Simulizi; "THE BLACK KILLER"       (Muuaji mweusi)


Simulizi; "THE BLACK KILLER"
     (Muuaji mweusi)

Mtunzi; HAKIKA JONATHAN

*SEHEMU 03***

Bwana Paul Agustino akiwa mwenye kujiamini sana baada ya kubadilisha sura yake, anaponda starehe na wadada katika kasino na hoteli ya Kasabranka bila kujali gharama ya pesa aliyokuwa akitumia. "My girls, just drink ……drink ……I will pay "(wasichana wangu ……kunyweni ……kunyweni nitalipa) bwana Paul aliwaondoa hofu wadada zaidi ya sita waliokuwa wamemzunguka wakiponda naye raha na kunywa vinywaji vya kila aina bila kujali gharama zake. "Thank you nigga "(asante nigga …)walimshukuru bwana Paul na kumwita nigga kutokana na weusi aliokuwa nao huku akiwa amevalia suti nyeusi iliyompendeza vilivyo.

…………………………………

Vijana watatu wazalendo wa nchi zao wanaiacha ardhi ya Tanzania, huku kila mmoja akiwa na mawazo mengi akifikiria jinsi ya kuikabili kazi nzito iliyoko mbele yake. "Bila shaka tutafika Marekani kesho saa sita mchana ",mrembo Jacline mmoja wa askari hodari kutoka Afrika Kusini alikisia muda wa Kufika Marekani na kujalibu kuwajulisha wenzake, ili wawe tayali kwa safari ndefu ndani ya ndege.Kutokana na kuishi Tanzania kwa takribani mwezi sasa,Jacline  alikuwa tayali anafahamu kuongea Kiswahili vizuri hali iliyorahisisha mawasiliano baina ya mashujaa watatu waliotumwa na nchi zao kwenda kumtafuta bwana Paul Agustino akiwa hai au amekufa.


…………………………………


Mfanyabiashara wa madawa ya kulevya pamoja na madini ya Tanzanite,bwana Benedict Mathayo anakuwa katika wakati mgumu akifikiria namna ya kujiokoa ili asiweze kukamatwa kwani alishirikiana na waziri wa ulinzi bwana Sarehe Athuman kufanya mipango ya kumuua raisi ili waipindue nchi."Bwana Sarehe hajanitaja,lakini ninahofu huyu mpuuzi akikamatwa lazima na mimi nitiwe hatiani……" mfanyabiashara muuaji na katili aliyekuwa ameahidiwa uwaziri mkuu na bwana Sarehe watakapofanikiwa kuipindua nchi,aliendelea kutafakari bila kupata jibu lolote namna ya kujiokoa kutoka katika kesi nzito iliyokuwa ikiwakabili mara tu atakapo kamatwa bwana Paul Agustino.

"Huyu mpuuzi kabadili hadi namba ya simu,ngoja nitumie barua pepe (email) nibahatishe kama ujumbe utamfikia……anatakiwa ahame Newyork haraka sana kabla hawa washenzi waliotumwa kumkamata hawajafika……" bwana Benedict alilalamika baada ya kupiga namba ya simu ya mkononi ya bwana Paul Agustino mara kadhaa,bila kupatikana na kuamua kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia barua pepe.


…………………………………

"Waaaooh kumbe nchi ya Donald Trump ni nzuri kiasi hiki……" Jacline aliongea huku akitabasamu baada ya kufika nchini Marekani,na kuanza kushangaa uzuri wa jiji la Newyork."Ndio ni pazuri sana,na hapa ni mwanzoni tu mwa jiji" Jonson alimjibu Jacline huku wakijiandaa kwa ajiri ya kushuka ndani ya ndege kubwa inayomilikiwa na shirika la ndege la Dubai Airlines.

"Mbona sioni askari waliokuja kutupokea nimechoka na safari, mimi ni mwenyeji sana wa jiji hili ……na hoteli ya Kasabranka ndo napenda kufikia kila nifikapo Marekani ……kwahyo tunaweza kwenda kupumzika mahali pale kwa siku ya leo kabla ya wenyeji wetu kuja kutuchukua
Powered by Blogger.