HISTORIA FUPI YA WABONDEI






HISTORIA FUPI YA WABONDEI
Kabila ya Wabondei ni miongoni mwa makabila kadhaa ya wakazi wa Mkoa wa Tanga, Makabila mengine ni Wazigua, wanguu, wakilindi, wasambaa, waruvu, ambao kihistoria wana asili moja yaani Waseuta kama nitakavyoelezea baadaye, Makabila mengine yaishiyo mkoani Tanga ni wasegeju, wadigo na wadaiso ambao wao sio waseuta na wenyeji kabisa wa inchi ya Tanga kihistoria ni Wambugu na wandorobo.
Waseuta ni kina nani?
Waseuta ni jina la umoja linalowakilisha makabila ya mkoa wa Tanga ambayo asili yao ni moja, makabila hayo ni wazigua, wanguu, wakilindi, wasambaa, waluvu na wabondei, wameitwa hivyo kwa sababu ya kiongozi wao wa zamani (Mkale) aliyeitwa Seuta ambaye alikuwa mtawala aliyewapigania na kuwalinda dhidi ya uvamizi wa wareno kabla hawajatawanyika, kwa sasa makabila hayo hutambika tambiko lao kwa matwala huyo au mtemi au chifu aliyeitwa Seuta.
Jina SEUTA ni muungano wa maneno mawili ya kibondei SE – Baba na UTA- ni Upinde kwa hivyo Seuta ni “Baba wa Upinde” wengine husema “mwana wa Upinde”, alizaliwa na Baba yake aliyeitwa Kuba Kaluli (seuta Kaluli) ambaye pia alikuwa mzimu wa zamani sana, na mama yake alikuwa binti wa kifalme aliyeitwa Musi au wengine walimuita Mchemno ambaye kaka yake alikuwa mfalme aliyeitwa Sekalingo, Seuta alianza kutawala akiwa na Umri wa miaka 12 alikuwa na akili za kupita kawaida mbunifu na pia alikuwa Mganga, moja ya maswala ambayo anakumbukwa sana Seuta ni namna alivyoweza kuwapiga Wareno kwa kutumia Upinde na Mishale na kuwauwa vibaya ingawa wao walikuwa na Bunduki.
Seuta alizaliwa huko Kwediboma katika tarafa ya Mgera wilayani Kilindi zamani Handeni umaarufu wake ulitokana na akili zake za kupita kawaida za ubunifu wa kuwashinda wareno waliokuwa wamekuja kuivamia inchi ya waseuta kwa kusudi la kuchimba madini na ili kupata watu wa kuwachimbia madini waliwaonea wenyeji na kuwakamata kwa nguvu ili wawachimbie madini watu walipogoma waliwaua na kuwachomea moto vijiji vyao jambo hili lilimuudhi sana Seuta na waseuta kwa ujumla kwani ukandamizaji huu wa Wareno haukukubalika.
Wareno walikuwa na ngome kubwa huko Mombasa lakini walikuwa wakisambaa kutafuta mali waseuta walipanga vita ambavyo vilipiganiwa katika eneo la Mto Ruvu, wareno walitumia Bunduki na mizinga na vita hii iliwakalia vibaya waseuta kwani milio tu ilikuwa tishio kubwa kwao na hivyo walirudi kwa kiongozi wao kutafuta ushauri, Seuta aliwashauri kuwa wanainchi waviache vijiji vyao na kila kijiji wanachokiacha sehemu ambazo Wareno wangepita wavichome moto na kuchafua maji, pia waharibu mashamba na vyakula kisha wajifiche vita hivi vilijulkana kama vita vya kuvunja mawe ya kusagia chakula “Nkondo ya kitula nyala” aliwambia kila wanapoharibu watambike na kuvunja mawe ya kusagia, Wareno walipoona kuwa askari wa Seuta wamekimbia waliendelea kuwafuatilia lakini walikuta maji yamechafuliwa, hakuna chakula na watu wamekimbia hali hiyo iliwashitua na wakakata tamaa kwa kuwafuatilia watu wasiowaona na pia njaa ilikuwa ikiwatesa wakiwa wamechoka na hofu ya njaa na magonjwa na silaha nzito ndipo Seuta alipoamuru kuwanyeshea mvua za mishale na wareno wengi sana na vibaraka wao walikufa na kuanza kukimbia wakirudi Mombasa wakiwa wameshindwa vibaya na hivyo Seuta alipata sifa kubwa sana kama mtu aliyekataa ukandamizaji na mwenye akili aliyekomesha kabisa uonevu na kuwashikisha Adabu na uganga wake uliaminika na watu walihofu kuwavamia waseuta na Tangu kifo chake ndipo waseuta wote walipoanza kutambika wakisema “Mtunga Katungile hale........Waseuta na Ugone.......”
jina Wabondei ni jamii ya watu walihama kutoka milimani na pwani kuhamia bondeni (Bonde)maeneo ya Muheza kwaajili ya kutafuta ardhi yenye rutuba kwaajili ya kilimo,miongoni mwasifa zao wanaakili sana shuleni ni miongoni mwawasomi wakwanza Tanganyika,hawapendi vita(watu wa Amani)hako radhi wakuachie mji,watu wa Dini nk Chifu wao wa mwisho kabla Nyerere hajaustopisha Uchifu alikuwa Chifu.Erasto Mang'enya (Spika wa Pili na wa Kwanza mweusi )wa Bunge la Tanganyika huru baada ya A.Y.Kariemjee (Mhindi)hata Nyerere alishangaa alipofika Pugu Secondary alishangaa kumkuta Mwalimu pekee mweusi ni Mwl.Joseph Muhando-Mbondei vilevile .
Thanks...
Powered by Blogger.