Simulizi; "NABII WA UONGO "


Simulizi; "NABII WA UONGO "
**SEHEMU YA 5**

Masaa yalikwenda, huku nikiwa naendelea kujisomea biblia. Mpaka nikajikuta napitiwa na usingizi pale pale sebuleni ,na kusema ukweli nilikalili mistari mingi sana, mistari ambayo ingenisaidia kanisani siku iliyofuata.

"What …!,hawajafika!,"nilishangaaa sana baada ya kushtuka usiku wa manane ,wazazi wangu wakiwa bado hawajafika. Nilipojalibu kuangalia saa yangu ya ukutani ,ilikuwa tayali imetimu saa tisa usiku.

"Hapa tayali mambo yamehalibika, jumamosi imekua ya majanga sana kwangu!au wamehisi jambo ambalo nilikuwa nataka kuwafanyia! ",niliongea huku nikiwa na wasiwasi sana, kwani kabla jua halijachomoza ilitakiwa nitoe sadaka, na sadaka iliyokuwa inatakiwa kutolewa ilikuwa ni ya watu ambao niliwapenda sana.

Sebuleni hapakukalika tena, nilizunguka kama kichaa, kwani sikujua nilikua naelekea wapi.Jambo pekee ambalo lilikuwa likinisumbua kichwani, ni kuhusu nyoka ambaye nilipewa kama zawadi kwa ajili ya kuishi naye Nyoka huyu ilikuwa siku ya nne tangu niishi naye akiwa bado hajapata chakula, na chakula chake ni binadamu. Siku zote kichwa kiliniuma kwani sikujua napata wapi chakula chake, nilipojalibu kumuulza mzee Jabir kuhusu chakula cha Nyoka yule, nyoka ambaye sikutakiwa kumfungulia katika chumba cha siri tangu aingie ndani kwangu, kwani ningeweza kuliwa mimi kama sikuwa na chakula cha kumpatia.

"Nyoka huyo atakuwa mtumwa wako maisha yote, atakulinda kila sehemu lakini nguvu zake ziko mikononi mwako. Inatakiwa umpatie chakula, tena chakula chake ni wazazi wako ,na ndipo mfungulie na atakuwa na nguvu za ajabu ",Hiyo ilikuwa ni sauti ya mzee Jabir pamoja na mganga, walipokuwa wakinipa masharti jinsi ya kuishi na nyoka niliyepewa kama zawadi baada ya kumtoa Juliet sadaka. Nikiwa nazunguka sebuleni bila mwelekeo, niliweza kukumbuka maneno ambayo niliweza kuambiwa na wakubwa wangu mala baada ya kukabidhiwa nyoka niweze kuishi naye.

"Sawa nimekubali ",nilijikuta nakubali bila kujitambua, kwani tayali nilikuwa nimeshakuwa muuaji na katili. Nilichokifanya nikuwapigia wazazi wangu,wazazi ambao walinipigia kila siku wakitaka waje kunitembelea,lakini mimi sikutaka waje kunitembelea kwani pengine wangeweza kugundua siri zangu.Lakini baada ya kuambiwa kuhusu kutoa sadaka ya watu niliowapenda sana,mala moja fikra za wazazi wangu zikanijia kichwani kwangu.Ama kweli! shetani alinizidi nguvu kila sehemu,nilifanya maamuzi magumu na bila kujitambua.

"Ngoja waje,kitakacho wakuta hawataamini,"nimaneno ambayo niliyazungumza mala tu baada ya kuwatumia wazazi wangu nauli ya ndege,waweze kuja kunitembelea.Lakini walikuwa wamenigomea kusafiri na basi au treni,kama vile walikuwa wamegundua mipango ya siri tuliyokuwa tumepanga na chama changu cha kishetani,kuwasababishia ajari na kisha kuikamilisha sadaka yangu.

"Hapa kuna jambo sio bure! mitego yote wameikwepa",niliketi tena kwenye sofa huku nikijilaumu,kwani  nisingeweza kuitoa sadaka yangu kwasababu  kulikuwa kunaelekea kupambazuka.

********

Mzimu wa Juliet ulitambua kila kitu kilichokuwa kikiendelea, mipango yetu ya siri kuhusu kuwafanyia mauaji wazazi wangu mala watakapofika nyumbani kwangu, pamoja na kuwatoa sadaka kwa nyoka niliyepewa, yote Juliet aliyatambua. Hivyo hakuwa na budi kuwaokoa wazazi wangu, na pia kufanya kila njia nyoka ashindwe kupata chakula kwani kama angeweza kupata chakula. Juliet angefanya kazi kubwa sana kupambana naye, na asingeweza kuniokoa kirahisi kutoka mikononi mwa utumwa huu wa kishetani niliokuwa nikiutumikia.

"Kuanzia leo mtaishi hapa, mtoto wenu kasafiri, atarudi baada ya siku mbili, mimi ndio mke wake",Juliet aliwakalibisha wazazi wangu kwenye nyumba nzuri sana, pengine nyumba hiyo hata mimi na pesa zote za kishirikina sikuwa na uwezo wa kuimiliki. Mzimu wa Juliet uliongea, ukiwa na uhakika kabisa siku mbili zilitosha yeye kukamilisha kila kitu, na kufichua maovu yote niliyokuwa nikiyafanya.

"Mtoto wetu kweli kapata pesa mjengo wote huu! ……kwelii imana ishimwe ",mama aliongea huku akishangaa jengo kubwa la kifahari, jengo ambalo Juliet alilitengeneza kimaajabu, kiasi kwamba hata mimi nilikuwa sifahamu alitumia uwezo gani wa ajabu kuwafanya wazazi wangu waweze kujiona kama wakiwa ndani ya jengo hili kubwa la Juliet. Jengo ambalo liliundwa katika mazingira ya kutatanisha sana, tena ya ajabu!

**ITAENDELEA **
Powered by Blogger.