Simulizi; NABII WA UONGO **SEHEMU YA 10**









Simulizi; NABII WA UONGO
**SEHEMU YA 10**

Mzimu wa Juliet unafanya kila njia kwa ajili ya kuokoa maisha ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake. Kwa uwezo wake wa ajabu aliokuwa nao, aliweza kuona vita kali ambayo ilikuwa mbele yake. Chama cha kishetani kilikuwa na nguvu ya kutosha kumdhibiti, hasa nyoka mkubwa mwenye vichwa vingi sana ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama hiki cha kishetani.

Juliet anaamua kuwapeleka wazazi wangu, pamoja na wazazi wake, katika nyumba yao. Nyumba ambayo wazazi  wake walikuwa wakiishi siku zote, nyumba ambayo Juliet aliweza kuishi na wazazi wake kabla sijamuua na kumtoa kafara. Haya yote yalitokea baada ya kutoka kanisani  kwangu, siku ambayo alijalibu kutoa siri zangu, lakini nyoka wa ajabu mwenye vichwa vingi sana aliweza   kumzuia na kisha kunisafishia jina langu.

"Wazazi wangu, pamoja na wazazi wa mchungaji! Hapa ndipo mahali sahihi pa nyie kukaa salama mpaka nitakapokamilisha kazi ya kumkomboa mchungaji kutoka katika utumwa huu wa kishetani, "

"Mwanangu hapa nyumbani kwetu patakuaje sehemu salama, halafu bado sijaamini yale uliyoyazungumza kanisani, ni kweli  mchungaji kakuua ",

"Ndio kaniua, lakini nimerudi kumkomboa kwani hayo yote anayafanya bila kupenda, !! sala zenu ndizo zitakazo walinda mikononi mwa watu hawa wabaya ",

Yalikuwa ni mazungumzo ya Juliet pamoja na wazazi wake siku iliyopita, siku ya jumapili. Mala baada ya kutolewa haraka sana kanisani kwangu, huku Juliet akiwalinda na kuwaongoza watoke salama. Juliet baada ya kuhakikisha wazazi wangu pamoja na wazazi wake wakiwa katika mikono salama, alitoweka na kisha kuanza kazi ya kunikomboa na kuyabadilisha maisha yangu.

Alitakiwa kuninyanganya pete ya ajabu, kitambaa pamoja na maji ambayo nilikabidhiwa siku ya kujiunga na chama cha kina mzee Jabir. Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuweza kuniokoa, lakini haikuwa kazi rahisi kwani hakufahamu mahali ambapo nilikuwa nikitunza vifaa hivi ambavyo siku zote nilivitumia siku ya jumapili, na kufanya miujiza iliyonifanya nionekane kama nabii wa kweli.

Siku hiyo hiyo ya jumapili, Juliet alitoweka haraka sana kuelekea Bagamoyo, katika jengo ambalo aliishi mganga, sehemu ambayo yalikuwa ndio makao makuu ya chama chetu. Aliamini kuwa, huko ndiko angeweza kufahamu sehemu ambayo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu.

"Tayali nimefanikiwa kumkomboa kijana wetu,lakini inatakiwa ulinzi uimalishwe katika chumba cha siri, kwani Juliet akifika katika chumba kile na kuchukua vifaa vya kijana wetu, tayali kijana huyu tutaweza kumkosa katika chama chetu ",ilikuwa ni sauti ya Nyoka, nyoka ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu  Nyoka huyu alikuwa akizungumza na mzee Jabir pamoja na mganga, jioni siku ya jumapili. Hawakufahamu kama mazungumzo yao Juliet aliweza kuyasikia, kwani hawakuweza kumuona kutokana na nguvu zake alizokuwa nazo.

Juliet alikuwa tayali amefika katika jengo letu Bagamoyo, na kufanya sala ambayo ilimuwezesha asiweze kuonekana kama alikuwa ndani ya makao yetu makuu. Sala yake iliweza kufanikiwa, kwani alikagua jengo lote akitafuta mahali ambapo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu, lakini hakuweza kugundua kitu. Akiwa amekata tamaa na kutaka kuondoka, ndipo aliposikia mazungumzo ya mkuu wetu pamoja na mzee Jabir yakiendelea. Hatimaye aliweza kugundua mahali ambapo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu, katika chumba cha siri ambacho nilikitumia kwa ajili ya kuua na kutolea kafara.

Aliamini lazima kutakuwa na ulinzi, ilibidi akajipange na kufika katika nyumba yangu siku ya jumatatu Akiwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kupambana na mlinzi yoyote yule atakayemkuta katika chumba changu cha siri.

Hatimaye siku ya jumatatu iliweza kufika, ilionekana kuwa siku nzuri sana kwani kulipambazuka huku hali ya hewa ikiwa nzuri. Jua liliangaza, huku ndege wa angani wakiruka ruka na kuifurahia dunia. Dunia ambayo ilijaa maovu ya kila aina, huku binadamu walioumbwa na Mungu wakiichafua, na kuijazia uovu wa kila aina.

Juliet alifika katika nyumba yangu asubuhi siku ya jumatatu. Alizunguka kila kona ya nyumba yangu lakini hakuweza kugundua chumba changu cha siri. Sikuwa na uwezo wowote wa kutambua uwepo wake ndani kwangu, niliendelea kuketi sebuleni na kufikilia juu ya kitu ambacho kiliweza kutokea kanisani kwangu siku iliyopita. Lakini fikra kuhusu mahali ambapo wazazi wangu walikuwepo ziliponijia kichwani, nilishangaa sauti ya Juliet ikinijibu. Nilipogeuka huku na kule kutazama sehemu ambayo sauti ya Juliet iliweza kutokea, lakini sikuweza kumwona.

