Simulizi; "THE BLACK KILLER " (muuaji mweusi)

Simulizi; "THE BLACK KILLER "         (Muuaji mweusi)

Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU YA 11**

Paul baada ya kufanikiwa kutoroka, akiwa ndani ya ndege anamuua rubani kwa kumpiga na bastora kichwani bila huruma na kuusambaratisha ubongo wake. "Nenda kaliwe na samaki nyau wewe",Paul aliitusi maiti ya rubani yule na kisha kuitupa ndani ya maji katika bahari ya Hindi. Kwa mbali sana Paul alikiona kisiwa kidogo kabla ya kufika Zanzibar, na kuamua kuishusha ndege ili aweze kuificha eneo lile. "Bila shaka naweza kuificha helikopta hii katika kisiwa hiki, nirudi Dar es salaam haraka sana nikamuue Benedict, mtu pekee ambaye anafahamu siri zangu nyingi sana baada ya hapo nitarudi kuichukua ndege hii na kutokomea ".Paul aliongea huku akiishusha ndege katikati ya msitu katika kisiwa kidogo kilichopo bahari ya Hindi, na kisha kuifunika na magome ya maiti ili isiweze kuonekana.


Paul akiwa katika kisiwa ambacho hakikuwa mbali sana na Dar es salaam, alisubili jua lizame ili iwe rahisi yeye kuingia jijini bila kufahamika. "Waaooh ……kweli nina bahati spidi boti hii ni ya nani?",Paul aliongea huku akiishangaa spidi boti iliyokuwa imechakaa sana,kutokana na kutotumika kwa muda mrefu, ikiwa imetelekezwa katika kisiwa kile kidogo. Paul alitumia ujuzi wake kuirekebisha mpaka ikawaka, na kisha kuondoka nayo kuelekea Dar es salaam. "Hapa dakika ishirini tu, nitakua mjini nimeshafika tayali ",Paul aliongea huku akiongeza spidi ya boti ile, ili kukamilisha lengo lake kabla hapajakucha na kisha kurudi katika kisiwa kile.



Paul baada ya kufika Dar es salaam, akiwa amevalia koti kubwa lililofunika mwili wake wote, pamoja na kofia iliyouziba uso wake usionekane anashtushwa na taarifa mbaya zilizoenea mjini juu ya afya ya Jacline, msichana aliyetokea kumpenda sana. Huruma pamoja na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Jacline, yanamsukuma kwenda hospitalini kujitolea damu ili kuokoa maisha yake, kama damu yake itakuwa grupu moja na damu ya Jacline.


"Hongera babu, baada ya kukupima tumegundua damu yako inafaa sana kwa ajili ya kuokoa maisha ya mgonjwa ",daktari aliongea huku akidhania Paul alikuwa ni mzee, kutokana na sura yake kukunjamana huku baadhi ya mnvi zikionekana sehemu ya nyuma ya kichwa kwani Paul alivaa kofia na kuivuta kwa mbele ili kufunika uso wake asiweze kutambulika. "Asante kwa kuokoa maisha ya mgonjwa, lakini jina lako ni nani ",daktari aliongea huku akifunga madirisha na kushusha pazia baada ya Paul kumaliza kujitolea damu, kwani giza lilikuwa tayali limeshakua nene na ilikuwa yapata saa tano usiku. "Sitoweza kutaja jina langu, na wala kukuonesha sura yangu ……lakini msichana huyu akiamka muoneshe kipande hiki kidogo cha ua ", Paul aliongea huku akimkabidhi dokta ua na kisha kutokomea..


