SIMULIZI YA KUSISIMUA-SIMULIZI YA KUSISIMUA
SIMULIZI YA KUSISIMUA
"Nastahili kunyongwa, hukumu ya kifungo cha maisha sio haki yangu ……nastahili kufa, kifo ni haki yangu "
Simulizi; "THE BLACK KILLER "
(..Muuaji mweusi..)
Mwandishi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 01**
Nchi ya Tanzania inakumbwa na janga la kutisha, kila kona ya nchi vilio vya wananchi masikini vikisikika baada ya kupoteza ndugu zao katika mlipuko wa bomu uliotokea siku ya kusherekea sikukuu ya uhuru wa Tanzania.
Vyombo vya usalama nchini Tanzania vikishirikiana bega kwa bega kutambua chanzo na muhusika wa mlipuko huo, huku vijana wengi na baadhi ya wanasiasa wakikamatwa na kutiwa rumande kwani walituhumiwa kuhusika na tukio hilo baada ya kura za maoni kupigwa kubaini wahalifu hao.
"Hii ni taarifa ya habari kutoka "TBC ", hali ya raisi wa Tanzania inaendelea vizuri na sasa karejea kutoka nchini india kwenye matibabu ………raisi wa Tanzania mheshimiwa Samuel Kizito anawapa pole wafiwa wote na majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea huku akiomba radhi kwa vifo na kujeruhiwa kwa baadhi ya viongozi wakubwa wa nchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo " …Sauti ya mtangazaji wa televisheni ya taifa ilisikika, na kumfanya afande mpelelezi wa Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam bwana Godfrey Manumbu kusitisha shughuli zake na kuwa makini kusikiliza taarifa ile ya habari .
"Angalau tutaanza kupumua japo kazi bado ni ngumu, lakini muhusika wa tukio hili alikusudia nini mpaka kuua maelfu ya watu wasio na hatia??, na kwanini kaamua kutugawa watanzania? Kwa sasa wananchi wanatuchukia sana, kwani wanatuona kama wazembe na hatufatilii kutambua muhusika wa janga hili ni nani………" Afande mpelelezi bwana Godfrey Manumbu aliendelea kujiuliza maswali mengi kichwani yasiyo na majibu.
………………………………
Siku zilizidi kusonga mbele huku nchi mbalimbali zikiilaumu serikali ya Tanzania kwa kutodumisha ulinzi imara siku ya sherehe za uhuru, na kupelekea vifo vya viongozi wa nchi zao. Mlipuko huu uliidhoofisha sana nchi katika nyanja zote za maendeleo, kwani hata urafiki wa Tanzania na nchi nyingi walizoshirikiana kibiashara ulitoweka kabisa.
"Just go to join the police force of Tanzania, we want to know the killer of our honourable president………I trust you my soldiers " (nendeni muungane na jeshi la polisi la Tanzania ,tunahitaji kufahamu muuaji wa mheshimiwa raisi wetu……nawaamini sana askari wangu ") sauti ya amri ilisikika kutoka kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa nchi ya Afrika kusini, bwana Jacob Nelson akiwatuma vijana wake nchini Tanzania kumtafuta mtuhumiwa huyo aliesababisha kifo cha raisi wao mheshimiwa Jackson Mbeki.
…………………………………
Ndege kubwa aina ya Boeing 777 inayomilikiwa na kampuni kubwa ya usafiri wa anga "Fly emirates " inagusa ardhi nzuri ya jiji la New York nchini Marekani.Kijana mtanashati Paul Agustino anashuka kwenye ndege akiwa amebeba briefcase yenye mabilioni ya pesa, baada ya kufanikiwa kutega bomu katika sherehe za uhuru nchini Tanzania. "Thanks to God, aim safe now……hahahaha " (Asante mungu, niko salama sasa ……hahaha).Kijana muuaji na katili akiwa amevaa suti nyeusi pamoja na miwani ya gharama sana iliyomuwezesha kuona kila kitu katika mwili wa yeyote yule aliyekua mbele yake, alizungumza kwa sauti ya chini na kisha kucheka kwa furaha baada ya kufanikiwa kutoroka nchini Tanzania.
