Simulizi; "NABII WA UONGO "


Simulizi; "THE BLACK KILLER "         (muuaji mweusi)
**SEHEMU YA 03**

Nikiwa ndani ya chumba changu cha siri, jasho jembamba lilianza kunitoka kutokana na hofu niliyokuwa nayo, hasa baada ya kumuua kikatili Juliet. Kwani tangu nijiingize kwenye unabii wa uongo, sikuwahi kuua hata siku moja japokuwa nilitakiwa nitoe sadaka ili nizidi kukubalika katika jamii na kujipatia utajiri mwingi.

"Hapa inatakiwa  nitamke maneno ya kumwita mtukufu Nyoka, aweze kupokea sadaka yangu ",damu zikiwa zimenitapakaa mwilini, niliangalia saa lakini muda ulikuwa unazidi kwenda, kwani tayali ilikua imefika saa tano usiku.Nilizungumza peke yangu huku nikijiweka tayali kwa ajili ya kumuita  Nyoka yule wa ajabu, nyoka aliyekuwa kama Mungu wangu ili aweze kuipokea sadaka yangu niliyomtolea na asiweze kuniazibu.

"Nyoka njoo Nyoka!, Ni mimi Hakika Nyoka!, Njoo uchukue chakula Nyoka!, nimekuandalia Nyoka……!",niliimba wimbo huu huku nikirudi kinyume nyume. ,na kisha tena niliweza kusogea mbele. Huu wimbo, ndio wimbo ambao mzee Jabir alinifundisha na kunitaka niweze kuuimba pale nitakapotaka kumtolea Nyoka sadaka.


Lakini baada ya kuimba kwa muda mrefu huku nikicheza, nilijikuta nikikata tamaa kwani Nyoka yule wa ajabu hakuweza kutokea. Taratibu nilianza kupunguza kasi ya kuimba tofauti na mwanzoni, huku nikiwa uchi wa mnyama na kichwani kwangu niliweza kujifunga kitambaa chekundu vazi pekee nililotakiwa niwe nalo wakati wa kutoa sadaka.

"Nyoka njoo Nyoka!, ni mimi Hakika Nyokaa!, nimekutayalishia chakula Nyokaaa, njoo ule nyo…ka…a ",kabla sijamalizia kutamka maneno ya wimbo, wimbo ambao nilikuwa naimba kwa sauti ya chini sana, kwani nilikuwa tayali nimechoka kuuimba kwa muda mrefu bila mafanikio, nilishangaa kumuona Nyoka yule akimmeza Juliet bila kutambua kuwa alitokea wapi. Baada ya kummeza Juliet, joka lile lilipotea katika mazingira ambayo sikuyaelewa lakini sikujali sana zaidi ya kumshukuru mungu kwani sadaka yangu iliweza kupokelewa na Nyoka wa ajabu, nyoka ambaye nilimshuhudia Bagamoyo kwa mala ya kwanza baada ya kupelekwa na mzee Jabir.

"Una bahati sana!, sadaka yako imekubalika kwa kiwango cha juu, kwani umekuwa mtu wa kwanza katika chama chetu kumtoa sadaka msichana wa kike ambaye bado ni kijana, na hivyo basi kichwa kimoja cha Nyoka wetu kitapungua, na hivyo basi utaishi na Nyoka nyumbani kwako akikulinda …!,akikulinda …akikulinda!, "yalikuwa ni maelezo marefu ya mtu nisiyemfahamu, aliyekuwa akinifahamisha juu ya kupewa nyoka mmoja kama zawadi kwa ajili ya kunilinda. Nyoka huyo atatoka katika mwili wa joka lile kubwa tuliloliabudu, na kulitolea sadaka kwani lilikua na vichwa vingi sana.

Nilitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na sauti ile ya ajabu, huku nikijifungua kitambaa chekundu kichwani na kisha kutoka nje ya chumba cha siri, chumba ambacho nilikitumia kufanyia ibada kwa mungu wetu Nyoka  tuliyemwabudu,mungu ambaye hakupenda kuona wanadamu wakimtukuza na kumwabudu Mungu wa kweli,bila kujali dini zao walizotoka.

Baada ya wiki moja;
        Baada ya takribani siku tano kupita,huku nikiwa tayali nimeshaanza kumsahau Juliet,msichana pekee na wa kwanza kanisani kwangu  kumuua.Nilishangaa sana usiku wa jumamosi,usiku ambao haukuwa wa raha
 katika siku zote ambazo nilikuwa nimeishi duniani.