…………………………………


Baada ya dokta kugoma kuwambia Godfrey na Jonson kuhusu mtu aliyemuongezea damu Jacline, na kisha kuokoa maisha yake …bila kutegemea Jacline anapata fahamu na kuanza kujishangaa kwani hakutambua kafikaje hospitalini. "Nimefikaje hapa hospitalini, vipi muuaji kakamatwa ",Jacline aliongea huku akishangaa mazingira yale ya hospitali, na kisha kuwauliza kina Jonson kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa baada ya kuwaona. ",Usijali kuwa na amani, utafahamu kila kitu ",daktari aliongea na kisha kumsimulia Jacline kila kitu baada ya kuwaomba wakina Jonson kutoka nje kwa muda, lakini Jacline alianza kulia kwa uchungu huku akiushika ujauzito wake baada ya kugundua kuwa mwanaume katili na muuaji, aliyempenda sana bila kumtambua kaweza kuokoa maisha yake baada ya kuoneshwa na daktari ua, ua ambalo lilichumwa eneo ambalo Jacline na Paul Agustino walipokutana kwa mara ya kwanza nje ya hoteli ya Kasabranka nchini Marekani.


Walinzi wakiwa wamelizunguka jengo zuri la kifahari eneo la Masaki wakiwa na siraha zao, wanajikuta katika usingizi mzito baada ya Paul kuwapulizia dawa ya usingizi kimya kimya.Baada ya kuhakikisha hakuna mlinzi hata mmoja alikuwa macho kwa wakati ule, aliingia chumbani kwa mfanyabiashara Benedict na kumkuta akifanya ufuska na kijana mmoja mwenye tabia za kike (shoga),kwa hasira Paul alimuua kijana yule kwa kumpiga risasi nyingi sana. "Pyuuu, pyuuu, pyuuu, pyuuu……",milio ya risasi ilisikika na kumtoboa toboa punga yule sehemu mbalimbali za mwili. "Shenzi kabisa wewe, hiyo adhabu ndiyo inayowafaa wanaume wote wenye tabia kama wewe. " Paul alimlaani mwanaume yule baada ya kumuua, na kisha kumnyoshea bastora kichwani mfanyabiashara maarufu na mtu mzima sana ambaye huwezi kutegemea kama anaweza kufanya upuuzi ule wa mapenzi ya jinsia moja.


"Sasa hii ni zamu yako, wewe ulimuua mr Sarehe ili kujilinda, na mimi nakuua wewe ili nijilinde nisikamatwe " ,Paul aliongea kwa sauti isiyokuwa na utani kwa yale aliyokuwa akiongea, bila kupoteza muda alimpiga risasi kichwani mr Benedict na kisha kutoweka eneo lile kabla ya Polisi kufika kutokana na milio ya risasi kusikika mtaani.

Jacline akiwa hospitalini anajikuta akijifungua mtoto wa kiume, kwani miezi tisa ilikuwa tayali imetimia. ",Nimejifungua salama, lakini naamini mtoto wangu atatengwa kama akigundulika ni mtoto wa jambazi Paul " ,askari wa kike Jackine aliongea moyoni mwake, huku akimtazama mtoto wake aliyekuwa ametokea kufanana sana na sura halisi ya Paul Agustino kabla hajafanyiwa upasuaji.
Bila kutegemea Paul anajikuta mikononi mwa Polisi, kwani mr Benedict alituma ujumbe haraka sana Polisi kwa siri kuhusu kutaka kuuawa na Paul Agustino, hivyo Polisi waliweza kuweka kamera za ulinzi na kuziunganisha makao makuu ya jeshi la Polisi  Hivyo baada ya Paul kuvamia nyumba ya Benedict, askari waliweza kumwona kupitia kamera zile zilizokuwa zimefungwa katika nyumba ya Benedict. "Utatukoma mpuuzi wewe, tumekutafuta sana, "Godfrey aliongea huku akimpiga teke zito Paul, teke lililomfanya kugaagaa kwani mikono yake ilikua imefungwa pingu hivyo hakuweza kujitetea. "Yaaala………aa",Kelele za maumivu zilisikika kutoka kwa Paul, baada ya kukatwa kidole kimoja cha mguuni na Jonson bila huruma ,kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kumpania kwa muda mrefu.
**ITAENDELEA*
Powered by Blogger.