Ghafla alijitokeza, na kuonana na mimi uso kwa uso. Alama ya kisu ikiwa shingoni kwake, alama ambayo ilibaki siku ambapo niliweza kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake na kumtoa kafara. Maneno ambayo Juliet aliweza kuyazungumza niliweza kuyapuzia, japo alionekana kuwa na nguvu nyingi za kunikomboa.

Baada ya Juliet kuzungumza na mimi alitoweka mbele ya macho yangu, hali ambayo iliweza kuniogopesha na hofu Yangu kuanza upya. Sikutaka kutoka ndani ya chama changu na kuwa maskini tena, ilibidi nielekee ndani ya chumba changu cha siri na kumuelezea nyoka wangu mdogo niliyepewa kwa ajili ya kuishi naye kile ambacho kilikuwa kimetokea.

Kumbe Juliet alikuwa bado yuko ndani ya nyumba yangu akizunguka huku na kule akitafuta chumba cha siri, japo alitoweka mbele ya macho yangu.

Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya yeye kufanikisha misheni yake,aliweza kugundua fikra zangu na kuanza kunifatilia sehemu ambayo nilikuwa nikielekea.Nilikatiza korido za kutoka sebuleni,na hatimaye kuelekea chumba ambacho niliweza kufunika mlango wake kwa pazia jeusi.Rangi ya pazia,ilifanana sana na ukuta wa nyumba yangu na ndio maana ilikuwa vigumu kwa mgeni yoyote wa nyumba ile kugundua chumba hiki cha siri.

Nilifunua pazia la nyumba yangu na kisha kuingia ndani,kumbe Juliet kwa uwezo wa ajabu aliokuwa nao,kabla hata sijafunga mlango na yeye aliweza kuingia haraka ndani ya chumba kile.Nilipofunga mlango tu ,sikuamini kile  ambacho kiliweza kutokea.

"Nyankii,nyankii,ingririii!nyanki nyanki ingriiriiii……",zilikuwa ni kelele za nyoka wangu,kelele ambazo zilipangiliwa kwa mpangilio mzuri,bila shaka nyoka yule alikuwa akiimba wimbo.

Nilimshangaa sana nyoka wangu,hakuonekana kujali uwepo wangu ndani ya chumba kile,bali aliimba wimbo huku akionekana kutazama pembeni ya ukuta.Lakini kwa upande wangu,ilibidi nimshangae tu na kushindwa kumwelezea jambo ambalo lilinipeleka ndani ya chumba kile,chumba ambacho kilitisha sana kwani kilipambwa kwa mashuka yenye rangi nyeusi,nyeupe,pamoja na nyekundu.Rangi ambazo sikuzote sikujua zilimaanisha nini,na kwanini sikuambiwa kuweka mashuka yenye rangi tofauti na hizi.


"Puuuuuuuuuuuh! " ulikuwa ni mlio wa sauti nzito,sauti ambayo iliashiria kitu kizito kiliweza kudondoka chini.Haraka sana niligeuza macho yangu,kuangalia sehemu ambayo mlio wa sauti ile uliweza kutokea.Sehemu ile ile ambayo nyoka wangu alikuwa akiangalia huku akiimba.

Sikuamini nilichokiona,Juliet alikuwa amedondoka chini huku damu zikimtoka mdomoni.Nyoka aliyepewa majukumu ya kunilinda,na kulinda chumba cha siri ,ndiye aliyesababisha Juliet kudondoka chini.Kwa upande wangu nilipigwa na butwaa kumshangaa tu Juliet,kwani sikufahamu kama alikuwa bado ndani ya nyumba yangu akinipeleleza aweze kutambua chumba changu cha siri.

Hatimaye niliweza kutambua chanzo cha nyoka wangu kuimba nyimbo ile,nyimbo ya kiasili iliyoonekana kuwa na nguvu sana pale inapoimbwa mbele ya Juliet.Isitoshe! ndipo nilipogundua ni kwanini chumba changu Juliet hakuweza kukitambua kutokana na pazia jeusi nililoliweka katika mlango wa chumba cha siri,kuwa na nguvu za ajabu ambazo zilifanya viumbe wa ajabu kutotambua chochote kile.Na ndio maana ndani ya chumba cha siri,rangi nyeusi ilikuwa moja kati ya rangi za mashuka ambazo zilitumika kupamba chumba kile.

Hatimaye Juliet alikuwa mikononi mwetu,kwa mbali nilimuonea huruma.Lakini sikuwa na la kufanya,mimi nilikuwa mdogo sana katika chama chetu na sikuwa na madaraka yoyote.Ghafla radi zilipiga,tetemeko la ardhi likapita kwa sekundee kadhaa.Kufumba na kufumbua,Nyoka mkubwa ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu,mzee Jabir pamoja na mganga,walitokea ndani ya chumba changu cha siri.Sikutambua ni jambo gani walitaka kulifanya,mbele ya mzimu wa Juliet.

*ITAENDELEA*

Mzimu wa Juliet umekamatwa katika harakati za kumkomboa mchungaji wa uongo, Hakika!!

Tukutane sehemu ya 11
Powered by Blogger.