Simulizi; NABII WA UONGO **SEHEMU YA 14**












Simulizi; NABII WA UONGO
**SEHEMU YA 14**

Ilikua siku ya ijumaa, siku ambayo ilikua ya maombi kanisani kwangu. Tabasamu zuri liliipamba sura yangu, kichwa changu kiliwaza tu kwenda kuishi kuzimu, sehemu ambayo ilionekana kunipendeza sana. Macho yangu yaliangaza huku na kule, na kukagua sura ya kila muumini aliyeingia kanisani kwangu. Neno kafara, kafara nyingi nilipaswa kutoa, ili niweze kupanda cheo, na kisha kwenda kuishi kuzimu. Hivyo basi, lengo la kukagua sura za waumini wangu jioni ile, ilikua ni kutafuta sura nzuri za wasichana warembo, na vijana wa kiume watanashati, niweze kuwalaghai na kisha kuwaua, kitendo ambacho kingeniongezea thamani ndani ya chama changu.

"Pendo, mtoto wa mbunge wa manispaa ya Temeke, atanifaa sana, muone alivyo mrembo ……"

"Jonson naye, nitamuwekea dawa kwenye soda akija nyumbani kwangu kwenye somo la biblia, harafu nitamuua "

"Kwahiyo, ninapaswa kumuua Pendo, Jonson na Stephano ndani ya wiki hii, na mwezi ujao nitaua wengine "

Yalikuwa ni maneno ambayo niliyazungumza moyoni mwangu, huku nikiongoza ibada ya maombi siku ya Ijumaa. Kanisa lilifurika kama kawaida, wananchi mbalimbali kutoka duniani kote, walifika kuombewa, baada ya kupata taarifa zangu za uponyaji kupitia redio na televisheni. Kwa kutumia vifaa vyangu vya ajabu, maji ya ajabu, kitambaa pamoja na pete ambayo nilikuwa nimeivaa mkononi mwangu .Viwete waliweza kutembea, na wenye magonjwa mbalimbali waliweza kupona.

"Let me take this opportunity to thank the son of God, apostle Hakika, for healing me "(Nachukua nafasi hii kumshukuru mwana wa Mungu, nabii Hakika, kwa kuniponya)  yalikuwa ni maneno ya furaha na shukrani, kutoka kwa mwanaume mmoja raia wa Kenya aliyesumbuliwa na ugonjwa wa ukimwi kwa miaka mingi, lakini baada ya kumgusa na pete yangu kichwani, aliweza kuwa mzima wa afya, na ripoti ya daktari iliweza kudhibitisha jambo hilo, baada ya kumfanyia uchunguzi mala baada ya kumuombea, na kisha kuleta majibu yake haraka sana baada ya saa moja.

"Aim from America, I was suffering from Cancer, but i thank the son of God, apostle Hakika for healing me, I got his information from BBC, and decided to come in Tanzania  to get healed "( Ninatokea Marekani ,nilikuwa nasumbuliwa na kansa, lakini namshukuru mwana  wa Mungu, nabii Hakika kwa kuniponya, nilipata taarifa zake kupitia BBC, na nikaamua kuja Tanzania nipate kuponywa)  ilikuwa ni sauti ya mzungu mmoja raia wa Kimarekani, aliyeonekana kuongea lugha fasaha ya kingereza, akiwa na furaha sana baada ya kuponywa. Sauti za shangwe na nderemo ziliweza kusikika, hakuna aliyeamini kama kweli niliweza kuwaponya wangonjwa wale, hasa mgonjwa wa Ukimwi, raia wa Kenya.

