HABARI NA HISTORIA YA KABILA LA WANGONI NA MGAWANYIKO WA MAJINA YAO.









HABARI NA HISTORIA YA KABILA LA WANGONI NA MGAWANYIKO WA MAJINA YAO.
Wangoni, ni moja ya kabila linalopaikana nchini Tanzania na sehemu zingine za kusini mwa bara la Afrika.
Na kutokana na kabila hili kupita sehemu mbalimbali wakitokea kusini mwa Afrika mpaka Afrika ya kati na mashariki,kuna mengi ya kujua.
Kimasingi kuna aina mbili za Wangoni, kuna Wangoni asilia na kuna Wangoni wa kujiita tu. Wangoni wa asili ni wale ambao chimbuko lako ni kusini mwa Afrika.
Na Wangoni wa kujiita hawa ni wale wakazi waliokutwa kwenye maeneo yao na kuamua kujiita Wangoni kwa sababu mbalimbali ambazo wao walikuwa nazo(nitafafua hili kwa kina hapa chini). Kwa ujumla Yapo mengi sana ya kusimulia juu ya kabila hili la Wangoni. Ila kwa leo tutajadili mgawanyiko wa majina ya Wangoni.
Ukweli ni kwamba, Wengi tumekuwa tukifahamu kuwa Wangoni wanapatikana mkoani Ruvuma hasa kwenye wilaya ya Songea. Na kutokana na kabila hili kuwa kubwa na kuwa na uwezo wa kutawala sehemu hizo imekuwa kama wao ndio wakazi asilia wa Songea na baadhi ya sehemu ya mkoa wa Ruvuma.
Lakini ukweli ni kwamba, kulikuwa na wakazi waliopata kuishi hapo hata kabla ya ujio wa Wangoni kwenye ardhi ya Ruvuma. Kwa mfano kulikuwa na makabila kama Wandendeule, Wayao, Wanyanja, Wamatengo na Wanindi.
Lakini kwa kuwa makabila haya yalikuwa hayana nguvu kivita, yakajikuta yakiwa chini ya kabila la Wangoni. Hivyo wapo waliokubali kutumia majina ya Wangoni ili kuleta heshima na wapo waliokataa kujiita majina ya Wangoni kama sehemu ya kupinga uwepo wao.
Sasa wale waliojiita Wangoni mambo yalikuwa kama hivi, kulikuwa na Mngoni mmoja aliyefahamika kwa Jina la Mtepa Gama. Alisifika kwa mapambano na kuteka baadhi ya makabila. Sasa wale waliotekwa waliamua kujiita na wao Mtepa ili kuonekana kuwa wao ni ukoo mmoja na Mtepa Gama.
Na mateka hao walipozaa watoto waliamua kuwaita Gama. Sababu za kuwaita watoto hao jina la Gama ni kwamba, watoto hao ni mali ya Mtepa Gama. Hivyo watoto wao wakahesabika kama mali ya Mtepa Gama. Na hivyo wakajikuta wanajenga ukoo ambao una jina ambao waanzilishi waliamua tu kujiita Wangoni kwa sababu zao. Na ndio hao Wangoni wa Kujiita.
Na wale Wangoni wa asili nadhani hakuna haja ya kufafanua kwa kina kwani, majina yao walikuwa wanayarithii kutoka familia hadi familia na kutoka ukoo hadi ukoo. Na sababu za wao kujiita majina hayo yanafahamika waziwazi tofauti na wale Wangoni waliokuwa wanajiita kwa sababu za kiutawala.
Kwa ujumla tunaweza kuyagawa majina ya wangoni katika mkundi yafuatayo. Na mgawanyiko wa majina haya yalitegemea sehemu walizokuwa wanafika na kuanzisha maisha yao huko.
1. Wangoni Waswazi: hili ni kundi la Wangoni ambao walipata majina yao wakiwa kwenye ardhi ya Waswazi ambapo walizaliana na kukutana na wakazi wa hapo ndipo kukapatikana majina hayo. kwenye kundi hili kuna majina kama Gama, Tawete, Chingwe,Magagura,Mswami,Maseko,Nyumayo,Ole, Jere ,Mshanga,Masheula, Nkosi, Mlangeni Na Malindisa.
