichotawaliwa na malikia aliyekuwa na huruma sana na kujizolea sifa kedekede katika nchi ya Mexiko kutokana na kuwasaidia watu mbalimbali. ",Tayali nimeshampatia taarifa waziri wa ulinzi wa Tanzania, pamoja na raisi kuhusu kurudi kwa Paul nchini Tanzania akiwa na sura bandia ",Paul aliongea huku akifurahia na wenzake kurudi Tanzania siku iliyofuata.


Siri ya Jacline ya kuwa na ujauzito inafichuka, huku muhusika akiwa hajulikani. ",Twambie muhusika ni nani?, "sisi ni rafiki zako, na pia ni askari wenzako, Jonson aliongea huku akilishangaa tumbo la Jacline lililokuwa limeanza kuwa kubwa. ",Mimi niliziona dalili zako za ujauzito muda mrefu, lakini nilishindwa kukuuliza kutokana na majukumu kutubana ",Godfrey pia alisikika akiongea huku akipanga vitu kwenye begi, kwa ajili ya safari ya kurudi Tanzania. ",Mtafahamu kila kitu muda ukifika, huu sio muda sahihi kuzungumzia swala hilo ",Jacline alijibu maswali aliyokuwa ameulizwa,huku akionekana kukelwa sana na maswali aliyoulizwa.


*ITAENDELEA*
Powered by Blogger.