HISTORIA YA WAGOGO: VITA VYA KWANZA VYA DUNIA KATIKA ARDHI YA UGOGO. SEHEMU YA KWANZA.



Image may contain: tree, car, sky, house and outdoor
HISTORIA YA WAGOGO: VITA VYA KWANZA VYA DUNIA KATIKA ARDHI YA UGOGO.
SEHEMU YA KWANZA.
Mara baada ya ujenzi wa maboma mawaili katika ardhi ya Ugogo, yaaani Boma la Mpwapwa na lile lilikuwa Kilimatinde. Kulijengwa boma lingine kubwa Dodoma, sehemu ya katkatii ya ardhi ya Ugogo.
Boma hilo lilifunguliwa mnamo mwaka 1912. Na mpaka kufikia mwaka 1914, mwaka ambao vita vya kwanza vya dunia vilianza, kulikuwa na vita kubwa kati ya Mwingereza na Mjerumani. Wakati huo vita vikianza, Maakida walishaanza kufanya kazi kwenye lile boma jipya pale Dodoma. Maakida waliopata kufanya kazi kwenye lile boma jipya pale Dodoma walikuwa kama ifuatavyo, Akida bakari Mwinyikambi, Hatibu ahmed na bakari Sadiki.
Maakida hawa walifanya kazi chini ya usimamizi wa Wajerumani. Kabla ya vita kufika meneo ya Boma lililopo pale Dodoma, vita vilikuwa maeneo ya Kondoa- Irangi. Na inasemekana wakati Waingereza wanafika maeneo ya Kondoa-Irangi, baadhi ya watemi wa Ugogo waliamua kumuunga mkono Mwingereza kwani walikuwa wakimchukia sana Mjerumani. Wakati Wajerumani walipokwenda vijiji kwa lengo la kukutana na watemi wa Ugogo.
Baadhi ya watemi hawakuwepo, mmoja wapo ni Mtemi Mazengo Chalula aliyekuwa Mtemi wa ardhi ya Mvumi. Wajerumani waliuliza kuwa Mtemi yupo wapi? Na ndipo wanakijiji walipojibu kuwa, Mtemi ameliwa na simba. Wajerumani kusikia vile walihitaji kujua mifupa yake iko wapi? Na wanakijiji hao walishindwa kuonyesha mifupa yake.
Na hapo kukawa na kizaazaa kwenye ardhi ya Mvumi. Wakati vita vinakaribia maeneo ya boma lililopo pale Dodoma, maakida wengi waliogopa sana. Na mara baada ya Waingereza kuchukua boma hilo, Maakida waliamua kumuunga mkono Mwingereza. Wakati Mjerumani anakimbia vita kwenye ardhi ya Ugogo, alikamata makabila mengi sana ya ardhi ya Ugogo.
Wapo Wagogo waliokimbia sehemu za Mahenge, Iringa na maeneo mengine yaliyokuwa yakipakana na Dodoma. Kwa yale makabila yaliokamatwa na Mjerumani, yalipata shida sana njiani, kwani walikuwa wakiteswa sana na wanajeshi wa kijerumani waliouwa wakatili sana. Wagogo wengi walikufa kutokana na njaa na mateso kutoka kwa wanajeshi wakatili wa Kijerumani.
Powered by Blogger.