2. Wangoni Watonga: hawa ni wale Wangoni waliopata majina yao wakiwa kwenye ardhi ya Watonga.na ndipo jina lao lilipobadilishwa kutoka Wanguni na Wangoni. Kuna majina kama, Makukura,Silengi,Ntocheni, Sisa, Ntani, Ngairo,Nguo, Matinga,Nkuna,Gomo na Pili.
3. Wangoni Wasenga: hawa ni wale Wangoni waliopata majina yao wakiwa maeneo ya mto Zambezi mpaka kufikia maeneo ya Malawi. Kwenye kundi hili kuna majina kama,Lungu, Tembo, Njovu, Nguruwe,Ng’ombe, Mumba Na Mwanja.
4. Wangoni Wakalanga: hawa ni Wangoni waliopata majina wakiwa kwenye ardhi ya Wakalanga. Kwenye kundi hili kuna majina kama Mbano, Soko, Moyo,Zenda,Newa, Shonga, Shawa, Chiwambo, Hara, Mapara, Mteka Na Nyati.
5. Wangoni Wasukuma. Hawa ni wale Wangoni waliopata majina yao wakiwa usukumani na unyamwezi.hawa walipewa jina moja ya Watuta. Kwenye kundi hili kuna majina kama.Chisi, Ntara,Mpepo, Satu,Zinyungu, Chawa Na Mzila.
6. Wangoni Wandendeule: hawa ni Wangoni waliopata majina wakiwa kwenye ardhi ya Songea. Kwenye kundi hili kuna majina kama, Ngonyani, Mapunda,Ntini, Milinga,Nyoni,Henjewele,Ponera,Luhuwa, Nungu,Mango, Nyimbo, Humbaro,Kigombe, Wonde, Ndomba, Tindwa, Maginga na Luambano.
7:Wangoni Wamatengo: hawa ni wale Wangoni waliochanganyika na kabila la Wamatengo waliowakuta hapo Songea: kwenye kundi hili kuna majina kama,
Nchimbi,Ndunguru,Komba,Nyoni, Kapinga, Kifaru, Pilika, Hyera, Mbele,Mkwera, Ndimbo, Mapunda, Ngongi, Mbunda, Kinyero,Nombo na Kumburu.
8: Wangoni Wapangwa: hawa nao ni wale wangoni waliopata majina kutokana na kujichanganya na Wapangwa waliokuw wanapatika hapo Songea kabla ya Wangoni kufika. Kwenye kundi hili kuna majina kama, Mhagama,Kimhwili, Nditi, Kugongo,Njombi,
Mwingira,Kihaule, Mbawala, Njerekela, Komba, Kayombo, Luena,Mbena,Mwagu, Mlimara, Sanga, Kokowo,Miloha, Kihuru, Chali Mwinuka, Nyilili, Mkuwa, Mhonyo, Mkinga, Ngoponda na Goliyama.
Wandendeule kwa kiasi kikubwa hawa asili yao ni Wapangwa ambao asili yao ni Songea.
Kabila la Wandendeule lilitokana na tukio la Wangoni kuwavamia Wapangwa waliokua wenyeji wa Songea. Hivo Wapangwa wakaamua kuihama songea kutokan na kupigwa na Wangoni na kukimbilia maeneo mengine ya Ruvuma hasa Namtumbo.
Kabila la Wandendeule lilitokana na Neno "NDANDAVULE" maana yke ni NTAFANYAJE! Yaaan wafanyeje baada ya kuvamiwa na Wangoni! Ndio wakaamua wakimbilie na kuanzisha utawala wao maeneo ya Namtumbo CHINI ya Chief wao waliompa jina la Chief NAMTUMBO.
Kiujumla MKOA wa Ruvuma ni MKOA wa kipekee kwani ndio mkoa unaokaliwa na makabila mengi yaliyokua na himaya zao kuliko MKOA wowote hapa Tanzania.
1. Wangoni -Songea
2.Ndendeule- Namtumbo
3.Yao - Tunduru
4.Matengo - Mbinga
5.Wanyasa - Nyasa
6. Wapangwa- Ruvuma yote wamechanganyika
7.Wanindi- Wamechanganyika.
8.Wamagingo -Wamechanganyika na ni wachache sana.
*Makala hii ni sehemu tu ya historia ya Wangoni, hivyo mawazo yako yanahitajika sana.
Powered by Blogger.