HADITHI-PENZI LA FUKARA🔥 MWANDISHI (MTUNZI)


h
SIMULIZI
🔥PENZI LA FUKARA🔥
MWANDISHI (MTUNZI)
IGS
SEHEMU
21
Instagram>igs_story255
ILIPOISHIA...................
Steven alikuwa akimfuta uku akimwangalia usoni na bila kujuwa ameshika wapi.
Sophia alidua mithili ya mtu ane shanga,katika ya barabara uku taa zikiwa zimeruhusu.
👇ENDELEA👇
Walikuwa hawahelewai na kutambua kama taa za kuongezea magari zimeweza kuruhusu magari kutembea.
Oni kutoka magari yaliyo kuwa nyuma yao ziliendelea kusikia.
Lakini awakuweza kusikia kabisa kutoka na situation iliopo kati yao.
Mpaka kondakta wa daladala lililo kuwa nyuma yao alipo amuna kushuka na kuwagongea kioo.
Hapo ndipo walipo weza kushtuka na kujuwa kuwa wamesababisha foleni kubwa nyuma yao.
Sophia aliondoka gari haraka haraka na kuendelea kusonga mbele.
Kila mmoja ndani ya gari alikuwa kimya sana dhidi ya mwenzake,uku wakiangaliana kwa kuibia ibia.
Wakati ayo yote yakiendelea Frank nae akiwa chini ya mti pembezoni kidogo mwa barabara, akiendelea kuwaza nini afanye ili aweze kufa maana ame jaribu sana kulala barabarani ili aweze kugongwa na magari imeshindikana kabisa kwani kila gari lilikuwa liki mkwepa.
Nja kari na uchovu wa kutembea kwa muda mrefu vitu hivi hakika vilianza kumtesa Frank.
Alipata wazo jingine la kuweza kujiangamiza, aliona ni bora akajitose baharini usiku ule kwani akuna mtu atakae weza kumuona.
Safari ya Sophia na Steven ilitia nanga mpaka mahali ambao Steven anatakiwa kushuka na kumuacha Sophia aendelee na safari.
Waliagana huku sito fahamu ikiwepo katikati yao,Sophia alivuta mafuta na kuendelea na safari.
Lakini Steven kabla ya kwenda nyumbani aliamua kupitia katika stationary moja iliopo karibu na nyumbani kwao na kununua vitabu vitatu vya mapenzi.
Frank alifanikiwa kufika mpaka maeneo ya feri,kusudi na madhuni yake ni kutaka kujitosa ndani ya maji ili aweze kupoteza maisha kwani anajiona hastaili kabisa kuishi kutokana na zambi pamoja na maovu aliyo yafanya.
Wakati uo Steven nae anafika nyumbani,mahali ambako alikuwa akihishi na familia yake yaani baba, mama,pamoja na mdogo wake wa kike aliye kuwa akiitwa Pamela, na kuna mdogo wake mwingine ambe ni mama mkubwa na mdogo aliye kuwa akiitwa Richard na wameachana mwenzi tu.
Maisha ya nyumbani kwako ayakuwa magumu sana na mazuri sana ila kwa kiasi fulani unaweza kusema ni ya kifukara.
Aliikuta familia nzima ikiwa subuleni iki msubiri kwa hamu uku kila mmoja wao aliitaji kujuwa kama Steven amefanikiwa kupata kazi au laah!.
Alingia akiwa na tabasamu zito lilio ambatana na kicheko.
Kwa sauti ya juu huku akinyoosha mikono yake Steven alisema nimefanikiwaaaaaah.
Familia nzima lilisimama na kwenda kumkimbatia kwa furaha ,kwani waliona maisha yao yanakwenda kubadilika baada ya Steven kupata kazi.
Pembezoni mwa bahari ya Indi Frank akiwa anasoma Sara zake za mwisho tayari kwa kujitosaa baharini.
Kwa sauti ya chini uku mikono yake ikiwa nyuma alianza kuhesabu kwanzia tatu kushuka chini ili itakapo fika moja aweze kujitosa baharini.
Alianza kuhesabu 3,2,1......lakini kabla ajajirusha alishikwa shat kwa nyuma na kuvutwa mpaka mchanagani.
Sophia akiwa nje ya geti la nyumbani uku akipiga oni akiitaji kuingia ndani.
Geti lilifunguliwa na kuingia mpaka ndani,Eliza alikuwepo kwa ajili ya kum lack Sophia ambae ivi sasa amemfanya kama dada yake na kwa jinsi walivyo kuwa wanapendana unaweza ukasema ni mtu na dada yake wa kulzaliwa kwa njinsi walivyo kuwa wakioneshana upendo wa kweli baina yao.
Na kitu kingine Sophia ni mtoto wa pekee kwenye familia ile ya kitajiri,ivyo uwepo wa Eliza ulimfanya Sophia kuwa na furaha wakati wote.
Mchanga mwingi uliweza kumuingiza Frank kwenye macho ni baada tu ya kurushwa pembeni na mtu ambae akuweza kumtambua kwa wakati uo.
Mtu yule alimsogelea Frank na kumuinua juu alionekana ni mtu mwenye nguvu Sana.
