Simulizi; "THE BLACK KILLER "
(muuaji mweusi)
Mwandishi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU 04**
Baada ya muda wa takribani masaa mawili, gari dogo aina ya taksi, lilipaki nje ya hoteli kubwa ya kitalii ya Kasabranka. Mziki mnene ulisikika huku biashara za kila aina zikifanyika katika hoteli ile, "Take your money……and thank you "(chukua pesa yako……na asante) Godfrey alimlipa pesa ya kutosha dereva wa taksi na kisha kumshukuru. "Thank you alot ……Africans"(asante sana …Waafrika) dereva yule alipokea na kushukuru sana kwani alilipwa pesa nyingi, takriban dola mia mbili sawa na zaidi ya shilingi laki tano za Kitanzania.
Godfrey na wenzake walichukua vyumba vya kulala wageni katika hoteli ya Kasabranka, na kukataa kulala katika nyumba za wageni walizokuwa wameandaliwa na serikali ya Marekani ili tu waweze kupeleleza kwa siri, katika hoteli ya Kasabranka baada ya kukisia kuwepo kwa Paul Agustino katika hoteli hiyo kutokana na taarifa walizopewa na dereva taksi. Bila kutegemea siku zilizidi kukatika, bila kutambua kitu chochote kuhusu Agustino na mahali alipo.
********
Paul Agustino aliendelea kukaa katika hoteli ya Kasabranka akisubilia kuitwa na matajiri waliokuwa wakimtumia kwa kazi mbalimbali, bila kutambua kuwa kuna baadhi ya askari walikuwa wameshawasili katika hoteli hiyo kumkamata.
Ilikua ni jioni nzuri iliyokuwa inaangazwa vema na mbalamwezi, huku upepo mzuri ukivuma na kuipendezesha mandhari ya nje ya hoteli ya Kasabranka. Msichana mrembo Jacline akiwa ameketi nje akipunga upepo, kwa mbali alimuona mwanaume handsome na mtanashati akipita mbele yake. Hisia za mapenzi zilimuingia Jacline, na kujikuta akitamani kumpata mwanaume yule awe mpenzi wake.
"Jina langu naitwa Mr Pius …nafurahi sana kukutana na muafrika mwenzangu kama wewe katika nchi ya ugenini ……" bwana Paul Agustino alijitambilisha kwa jina la uongo mbele ya msichana mrembo Jacline. "Nafurahi pia kukutana na mwanaume mtanashati wa kiafrika nikiwa ugenini ……sijui umejuaje kama nafahamu Kiswahili " Jacline aliongea kwa tabasamu nzuri zenye hisia za mapenzi ndani yake mbele ya Paul Agustino, aliyejitambulisha kama mr Pius. "Hahaha…Mswahili anajulikana popote pale"Paul Agustino alicheka huku akifurahi kukutana na msichana mrembo sana Jacline, moyoni aliapa kumpata Jacline kwa gharama yoyote ile awe kama mpenzi wake bila kutambua kuwa Jacline ni mmoja kati ya askari hodari watatu waliotumwa kuja kumkamata.
"Samahi mr Pius, unatokea nchi gani Afrika?? ",Jacline alimuulza bwana Paul Agustino huku akimwita kwa jina la mr Pius, jina ambalo Paul alidanganya tangu alipofika katika hoteli ya Kasabranka kwa mara ya kwanza. "Natokea nchi ya Tanzania, nchi ambayo mrima mrefu barani Afrika ……mrima wa Kilimanjaro unapatikana ",Bwana Paul aliongea na kuisifia nchi ya Tanzania na kumfanya Jacline atabasamu kwani alimuona Paul kama mzarendo wa nchi yake.
Ghafra ujumbe mfupi wa barua pepe uliingia katika simu ya Paul, kutokana na siri nzito iliyokua moyoni mwake hakuweza kumwamini mtu yeyote hivyo aliufungua na kuusoma kwa siri bila Jacline kufahamu chochote. "Samahani mrembo ……ukinihitaji napatikana chumba namba mia moja, ghorofa ya kumi. ……nimechoka sana ngoja nikapumzike " ,Paul alikatisha mazungumzo na Jacline haraka sana na kisha kuondoka haraka eneo lile na kumwacha Jacline akipigwa na butwaa.. Kutokana na Paul Agustino kubadilisha sura yake, Jacline hakuweza kumuhisi kuwa ndiye bwana Paul Agustino, jambazi katili walilokuwa wakilitafuta bali aliamini kuwa ni mr Pius ambaye alikuwa raia wa Tanzania huku akiwa hatambui kazi yake kwani mazungumzo yao yalisitishwa ghafra bila Jacline kuitambua sababu iliyosababisha Paul kuondoka haraka kiasi kile.
