HISTORIA YA ASANGUW












Kilemaganga, Binti Wa Mfalme Wa Wahehe Aliyepofuka Macho Kwenye Himaya Ya Wasangu..
Ndugu zangu,
Tunaipitia hapa historia yetu, kwa vichwa vyetu na kalamu zetu. Ni kwa utafiti wetu wenyewe na kusaidiwa na maandiko ya watafiti wengine.
Nilianza jana, kuna mlionyesha kuvutiwa. Nasimulia leo kisa cha binti wa kwanza wa Chifu Munyigumba wa Wahehe.
Binti huyu aliozwa kwa Chifu wa Wasangu, Merere Musukulu.
Kwanini aliozwa huko?
Chifu Munyigumba alijiona yuko kwenye hatari ya kushambuliwa na machifu watatu nje ya mipaka ya himaya yake; ni machifu wa Ubena, Usagara na Merere wa Wasangu.
Tishio kubwa zaidi lilitoka kwa Wasangu kwa vile Munyigumba alitambua uwezo wao wa kivita.
Mara ile Munyigumba wa Wahehe alipoambiwa kuwa Merere wa Wasangu katuma mshenga na posa ya kumuoa binti yake, basi, Chifu Munyigumba alikubali kwa haraka sana.
Aliiona busara ya kumwoza bintiye kwa adui yake. Kwamba angekuwa amempunguza adui mmoja.
Kwa mila za Wahehe, Wasangu na Wabena, anayeoa binti yako anakuwa mwanao.
Binti wa Mfalme, Kilemaganga Musakifwa Semuyinga anaelezwa alikuwa mrembo sana. Habari za urembo wake zikamfikia hata Chifu Merere wa Wasangu. Ndio sababu ya kumtuma mshenga kwenda kuchumbia na hatimaye kumwoa.
Ajabu ya jambo lile, hata baada ya Binti wa Mfalme, Kilemaganga kuingia kwenye Ikulu ya Merere ya Utengule Usangu, ikafika mahali Merere akasahau kuwa Munyigumba ni mkwe wake.
Akaandaa vikosi kwenda kuvamia himaya ya Munyigumba. Taarifa za askari wa Merere kusogelea himaya ya Munyigumba zilimfikia Munyigumba mwenyewe, naye akazipuuzia akisema;
" Huyo ni mwanangu tu". Kwa Kihehe, ( Iyo nguo mukunungwa)
Munyigumba alipobaini baadaye kuwa mkwewe anakuja kweli kumvamia, ndipo alipotengeneza kwa haraka silaha za sumu kuzuia uvamizi huo.
Tunaona hapa, hata wakati huo, kulikuwa na maarifa ya kutengeneza silaha za sumu.
Munyigumba alitengeneza silaha gani za sumu kukabiliana na Wasangu?
Itaendelea..
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Powered by Blogger.