Waandishi wa habari walipiga picha na kurekodi kila tukio ambalo lilifanyika kanisani kwangu, huku chaneli ya ITV ikirusha laivu kipindi changu. Hivyo basi, sifa zangu zilienea kila mahali, na kunifanya nizidi kuwa maarufu. Hakuna aliyefahamu kama nilitumia nguvu za giza kuwaponya watu, bali niliendelea kupata wafuasi wengi zaidi kila kukicha. Japokuwa mzimu wa Juliet ulijaribu kunichafua na kusema ubaya wangu kanisani kwangu, lakini haikusaidia chochote kwani mkuu wangu nyoka aliweza kufuta kumbukumbu zao, na kuwafanya wasahau kila kitu ambacho Juliet aliweza kuwaambia, kuhusu unabii wangu wa uongo, na kuhusika na mauaji yake.

…………………………………

Ilikuwa ni jioni njema, jioni ya siku ya ijumaa, wazazi wangu pamoja na wazazi wake Juliet, wakiwa wameshakamilisha siku mbili za kufunga na kuomba ,ili mzimu wa Juliet upate nguvu kwa mala nyingine tena, ili aweze kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani.

Matumaini ya kunikomboa yaliweza kufifia, kwani japo walikuwa wametimiza siku mbili za maombi, lakini hawakuweza kusikia chochote kuhusu mzimu wa Juliet. Tangu uondoke siku ya Jumatatu, mzimu ulikuwa bado haujarudi na kuwapatia matokeo mazuri, kuhusu ukombozi wangu.

"Mwanangu jamani, anazidi kumchukiza Mungu, ona anavyosifiwa kuwaponya watu, Eeeeeh Mungu msamehe kijana wetu, halijui alitendalo " ,yalikuwa ni maneno yenye uchungu wa mwana, maneno mazito kutoka kwa mama yangu mzazi, mama ambaye alinilea kwa uchungu tumboni mwake kwa muda wa miezi tisa. Japo alinilea kwa uchungu, kwenye shida na raha, lakini nilishindwa kumlipa fadhira na kutaka kuwaua, niwatoea kafara yeye na baba yangu mzazi. Lakini kwa msaada wa mzimu wake Juliet, sikuweza kufanikiwa kutimiza malengo yangu. Kwahiyo basi, mama yangu alizungumza maneno hayo mazito ya uchungu, baada ya kutazama kipindi changu katika chaneli ya ITV, alishuhudia jinsi ambavyo niliweza kuwaponya watu kwa kutumia nguvu za pete yangu, na kumfanya aweze kusononeka sana. Alitambua kuwa nilikua na shetani ndani yangu, akinitumikisha na kumsahau Mungu.

"Usjali mama Hakika, kila kitu kitakua sawa, Mungu wetu hashindwi! " ,yalikuwa ni maneno ya hekima kutoka kwa baba yake Juliet, akimtia moyo mama yangu, aliyeonekana kuhuzunika na yale niliyokuwa nikiyafanya. ………

……………………………

Kuzimu; Masaa sita nyuma

       Ilikuwa siku ya ijumaa, mida ya mchana, kivumbi kiliweza kutimka kuzimu. Gereza la kuzimu, gereza ambalo lilitengenezwa kwa vyuma, vyuma ambavyo vilikuwa vya moto sana kiasi kwamba hakuna binadamu yoyote wa kawaida ambaye angeweza kusogelea vyuma vya gereza hili. Vyuma hivi vya gereza viliweza kuyeyuka na kuwa kama uji, macho ya Juliet, macho ya ajabu ndiyo yaliyoweza kuyeyusha vyuma hivi baada ya kutoa mwanga mkali sana. Maombi ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, yaliweza kufanikiwa ,kwani nguvu za Juliet ziliweza kurudi na kuwa za kutisha sana. Uji ule wa moto, uji ambao ulitokana na vyuma kuyeyushwa na macho ya Juliet, uliwaunguza nyoka waliokuwa wakimlinda Juliet kwa kumuimbia nyimbo zenye kumdhoofisha nguvu zake na kumpulizia filimbi.