"Nitamtembelea kesho chumbani kwake ……"Jacline aliongea kwa sauti ya chini peke yake huku akielekea chumba namba tano, ghorofa ya kwanza. Jacline na wenzake waliamua kuishi vyumba vya ghorofa ya kwanza ili angalau waweze kuona watu waliokuwa wakiingia na kutoka hotelini hapo, kama wangeweza kubahatisha kuiona sura ya Paul Agustino..
Baada ya Paul kupokea ujumbe mzito kuhusu kukamatwa kwa waziri Sarehe, na kuifahamisha serikali kuhusu kuwepo hai kwa Paul Agustino na wala hakuwa amekufa kama ilivyojulikana, Paul alichanganyikiwa ghafra na kujikuta akielekea chumbani haraka sana ili aweze kuvaa miwani yake iliyomuwezesha kuona kila kitu katika mwili wa yeyote yule aliyekuwa mbele yake. Miwani hii ingemsaidia kugundua watu ambao hawakuwa salama kwake pale hotelini.
"Waziri ni mpuuzi, kwanini aseme kila kitu kuhusu mimi mpaka kuhusu swala la mimi kutorokea huku Newyork ……inatakiwa nianze kuua baadhi ya watu wanao fahamu siri zangu ili kujilinda "Paul aliongea huku akiwa amejilaza kitandani akisoma kwa kurudia rudia ujumbe aliokuwa ametumiwa na bwana Benedict, ujumbe ambao ulimfahamisha juu ya kuwasili jijini Newyork kwa askari waliotumwa kumkamata.
…………………………………
Jacline akiwa mwenye kusumbuliwa na mapenzi,alishindwa kulala kwani alikosa usingizi kabisa akimfikiria Paul Agustino ,kijana aliyejitambulisha kama mr Pius na kuziteka hisia za Jacline.
"Lazima nimpate kwa gharama yoyote ile,kesho kukipambazuka ……jambo la kwanza naamkia chumbani kwake",Jacline aliendelea kusumbuliwa na hisia za mapenzi na kufikia uamuzi wa kuonana na Paul,asubuhi iliyofuata.
Godfrey na Jonson wakiwa katika hali ya kukata tamaa,wanajikuta wakisumbuliwa na mawazo mengi kwani shughuri ilizidi kuwa ngumu siku hadi siku huku matarajio ya kumkamata Paul yakiwa yametoweka ghafra."Nimepakumbuka nyumbani ……nakupenda sana Afrika kusini"Jonson aliongea peke yake kwa sauti ya chini huku akiwa anatazama kitambaa chake cha mkononi chenye bendera ya nchi yake."Usjali ipo siku utarudi ukiwa na medali ya ushindi shingoni mwako," Godfrey kijana jasiri wa Kitanzania alimtia moyo Jonson baada ya kuyasikia maneno aliyoyatamka.
Ndi…ndii…ndiii…kengele ilipiga fujo na kumshtua kutoka usingizini bwana Paul,akiwa amevalia bukta na singrendi na kufanya kifua chake kuonekana vizuri. Alikwenda kufungua mlango wa chumba chake haraka sana kwani alidhani muhudumu wa hoteli alikuwa amemletea chai kama ilivyo kawaida.
"Waaaaooh kumbe ni wewe mrembo,karibu sana"Paul aliongea kwa sauti iliyojaa tamaa ya mapenzi huku akimkumbatia Jacline."Aaasantee…nte"Jacline alijibu kwa kusita sita huku wakiwa wamekumbatiana na Paul,hali iliyowafanya wote kuzidiwa na tamaa za mwili na kujikuta wakishiriki tendo la ndoa bila kutegemea.
Bila kutegemea Jackine akiwa haamini kilichotokea,alitabasamu na kupuuzia mawazo ya kujuta kukubali kutoa penzi kwa mwanaume asiyemtambua kwa undani zaidi na kuendelea kupumzika katika kifua cha Paul,huku moyo wake ukiwa na furaha kumpata mwanaume aliyetokea kumpenda sana.
"Mhhh siamini macho yangu……hichi kitambilisho cha jeshi cha Paul Agustino kimefikaje hapa…"Jacline aliongea kwa sauti ya chini sana huku akishangaa kitambulisho cha jeshi cha Paul Agustino,mara tu alipoamua kukagua mifuko ya suruali ya Paul ambaye Jacline alimfahamu kwa jina la Pius,wakati Paul akiwa ameenda bafuni kuoga.
*ITAENDELEA**