HADITHI
Maana baada ya waarabu kumuua waliweza kumzika kwa jina hilo kwakua jina halisi hawakua wanalifahamu.
Alikurupuka alifajiri. Aliangalia saa yake ilimsomea kua ni saa kumi na moja na robo. Aliamka na kutoka nje.
Aliweza kuliona gari ambalo walifika nalo hotelini hapo akiwa na Rosemary kabla ya kupotea na kuondoka.
Aliufungua malango na kukuta upo wazi. Funguo ilikua pale pale kwenye eneo lake.
Alitekenya na gali hilo lkikawaka na kumpautyari wa safari.
Hakika kila alichokiota kilikua sahihi. Maana hakhitaji hata kuuliza Zaidi ya kufuata ramani ya ndoto ambayo ilimjia mara moja na kumfganda ubongoni.
Kulikua na umbali kiasi ambacho kilimfanya atumie dakika ishirini na tano kwa mwendo wa gari. Tena alitembea sipidi mia ishirini mapaka mia moja kwenye mabango ya mwendo mdogo.
Makaburi hayo yalikua nje kidogo ya mji na hivyo kulitawaliwa na mapori kabla hajauona ukuta mkubwa ambao ndani yake ndio kuna makaburi.
Alipaki agari pembeni na kuruka ukuta tayari kwa ajili ya kwenda kulitafuta Kaburi lililoandikwa Abdul Kareem ambalo ndani yake ndio kuna mwili wake.
Aliweza kulifikia kaburi hilo. Lakini cha ajabu kilichomshangaza kuliko kitu chochote, alikuta kaburi tayari limeshafukuliwa na maiti hapo ndani.
Alishika kichwa kwa mshangao. Kabla hajafanya chochote alivisikia ving`ora vya magari ya askari ambao walishafika eneo hilo.
“Tafuteni kila mahali… huyu muhalifu bado yupo… si mnaona hata gari yake bado haijaondoka.”
Zilisikika kelele za askari zilizomfanya aamue kutafuta mti mkubwa na kujificha. Mana hakuku na njia ya kutokea na eneo hilo lilikua wazi sana na miti mikubwa ilikua michache sana.
Asakrali walikua wengi sana. Na haikuchuua muda mrefu walimnasa na kuanza kumsulubu kwa mabuti yao yaumizayo.
“utatueleza kwanini unakuja kufukua makaburi.. na hii maiti umeipeleka wapi.”
Aliongea mkuu wa msafara baada ya kumuona Deo akiwa hoi kabisa baada ya kipigo kitakatifu.
Walimkokota na kumuweka kwenye moja ya gari zao walizofika nazo pale
Walimfikisha kituoni kwa ajili ya mahojiano Zaidi.
“kweli jamani, mimi sijui kitu chochote.” Deo alijitetea huku machozi yakimtoka baada ya mateso makubwa aliyoyapata.
“tumekukamata makaburini. Na kule ulienda kufanya nini?” Kachero huyo wa polisi aliuliza kwa sauti ya ukali.
“Mimi nilienda kufagilia kaburi la ndugu yangu. Ndio kufika pale nakuta kaburi limefukuliwa.” Deo alijitahidi kujitetea.
“anhaa… kumbe unafahamiana na yule fedhuli aliyetaka kupora pete ya kifalme… sasa ndio utatueleza kinaga ubaga huyo ndugu yako alitumwa na kina nani katika jaribio la kuharibu sherehe yenye heshima kwenye taifa letu.”
Baada ya kujitetea, akajikuta amejiingiza kwenye matatizo Zaidi. Maana aliwaona watu hao wakizivaa sura nyingine kbisa Zaidi ya hizo walizokuwa nazo.
“mrudisheni… nitakuja baadae kumuhoji kwenye chumba cha mateso. Atasema tu.”
Aliongea kachero huyo na Deo akapelekwa kwenye chumba maalumu kilichopo ndani ya kituo hicho kikubwa cha polisi.
“Rosemary.. Njoo uniokoe.”
Deo aliita mpaka akawa Analia. Lakini hakuweza kumuona Rosemary wala kuisikia harufu yake.
Usiku mkubwa alikuja kutolewa kwenye chumba hicho na kuvuliwa nguo zake zote.
“mpelekeni akaoge… hajaoga toka alfajiri huyu.”
Sauti iliamrisha na asakari watiifu walimpeleka Deo kwenye chumba kingine kilichokua na zana nyingi zitishazo.
Hakika kilionyesha wazi kua halikua bafu, bali ni chumba cha mateso.