Kiongozi msaidizi wa Jeshi la shetani, kiongozi ambaye ndiye aliyetupokea siku tuliyoenda kuzimu, na kunieleza mambo ya kufanya kama nitataka kuishi nao kuzimu, kiongozi ambaye alivalia mavazi ya kifalme. Alipiga tarumbeta, tarumbeta ambalo liliashiria hatari ili askari wake waweze kujiandaa kwa mapambano.

"Taaantii …tantaa, tantiii …tantaaa, yeeeeeh!!!!! " ,ilikuwa ni sauti ya tarumbeta kubwa sana ya kijeshi, tarumbeta ya kuzimu ambayo ilitofautiana sana na tarumbeta zetu za duniani. Ilitoa amli ya kuanza mapambano, huku mkuu wa jeshi hili akishangilia sana kuashiria ushindi zidi ya Juliet. Mala tu baada ya kumaliza kupuliza tarumbeta lake  na kuruhusu mapambano. Askari wake walianza kukimbia, kuelekea sehemu ambayo kulikuwa na gereza ambalo Juliet alikuwa amefungwa.

"Iiiiiiiih………wiiiih …………iiiiih ……wiiiiiih ",sauti za vilio zilisikika, sauti zenye kutia huruma, walikuwa ni askari wa kuzimu wakipiga kelele za maumivu, baada ya kupigwa na shoti kali za macho ya Juliet. Kwakweli Juliet alibadirika sana, alikuwa na nguvu za ajabu  nguvu ambazo zilisababishwa na wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, kufunga na kuomba kwa siku mbili bila kukata tamaa.

Askari wengine waliyeyuka baada ya kukanyaga uji ambao ulitokana na vyuma vya gereza la Juliet vilivyoyeyuka  ,walipiga kelele huku wakifa na kuteketea kama nzige.

"Unaitwa nani ,mbona sijawahi kuona kiumbe na mzimu wa ajabu kama wewe ……" ,kiongozi wa Jeshi la kuzimu aliongea na kumuuliza swali Juliet, ni baada ya kujikuta akiwa peke yake huku askari wake wote wakiwa wameteketea.

"Mimi ni Juliet, niliyekufa bila hatia, na kurudi tena duniani kuwateketeza watu waliosababisha nife " ,Juliet aliongea na kisha kumnyoshea vidole kiongozi yule, muda mfupi badae, askari yule aligaa gaa na kupoteza maisha. Kwani moto ulitoka katika vidole vya Juliet na kumuunguza, japo  askari yule alijaribu kuuzuia moto kwa dakika kadhaa bila mafanikio.


…………………………………

Ijumaa; jioni ………
     
     Nyumba ya kina Juliet ilionekana kuwa na simanzi, mama yangu alihuzunika na kujuta kunizaa, kwani nilionekana kama mkosi katika familia, kutokana na kumkufuru Mungu kwa matendo yangu mabaya, na kumtumikia shetani.

"Usilie mama, nimerudi, asanteni kwa kutii maagizo mliyopewa na malaika, kesho haya yote yataisha ",ilikuwa ni sauti ya mzimu wa Juliet, baada ya kutokea sebuleni na kusababisha baba yangu atimue mbio kutokana na uoga. Juliet aliongea huku akimsogelea mama yangu, aliyekuwa akibembelezwa na mama yake kwa muda wote.

"Usikimbie baba Hakika, japo mimi sio binadamu wa kawaida, lakini sio mtu mbaya kama unavyofikilia, nimetumwa duniani kwa makusudi ya kuteketeza watu wote wabaya, na kumgeuza adui kuwa mtu mwema ",Juliet aliongea maneno mazuri, maneno ambayo yalimfanya baba yangu arejee sebuleni. Lakini wakati hayo yote yakitokea, baba yake Juliet alikuwa amepigwa na butwaaa, akimshangaa Juliet kutoka chini mpaka utosini, hakuamini kama kweli mwanae aligeuka kuwa wa ajabu kiasi kile.


*ITAENDELEA **

TUKUTANE SEHEMU YA MWISHO, SEHEMU YA 15
Powered by Blogger.