"Samahani mchungaji,jana usiku Juliet alituaga anakuja kanisani kwenye maombi,alifika mahali hapa?,hajarudi nyumbani mpaka sasa!",yalikuwa ni maneno ambayo yalijirudia rudia kichwani kwangu tangu asubuhi mpaka usiku wa siku ya jumamosi nikiwa nimeketi sebuleni kwangu.Haya maneno waliweza kunitamkia wazazi wake Juliet,siku ya jumatatu walipokuja kumtafuta mtoto wao kwani Juliet nilimuua na kumtoa sadaka jumapili usiku,alipokuja nyumbani kwangu.

"Itabidi kesho nitangaze kanisani,kuhusu Juliet kupotea",nilizungumza maneno haya huku roho yangu ikinisuta,kwani wazazi wake Juliet niliwaogopea na kukataa kuwa Juliet hakuweza kufika nyumbani kwangu.Lakini walipojaribu kumtafuta kila kona ya jiji la Dar es salaam,hawakuweza kumpata huku taarifa juu ya kupotea kwake ikitangazwa na vituo vingi vya televisheni kwani niliweza kulipia pesa kwa ajili ya matangazo hayo,sikuwa na jinsi ilibidi nifanye hivyo na kutoa ushirikiano wa hali ya juu nisiweze kugundulika kama mimi ndiye niliyeweza kumuua.

"Mimi sijafa,bado ninaishi,bado ninaishi!bado ninaishi!",ilikuwa ni sauti ya mwangwi iliyokua ikijirudia rudia masikioni kwangu,lakini nilipotaka kuikimbia sauti ile nilishangaa kukutana na Juliet uso kwa uso,huku alama ya kisu ikiwa shingoni,sehemu ambayo niliweza kumchinja kwa kutumia kisu.

Nilitetemeka sana kwa hofu,,huku mkojo ukinitoka.Ilibidi nisimame tu kama zezeta kwani sikuwa na chochote cha kufanya,na kubaki nikimshangaa tu Juliet.

"Sitaki kukuua wewe kama ulivyoniua mimi,wewe nitakuaibisha ulimwenguni wajue siri zako,lakini nitafanya hayo yote mpaka nitakapokamilisha kazi ya kupambana na wakubwa zako waliokutuma",ilikua ni sauti ya Juliet,msichana aliyegeuka mzimu na kunitokea huku akiwa amevalia kanzu nyeupe iliyofunika mpaka miguu yake.

Kigoma;
         Wazazi wangu wanaiacha ardhi ya  kigoma,na kulishuhudia ziwa Tanganyika kwa chini likiwa linaonekana vizuri sana.Walikuwa katika moja ya ndege aina ya Bombadier inayomilikiwa na Air Tanzania,baada ya kuwatumia pesa waje kunitembelea Dar es salaam.Kwani nilipowatumia pesa ya kupanda treni aina ya deluxe waliweza kunigomea,basi pia walikataa,eti wataniaibisha wakipanda usafiri wa aina hiyo.Kusema ukweli walikuwa sahihi,kwani waandishi wa habari wasingeniacha salama,kutokana na umaarufu wangu kama mchungaji aliyeibuka ghafla na kuwa na pesa nyingi huku akijaza maelfu ya watu katika kanisa lake.Hivyo siku zote walifuatilia maisha yangu ili waweze kuuza magazeti yao,kwani taarifa zilizonihusu ziliwavutia watu wengi sana.

Lakini mimi nilikuwa na maana yangu,kuwataka wazazi wangu waweze kupanda treni au basi,japo walinigomea kutumia usafiri huo.

Bagamoyo;
        Mganga wa kienyeji aliyekuwa na nguvu nyingi sana za kishirikina,akiwa ameketi juu ya joka lile la ajabu ambalo tuliliabudu ,mimi pamoja na wanachama wenzangu akiwemo mzee Jabir na kumpinga Mungu wa kweli,alijikuta akishangaa sana kwani alisikia kelele za vitisho ,bila kutambua sauti ile ilikuwa ikitokea sehemu gani,na nani aliyekuwa akitoa vitisho hivyo.

**ITAENDELEA**

Powered by Blogger.