Frank aliendelea kupikicha macho yake ili aweze kumuona mtu yule aliye weza kuokoa maisha yake alipo taka kujitosa baharini.
Mara ya kwanza aliona ni kama polisi,lakini pindi alipo jaribu kupikicha macho yake zaidi ndo aliweza kugundua kuwa alikuwa ni mlinzi wa eneo lile la feri.
Kwa sauti ya ju na yenye kutoa msisitizo mkubwa mlinzi yule ilisema.
Mlinzi: We kijana kwa nini unataka kujiua?
Frank:Kaka maisha tu ndo yanasabisha yote haya.
Mlinzi: maisha yamefanya nini?
Frank: Ni story ndefu sana kaka iliyo nifanya mimi mpaka kuchukua maamuzi aya magumu.
Mlinzi:Acha ujinga wewe kijana, mbona wewe ni kijana mzuri na una kila kitu fanya kazi na siyo kuka na kuwaza vitu vya kipuhuzi,maisha isiwe sababu ya wewe kutaka kujiua pambana ili uweze kusonga mbele usikate tamaa,sasa sikia nakupa hii buku mbili najuwa ita kusaidia mbele kwa mbele na kingine nisije nikakuona eneo ili tena kwa nzia leo, aya potea.
Frank akuamini kama kaachwa salama, alikuwa akidondoka dondoka pindi alipo kuwa anatembea kwenye mchanga ni kwa sababu ya uchovu na njaa aliyo kuwa nayo.
Alianza kutafuta chakula lakini sehemu nyingi za kuhuzia chakula zilikuwa zimefungwa.
Ni baada ya kuzunguka sana alifika mpaka kariakoo na kubahatika kukuta mgahawa mmoja wa chakula ukiwa ndo unafungwa fungwa.
Alimkuta baba lishe mmoja eneo ilo, alimfuata na kumuelezea shida yake.
Baba lishe aliweza kumjibu.
Baba/lishe:kijana chakula kimetuishia ivyo mpaka kesho asubuhi tena umechelewa.
Frank:Kaka siwezi kupata ata ukoko mana nina njaa sana kaka angu naomba unisaidie.
Baba lishe:Kijana kama nilivyo kuwambia chakula kimeisha sasa kwakua unasema una njaa sana,Hapa kuna mabasi ya vyakula tu ambayo ayo pia uwa atuyatoi bure uwa tunayuza kwa watu wanao fuga mbwa kwa lengo la kulishia mbwa wao.
Frank:Sawa kaka nipate tu nitakula ivo ivo.
Yule baba lishe alizama ndani na kutoka na ule ukoko wa wali ulio changanywa na vyakula vingine kama ugali, mboga za majani, nyama, mahalage, miba za samaki na kazalika.
Frank alitoa ile elfu mbili na kumpatia yule baba lishe kisha akachukua kile chakula na kukimwaga chini.
Frank alika chini na kuanza kula kama mbwa uku machozi yakimtoka na kuendelea kumkumbuka Sophia wake.
Aliye kuwa anampika chakula kizuri sana na kumlisha uku walicheka na kutabasamu kwa pamoja.
Lakini leo imekuwa ni tofauti hii yote ni kwa sababu ya tamaa zake za kimpenzi na ulimbukeni wa mali pamoja na pesa.
Umemfanya leo kupata shida na kuto thaminika na mtu yoyote,amekuwa kama mbwa au mbuzi aliyo kosa mchungaji aliendelea kulia Frank huku akiendelea kula chakula kile kilicho mwagwa chini,na akikiokota taratibu kama kuku.
Leo hii ata alie vipi ni kama machozi ya samaki baharini.
Kilio cha kwikwi na maumivu makubwa moyoni Frank alisimama angali ya kuwa ata kile chakula alicho kuwa anakula ajamaliza na kuanza kujongea taratibu,na.asijue aendako.
Alitembea umbali wa kama hatua kumi na nane kutokea sehemu aliyo kuwa akila chakula.
Ghafla! Aliona kundi kubwa la watu, wakikimbizana mbele yake Frank alisimama na kwa sauti ya juu aliwauliza watu wale.
"Jamani kuna nini? Mbona munakimbia"
Hakuna aliye weza kumjibu kabisa kwani kila mmoja alionekana kuwa na hofu kubwa.
Wakati akiendelea kushanga kundi lile la watu walio kuwa wanakimbia ghafla.
Ali pingwa na kitu kizito kwenye mgongo wake akujuwa ni nini? Ila alienda mpaka chini huku akiwa na maumivu makali sana.
Akiwa chini akiendelea kuugulia maumivu pindi alipo jaribu kuyangaza macho yake mbele aliweza kuona kundi kubwa la polisi.
Hapo ndio alipo weza kujuwa kile kitu kilicho weza kumpiga kwenye mgongo wake kilikuwa ni kirungu.
Walifika polisi wawili mpaka sehemu ile Frank alipo kuwa ameangukia baada ya kupingwa na kitu kinacho sadikiwa kuwa ni rungu.
Walianza kumbuluza kana kwamba ni gunia la mkaa na mkurushia kwenye gari pila ata ya huruma.

INAENDELEA..........
Powered by Blogger.