HISTORIA YA KABILA LA WAGOGO. MAISHA KABLA YA KABILA LA UGOGO. SEHEMU YA PILI



No automatic alt text available.
HISTORIA YA KABILA LA WAGOGO. MAISHA KABLA YA KABILA LA UGOGO.
SEHEMU YA PILI
Kabila la pili kuwepo katika Ardhi ya Ugogo ni Wamankala ambao walikuwa wakiishi magharibi mwa Dodoma katika maeneo ya nyasi za Surungayi. Historia inasema kuwa kabila hili lilikuwa na tamaduzni zinazofanana na Wang’omvia kwa mfano waliishi kwa uwindaji na uokotaji. Licha ya Lugha yao ya Kimankala kuwa tofauti na ile ya Wang’omvia ila waliweza kuelewana kutokana na mahusiano hayo. Na kwa utafiti wa Mathias Mnyampala wa mwaka 1969, unasema kuwa Wamankala walikuwepo na waliishi katika sehemu za nyasi za Surungayi,Mgunguko, Kinyambwa na Bahi. Kabila la tatu ni Wanyanzi, Wanyanzi walipatikana katika maeneo ya Manyoni. Kama iliovyokuwa kwa Wangomvia na Wamankala, Wanyanzi waliwinda na kuokotaokota. Mpaka tafiti ya Mathias Mnyampala ikifanyika mwaka 1969, Wanyazi waligawanyika katika sehemu mbili. Yaani kuna Wanyanzi waliokuja kuwa kabila la Wagogo ambao walipata kuishi katika ardhi ya ugogo na wengine wakaja kuwa Wakimbu ( Wanyamwezi) waliokuja kuishi katika ardhi ya Unyamwezi.(rejea historia ya Ukoo wa Mtemi Mirambo)
Powered by Blogger.