Simulizi; "THE BLACK KILLER " (Muuaji mweusi)







Mwandishi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU 05**


Jacline alirudisha kitambulisho kile haraka sana baada ya kusikia mlango wa bafuni ukifunguliwa, huku Paul akitoka na kuhisi hali isiyo ya kawaida kwani Jacline alionekana kutojiamini kama awali huku wasiwasi na woga ukiionekana wazi katika sura yake. "Vipi mpenzi, kuna tatizo lolote "Paul alimuulza Jacline huku akijifuta vizuri mwili wake kwa taulo na kukausha maji yaliyokuwa yakitililika mwilini. "Hapana mpenzi niko sawa,ondoa hofu kabisa "Jacline aliongea kwa sauti nzuri iliyomfanya Paul kupotezea swala lile.


…………………………………


"Kuna jambo nataka niwafahamishe, kuna kijana nimekutana naye ……inaonekana anafahamiana na Paul Agustino, kijana huyu nilikagua suruali yake alipokuwa ameenda kuoga na bila kutarajia nilikuta kitambulisho cha jeshi cha Paul. " Jacline aliwafamisha wenzake baada ya kutoka chumbani kwa Paul na kugundua jambo ambalo alishindwa kulihifadhi moyoni, kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa Paul kwani hisia za mapenzi zilimsumbua na kumtaka asitoe siri ile kwani angemuweka mahali pabaya Paul ambaye yeye alimfahamu kama mr Pius. "Kijana huyo anaitwa nani?……na umefahamiana naye kivipi " Jonson alimuulza swali Jacline, huku Godfrey akiwa makini kusikiliza mazungumzo hayo.



"Kijana huyo anaitwa mr Pius, nilikutana naye nje ya hoteli jana baada ya kusikia akiongea Kiswahili, kutokana na kuniambia anatokea Tanzania nilijikuta nikiwa rafiki yake " Jacline alimjibu Jonson huku akionekana kuchoshwa na maswali mengi aliyokuwa akiulizwa. "Mi nakuomba endelea kuwa karibu naye na uzidi kumchunguza zaidi, lazma atakuwa anafahamu kitu "Godfrey askari aliyekuwa na busara sana katika kila maamuzi aliyoyachukua, alimsihi Jacline aendelee kuwa karibu na Paul, bila kutambua madhara makubwa yatakayotokea mbeleni.


"Mimi pia, naona hilo ndo jambo sahihi nalotakiwa kulifanya ……"Jacline aliongea huku akitabasamu kwa furaha baada ya kuruhusiwa kuwa karibu na Paul, hali iliyowashangaza Jonson na Godfrey kwani hawakufahamu chochote kuhusu furaha hiyo.


…………………………………

Paul Agustino akiwa chumbani kwake anajiandaa na kutafakari namna ya kumuua  Benny Hanson, daktari aliyemfanyia upasuaji na kuibadilisha sura yake. "Nikifanikiwa kumuua Benny, angalau nitaishi kwa amani kwani ndio mtu pekee anayefahamu siri hii ya mimi kubadili sura yangu "Paul aliongea huku akiisafisha bastora yake na kuiondolea mfumo wa sauti na kuwa na uwezo wa kuua bila kutoa mlio (silent). "Hello doctor, aim very sick …just come to help me "(haloo daktari, naumwa sana njoo unisaidie) Paul Agustino alimpigia simu Benny Hanson kwa sauti ya unyonge sana na kujifanya anaumwa ili aweze kufika haraka na kumuua.


Muda si mrefu dokta Benny aliwasili kwani aliyaamini maneno aliyozungumza na Paul kwenye simu, kwani haikuwa kawaida ya Paul kuongea naye kwa sauti ya kinyonge kiasi kile. "Ndiii…ndiiiii ……ndiii…ndiii" mlio wa kengele ulisikika na kumfanya Paul kuikoki bastora yake, kwani kengele hiyo iliashilia dokta Benny alikuwa tayali  amewasili. "Aaaaah.... …ah…aah" dokta Benny alilalamika baada ya kupigwa risasi ya ubavuni huku akichomwa na kisu tumboni ……shambulio lililofanywa kwa sekunde kadhaa baada ya kufunguliwa mlango wa chumba cha Paul. "Ndii …ndiii "kengele ilitoa mlio kwa mara nyingine kuashilia ujio wa mgeni katika chumba cha Paul, hali iliyomtia hofu Paul na kumfanya kuchukua maamuzi ya kikomando kwani alikuwa tayali ameshaandaa begi lake dogo lenye kila kitu alilolitumia katika safari.


Jacline aliendelea kugonga mlango huku akihofia Paul ambaye yeye alimtambua kwa jina la mr Pius, atakuwa amepatwa na matatizo kutokana na kelele za maumivu alizokuwa akizisikia chumbani.


Paul Agustino anashuka ghorofani kwa kutumia kamba ndefu aliyoifunga dirishani, akiwa katika mavazi yake ya suti nyeusi anafanikiwa kutokomea katika hoteli ya Kasabranka kishujaa baada ya kumpiga teke raia wa kizungu aliyekuwa amepaki pikipiki yake nje ya hotel akisubili wateja, na kisha kutokomea nayo huku akimuacha mzungu yule akilia kwa maumivu makali aliyoyasikia baada ya kupigwa teke.


Godfrey na Jonson wanafika haraka sana chumba namba mia moja baada ya kutumiwa ujumbe wa hatari na Jacline ,ujumbe huo ulitumwa kwa kutumia saa za kijeshi walizokuwa wamezivalia mikononi kila mmoja wao. "Hatuna budi kuvunja mlango ……"Godfrey aliongea na kisha kupiga teke la nguvu mlango ule na kisha kufunguka ,katika hali ambayo hawakutarijia walishangaa kumwona mzungu raia wa Marekani akiwa amepigwa risasi na kisha kuchomwa kisu huku mtuhumiwa akiwa ametoweka kupitia dirishani kwani kamba aliyoitumia ilikua ikining'inia. "Huyu aliyehusika inaonekana aliwahi kuwa askari "Jacline aliongea huku akishangaa sana kile kilichokuwa kimetokea.

"Take this file, you will know the one who killed me ……"(shika faili hili, utamfahamu aliyeniua) Mzungu yule alimkabidhi faili Godfrey na kisha kupoteza maisha.


Wote kwa pamoja walilipitia faili lile,huku kila mmoja akishangazwa sana na taarifa zilikuwa latika faili lile,kwani waliishi na Paul bila kumtambua kutokana na sura yake kubadilishwa na dokta Benny ambaye tayali alikuwa marehemu."Mpuuzi kweli huyu,alinidanganya anaitwa Pius kumbe ni muuaji mkubwa" ,Jacline alilia kwa uchungu huku akijuta kumpatia penzi Paul kabla ya kumfahamu vizuri.


Vyombo vya habari duniani kote vilipambwa na taarifa ya jambazi Paul ,huku picha zikioneshwa katika televisheni na magazeti na donge nono likitolewa kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake."Popote alipo tutamkamata,akiwa hai au amekufa" vijana watatu waliongea na waandishi wa habari huku wakiwa na hasira sana dhidi ya Paul Agustino.


*ITAENDELEA*

Powered by Blogger.