Simulizi; NABII WA UONGO **SEHEMU YA 13*









Simulizi; NABII WA UONGO
**SEHEMU YA 13*

Kuzimu;
     Mzimu wa Juliet unajitahidi kuponyoka kutoka katika kifungo ,katika gereza ambalo lililindwa na nyoka hatari sana, nyoka ambao waliimba nyimbo za asili. Nyimbo ambazo zilidhoofisha nguvu za Juliet, kiasi kwamba alishindwa kujikomboa na kueendeleza harakati za kunikomboa.

Nguvu zilimuishia mwilini mwake, damu zilimtoka mdomoni kadri ambavyo nyoka wale hatari walivyokua wakiimba nyimbo.Kadri damu zilivyozidi kumtoka mdomoni ndivyo nguvu zilimuishia zaidi na zaidi, kiasa kwamba kulikua na uwezekano wa kushindwa kukamilisha misheni yake iliyomurudisha duniani.


Dar es salaam
        Hatimaye wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, walianza harakati za kurudisha nguvu za Juliet. Walitakiwa kufunga na kuomba, kwa muda wa siku mbili, kama jinsi walivyokua wameambiwa na binadamu wa ajabu ambaye aliwatokea katika mazingira ya kutatanisha.

"Ni siku ya kwanza ya maombi, tunapaswa kutimiza kama ambavyo tuliweza kuambiwa, maisha ya mchungaji yako mikononi mwetu " ,

"Nitashukuru kama mwanangu ataweza kubadilika, na kuwa mtu mwema, nashukuru sana kwa msaada na umumilivu wenu, mmempoteza binti yenu, lakini hamjaonesha chuki yoyote baina yetu",yalikuwa ni mazungumzo ya wanawake wawili,wanawake ambao kwa muda mfupi tu tangu wafahamiane.Waliweza kupendana sana na kuwa kama ndugu.Mazungumzo yao,yaliendelea baada ya kumaliza maombi na kuketi kwa ajili ya kubadilishana mawazo.Wanaume wakiwa peke yao,wanaume ambao alikuwa ni baba yangu pamoja na baba yake Juliet.Lakini pia,wanawake waliweza kuketi peke yao,na kubadilishana mawazo.

"Nisamehe ndugu yangu, sikujua kama mwanangu ni mtu mubaya kiasi hiki ",

"Usjali mzee mwenzangu, watoto wetu wa siku hizi wanataka mafanikio ya haraka ,tofauti na enzi zetu!  Lakini naamini tukimaliza maombi ya siku hizi mbili, kila kitu kitakua sawa ……", yalikua ni mazungumzo kati ya baba yangu, pamoja na baba yake Juliet. Baba yangu muda mwingine alijiona mwenye hatia, kwani Juliet aliuawa na mimi mwanae, ambaye nilijifanya nabii wa kweli kumbe sivyo, na kumtoa Juliet kama kafara kujiongezea utajiri, huku nikidanganya watu mbalimbali katika kanisa langu.

Bagamoyo;
         Kasri la chama chetu cha kishetani, kasri ambalo liliundwa kwa jengo ambalo lilionekana kuwa la kale. Hali ya furaha ilitawala tofauti na awali, kwani mzee Jabir pamoja na mganga walionekana kuwa na nyuso zilizopambwa kwa tabasamu muda wote. Hofu za kuuawa na Juliet, zilitoweka kabisa, kwani waliamini Juliet asingeweza kutoroka na kutoka kifungoni, kuzimu.
Tofauti kabisa na fikra zao, hawakutambua kama harakati za kumuokoa Juliet kutoka kifungoni, zilikuwa zimeanza. Muda wowote baada ya siku moja mbele, mzimu wa Juliet ungeweza kutoka kuzimu na kukamilisha lengo lake, lengo la kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani.

Kipindi yote hayo yakitokea, mkuu wa chama chetu, nyoka wa ajabu aliyekuwa na vichwa vingi sana, alikuwa amelala tu baada ya shughuli nzito aliyokuwa ameifanya kuweza kukamilika. Mawazo ya nyoka hayakutofautiana na mawazo ya mzee Jabir pamoja na mganga, aliamini kwa asilimia zote kuwa mzimu wa Juliet usingeweza kutoka kuzimu, kwani haukuwa na nguvu zozote za kufanikisha jambo hilo. Hata hivyo, kama mzimu wa Juliet ungefanikisha kutoka gerezani, lakini ilikua ni ngumu kulishinda nguvu ya jeshi la kuzimu, jeshi ambalo liliongozwa na mtu aliyetukaribisha mala ya kwanza nilipofika kuzimu, mtu huyu aliyeonekana kuvalia mavazi ya kifalme, sikuweza kufanikiwa kulifahamu jina lake, kwani niliogopa sana kumuuliza na kujikuta nikitoka kuzimu mala baada ya kwenda kumfunga Juliet, bila kulitambua jina lake.

Kuzimu;
       Baada ya siku moja na masaa kadhaa kupita tangu wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet kufunga na kuomba, kama jinsi walivyokuwa wamepatiwa maelekezo. Damu zilianza kupungua kuchuruzika kutoka mdomoni mwa mzimu wa Juliet, alianza kufumbua macho kwa mbali sana, na kushuhudia nyoka waliokuwa wakimlinda, wakiendelea kuimba huku wakipuliza filimbi.

Nyoka baada ya kumuona Juliet akifumbua macho kwa mala nyingine, tangu alipofungwa, walianza kuimba wimbo wao wa kiasili kwa fujo sana ili kudhoofisha nguvu zake zisiweze kurudi, na kuleta balaa.

"Nyankii, nyakiii …nyakii! ingriiii ……!nyankii ingriiii ……nyankii ingriiiii",sauti nzuri za nyimbo ziliendelea kusikika, nyoka walinzi ambao walikuwa wakimlinda Juliet katika gereza la kuzimu,  waliendelea kuimba ili kudhoofisha nguvu za Juliet. Hali ya taharuki iliwakumba walinzi hawa, kwani japo waliimba nyimbo hizi, nyimbo za ajabu ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya nguvu za binadamu wa ajabu kama Juliet, lakini tofauti na awali, Juliet hakutokwa na damu mdomoni tena. Bali alifumbua macho na fahamu zilianza kumrudia taratibu.

…………………………………

Maombi ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, ndiyo yaliyopelekea Juliet aweze kupata fahamu. Na kadri masaa yalivyosonga mbele, ili siku mbili ziweze kukamilika, ndivyo ambavyo nguvu za Juliet ziliweza kurudi maradufu, na kuwa za kutisha tofauti na awali.

*ITAENDELEA *

Mzimu wa Juliet utafanikiwa kutoka kuzimu?? Na kuendeleza harakati za kumkomboa mchungaji ………
Powered by Blogger.