HISTORIA YA WAKINGA

Image may contain: cloud, sky, mountain, grass, outdoor and natureMapembelo!! Ijue kwa ufupi historia ya wakinga na makabila madogo madogo yanayounda kabila la wakinga
Wakinga ni watu wanaopatikana mkoani Njombe wilaya ya Makete na lugha yao ni Kikinga ambacho asili yake ni misitu ya Kongo.Wakinga wanaundwa na makabila madogo manne nayo ni Wamahanji,Wawanji,Wamagoma na Wakinga halisi
Zifuatazo ni sifa na tabia za makabila haya
1.WAMAHANJI hawa ni watu wanaopatikana Kipagalo tarafa ya Bulongwa sifa kubwa ya watu hawa ni kusoma yaani ni wasomi na ni wafanya biashara wakubwa pia hupenda sana michezo hususan soka watu hawa si watu wa kujisifu kabisa yaani hata akifanikiwa kivipi ktk jambo lolote lile utasikia najaribu tu
2.WAMAGOMA, hawa ni watu wanaopatikana tarafa ya Magoma na hasa hasa Kata ya Ipelele sifa kubwa ya watu hawa ni biashara ndogondogo hasa biashara ya mazao kama viazi na ngano pia watu hawa ni wakarimu sana kuhusiana na suala la shule wao wapo moderate tu
3.WAWANJI, Wawanji wengi wanapatikana kwa wingu tarafa ya Matamba na Chimala watu hawa huwa hawapendi kabisa kuitwa wakinga na ni wafanyabiashara wa mazao na mbao pia
4.WAKINGA halisi, Watu hawa wanapatikana maeneo yote ya MAKETE ni wafanyabiashara,wapo pia walevi watu wa kupenda sifa na ni watu wasio pendelea sana shule Ila biashara
Kwa Leo tuishie hapa
Pride of Ukinga
Powered by Blogger.