“utatueleza hao waasi walikua wakitaka pete ya kifalme wanapatikanaa wapi.” Kachero wa polisi aliongea kwa hasira na kuzidi kumuogopesha Deo.
“mnanionea tu jamani… mimi sijui kitu chochote.” Deo alilalamika.
Lilikuja bomba kubwa kama la kuzimia moto na maji makali yakaanza kutoka kwa kasi ya ajabu.
Kelele za Deo zilidhihirisha kua alikua akipata maumivu makali pasi na kifani.
Hawakujaii kilio chake. Waliendelea kumwagia maji hayo mpaka alipozirai.
Alikuja kushtushwa baada ya kumwagiwa maji.
“huwezi kufa… bali tutakutesa mpaka useme. Hutoenda mahakamani wala hutatoka humu mpaka utueleze kweli… unajua nini kuhusu ndugu yako na watu waliomtuma wanapatikana wapi?”
Ilisikika sauti ya mtu mwengine mwenye miraba minne. Huyo alifunga vitambaa kwenye mkono yake kuashiria kua alifka kwa kazi moja tu. Ya kupiga mpaka aseme.
“jamani, mimi sijui…”
Kabala hajaongea chochote, alikutana na ngumi nzito ilimchana pua na kuanza kutokwa na damu. Alijikuta Analia tu kama mtoto na kushindwa kunyanyuka pale alipo dondoka.
“mimi naona tusimalize nguvu zetu . muacheni na njaa kwa muda wa siku mbili. Halafu tukamtetemeshe na umeme. Ataita malaika wake waje wamtajie kama kweli hajui chochote..”
Iisikika sauti ya kachero aliekua anamuadhibu hapo awali na ndipo askari watiifu walipoenda kumnyanyua na kumpeleka kwenye kile chumba na kumtupia huko kwa mara nyingine.
Alijihisi kufeli mtihani wapili kabla hata hajafanya kitu chochote. Kwanza kufukuliwa kwa maiti ni wazi kua hatoweza kurudisha mwili wake tena. Pili amekamatwa na polisi na Rosemary ambaye ndio tegemeo lake pekee amegoma kufika na kumsaidia. Ni wazi huenda toka alipofeli na mawasiliano yao yameishia hapo.
“ni bora hata ungeniacha tu na kumbukumbu zangu. Haina haja ya kuurudisha mwili. Kama ni mpenzi ningepata mwengine, kwani lazima awe Martha. Umeniuza Rosemary.”
Alijikut akilia na lawama zote zikimuendea Rosemary kwa kushindwa kumsaidia kwenye kipindi hiko kigumu kuliko kipindi chote cha maisha yake anacho kikumbuka.
Masaa yalizidi kusogea mpaka jua likachomoza kuashiria kua siku nyingine imeingia.
Njaa nayo ilianza kumsumbua baada ya kukaa masaa ishirini na nane bila kula chochote.
Zaidi aliteswa sana na kumfanya ahisi mwili mzima hauna nguvu.
Kadri masaa yalivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kunyong`onyea na kupoteza nguvu na nuru ya macho.
Hatimaye kiza kikaingia tena na asakari hao walionesha wazi kama hawakua wanaujali uhai wake.
Hata selo aliyowekwailiua yap eke yake na ilitengwa kabisa. Alihisi hiyo ni selo ya magaidi na yeye pia amejumlishwa kwenye kundi hilo.
Aliujutia utetezi wake ambao ulizidi kumuweka matatani kuliko ile kesi ya kufukua makaburi aliyokamatwa nayo mwanzo.
“ndugu… kama malaika hwajaja kukuambia kua hao magaidi aliokua akifanya nao kazi ndugu yako wanapatikana wapi.. basi jaindae kuruka ruka kweye umeme mpaka utakapopoteza maisha.”
Aliisikia sauti tu ambayo ilikua ikitokea nje. Japo hakumuona kwa sura aliyeongea hayo, ila aliweza kuikumbuka ni sauti ya yule kachero aliyeongoza msafara wakati wanamkamata makaburini.
“Ahsante Rosemary kwa kunifanya nife kwa mateso… nakushukuru sana.”
Aliogea hayo Deo na kujilaza kusubiri kukuche ili akarushwe na umeme mpaka atakapopoteza maisha yake.
ITAENDELEA………
Bado mitihani Sita na mtihani wa pili tu unaonyesha wazi kua Deo anakaribia kupotea iwapo atakosa msaada kwa siku nyingine. Rosemary ni kiumbe kilichokuja kumuokoa au katumwa kummaliza Deo?