Alitembea kwa wasiwasi na umakini mkubwa, huku akikwepa askari waliokuwa wakifanya ukaguzi wa kila raia wa kigeni aliyeingia na kutoka nchini Marekani.Kutokana na taarifa za mauaji yaliyotokea nchini Tanzania kusambaa duniani kote, bwana Paul Agustino alitumia mafunzo yake ya kikomando aliyoyapata nchini Urusi kutoroka bila kugundurika na mtu yeyote katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Newyork internatinal airport.Paul Agustino aliwahi kuwa komando wa jeshi la ulinzi la Tanzania kabla ya kujiingiza katika ugaidi na ujambazi wa kutumia siraha kwasababu ya tamaa ya pesa.
"Hey boy ……take me to Casabranca Hotel as soon as possible …I will pay you well "(Kijana ……nipeleke katika hoteli ya kasabranka haraka iwezekanavyo ……nitakulipa vizuri " )Paul Agustino akiwa mwenye kuhema sana baada kuruka ukuta wa uzio wa uwanja wa ndege na kukata nyaya zilizopeleka mawasiliano katika cctv Camera ili asijulikane, anajipakia kwenye taxi na kisha kumuomba dereva kumtoa haraka sana mahali pale.
"Whatsup ……nigga "you will give me only fifty dollars "(sawa……niga utanilipa dola hamsini tu) dereva alimjibu Paul Agustino na kisha kuondoa gari kwa kasi sana, hakua na hofu yoyote kwani alizani Paul alikuwa ni "brack American " (mmarekani mweusi )……hivyo alimchukulia kama raia wengine tu wa Marekani.
Muda si mrefu gari lilitua pembeni ya hotel kubwa ya kitalii ya Kasabranka, huku kijana Paul Agustino akiwa na furaha sana kufika mahali apo baada ya kukubaliana na dokta Benny Hanson wakutane mahali hapo ili kupanga mipango ya kumuwekea Paul sura bandia.
,…………………………………
Nchini Tanzania afya ya raisi mheshimiwa Samuel Kizito ilizidi kuimalika siku hadi siku, huku akitembea kwa kuchechemea baada ya kuwekewa miguu ya bandia. Raisi wa Tanzania Samuel Kizito alinusurika kufa baada ya mlipuko wa bomu kupitia miguu yake na kuisaga kabisa huku mlinzi wake akipoteza maisha kwani alimkumbatia ili kumuokoa raisi,na kuunguzwa mgongoni na kichwani na moto uliotokana na bomu hilo.
"Welcome Tanzania my friends, feel at home "(Karibuni Tanzania rafiki zangu, mjiskie mko nyumbani) afande mpelele zi wa jeshi la polisi bwana Godfrey Manumbu aliwakaribisha kwa furaha askari wawili kutoka Afrika kusini ,waliotumwa kwa ajiri ya kushirikiana na askari wa Tanzania kumsaka muhusika wa mlipuko wa bomu uliotokea na kureta maafa makubwa.
"My name is police inspector Jonson ……nice to meet you ",(jina langu ni mkaguzi wa polisi Jonson ……nafurahi kukutana na wewe), "my name is Jacline ……nice to meet you (Jina langu naitwa jacline……nafurahi kukutana na wewe).…askari wale walijitambulisha majina yao na kisha kupanda defender ya polisi kwa ajili ya kuelekea ikulu.
…………………………………
Dokta Benny Hanson anafanikiwa kuibadirisha sura ya Paul Augustino, shughuli iliyofanyika kwa siri ndani ya chumba cha wageni katika …
"Doctor Benny your the best, I have changed alot in such a way that even my woman can not identify me …"(Dokta Benny wewe ni bora zaidi, nimebadilika sana kiasi kwamba hata mwanamke wangu hawezi kunitambua ).....Paul Agustino alizungumza kwa furaha huku akimuhesabia pesa nyingi dokta Benny, kama malipo ya kazi kubwa aliyoifanya.
"Don't worry young boy …this is my job "(usjali kijana …hii ni kazi yangu) dokta Benny alimjibu Paul huku akihesabu pesa zake kama zilikua zimekamilika.
………ITAENDELEA ……
"Doctor Benny your the best, I have changed alot in such a way that even my woman can not identify me …"(Dokta Benny wewe ni bora zaidi, nimebadilika sana kiasi kwamba hata mwanamke wangu hawezi kunitambua ).....Paul Agustino alizungumza kwa furaha huku akimuhesabia pesa nyingi dokta Benny, kama malipo ya kazi kubwa aliyoifanya.
"Don't worry young boy …this is my job "(usjali kijana …hii ni kazi yangu) dokta Benny alimjibu Paul huku akihesabu pesa zake kama zilikua zimekamilika.
………ITAENDELEA ……