Simulizi ; "THE BLACK KILLER" (muuaji mweusi)

Simulizi; "THE BLACK KILLER "          (muuaji mweusi)





Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
**SEHEMU YA 12*

Habari za kukamatwa kwa Paul zinakua gumzo nchini Tanzania ,huku watu wengi wakitamani kuiona sura yake uso kwa uso bila kuambiwa na mtu yeyote. Vyombo vya habari hasa magazeti yalipambwa na habari iliyohusu kukamatwa kwa Paul, na kuwavutia wasomaji wengi. "Huyu jambazi anyongwe tu, kaua watu wengi sana,"mmoja wa wananchi alisikika akiongea huku akitazama magazeti yaliyokuwa yakitembezwa na kuuzwa na machinga. "Mwenye pesa sio mwenzako, utashangaa kusikia jamaa katoroka au kaachiwa huru ",raia mwingine alisikika akimjibu mwenzake, na kisha kuondoka eneo lile.


Jacline anamtazama Paul kwa huruma akiwa mahabusu, akisubili siku yake ya hukumu huku damu nyingi na madonda yakiutapakaa mwili wake."Pole sana Paul, nimejifungua mtoto wa kiume ……mtoto ambaye ni damu yako lakini mwanangu hatabahatika kuiona sura ya baba yake kutokana na wewe kunyongwa kwa dhambi ulizozifanya",Jacline aliongea huku akiwa ameshikilia vyuma vya gereza la Segerea, akiitazama sura ya Paul iliyoonekana kutafakali mambo mengi sana kwa wakati ule.


"Kama nikifa naomba umtunze sana mwanangu, na hakikisha hawi mtu mbaya kama baba yake na wala usije kumwambia lolote kuhusu baba yake ",Paul alizungumza maneno yalimchoma sana Jacline, na kuifanya sura yake kulowa machozi kwa huzuni. Lakini kutokana na mapenzi makubwa Jacline aliyekuwa nayo, anajikuta akiweka uaskari pembeni na kusahau maovu yote Paul aliyoyafanya na kumsaidia kutoroka mahabusu.


"Naskia kuna mfuniko wa chemba ya taka humo ndani ,unaopeleka maji taka baharini ,tumia njia hiyo kuondoka mahali hapa na kisha ondoka Dar es salaam haraka sana ",Jacline alimpatia siri Paul iliyomuwezesha kutoroka eneo lile.


Hali ya ukimya ikiwa imetawala eneo lote la gereza la Segerea, huku wafungwa wengi pamoja na askari waliokuwa lindo, wakiwa wanakoloma kutokana na uchovu. Paul anafanikiwa kufungua mfuniko alioelekezwa na Jacline, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu. Bila kupoteza muda aliingia ndani ya shimo lile na kisha kusombwa na maji taka yaliyokuwa yakipita kwa kasi, na kisha kwenda kumtupia baharini.


Taarifa za Paul kutoroka gerezani zinatangazwa,baada ya kuamka na kukuta akiwa hayumo mahabusu asubuhi, huku askari wengi waliokuwa zamu wakiachishwa kazi kwa uzembe mkubwa walioufanya. "Naamini Jacline kahusika na kutoroka kwake, hakuna mtu yeyote aliyeifahamu njia hii zaidi yake na nilimuona akiongea naye jana ",Jonson aliongea huku akionekana kukasirishwa na tukio lile. "Kaamua kuweka mapenzi mbele, mi nilijua tu kuwa hili litatokea " ,Godfrey aliongea huku akitoa amri ya Jacline kukamatwa haraka sana, kujibu tuhuma za kuhusika na utorokaji wa Paul mahabusu.


"Hahahaa, we kichaa unanuka sana hebu toka hapa ",mvuvi mmoja alicheka sana huku akiziba pua yake kutokana na harufu mbaya ya Paul, baada ya kumwona akiwa amechakaa tope la maji taka.Bila kutegemea alijikuta akipigwa mateke mawili mfululizo, na kuugulia maumivu makubwa. "Chunga mdomo wako, sura zingine siyo za kuchezewa ",Paul aliongea na kumpatia onyo kali mvuvi yule, na kisha kuondoka eneo lile.


Wananchi wenye hasira kali wanamtupia Jacline mawe, huku wengine wakitumia viatu vyao kumuadhibu Jacline kutokana na siri nzito aliyoifichua baada ya kupewa mateso makali bila huruma. "Nastahili mateso haya, mwanangu nikifa naomba usiwe mbaya kama baba yako",Jacline aliongea na kulia kwa uchungu, baada ya kukubali kuhusika na kumtorosha Paul, huku akikubali kuzaa naye mtoto hali iliyowafanya wananchi kukasirika na swala lile.
"Mungu wangu, nini hiki tena ",askari mmoja alishangazwa baada ya kumkuta Jacline mahabusu akiwa amepoteza maisha, baada ya kujiua kwa kutumia kisu. "Jacline, rudi rafiki yangu rudi………umechukua maamuzi magumu, rudi twende nchini kwetu sitaki kurudi peke yangu ",Jonson aliongea huku akilia kwa uchungu, baada ya kushuhudia maiti ya Jacline huku damu mbichi zikimtoka tumboni mwake.
*ITAENDELEA **
Powered by Blogger.