FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
MATATIZO YA TAFSIRI
Tafsiri
Ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi
kutoka lugha chanzo na kuyaweka mawazo
yanayolingana nayo katika lugha lengwa.
Ni
zoezi la uhawilishaji wa mawazo katika
maandishi kutoka lugha moja kwenda nyingine.
Mwansoko (2006) Kitangulizi cha Fasihi
Tafsiri ni daraja linalounganisha jamii zinzotumia lugha mbili tofauti. Husaidia kueneza utamaduni maarifa na fasihi
toka jamii moja hadi nyingine.
Katika karne 20 Tafsiri zilitumika katika
kuleta maarifa kwa jamii.
- Pia hadithi mbalimbali za mataifa
mengine zimetafsiri kuwa Kiswahili
Mfano: Hekeya
za abunuasi, Tafsiri mbalimbali
zinafanyika katika tanzu mbalimbali lakini tafsiri hizi zina changamoto zake.
Matatizo hayo yanaweza tokana na tofauti ya
lugha, utamaduni, Umahiri wa anayetafsiri, Itikadi ya anayetafsiri.
* Wageni
walitafsiri vitu kwa ufinyu na kumba mambo ambayo ni muhimu
Mfano: Okpewho jamii (2004) Bacha alifanya utafiti katika
kiswhili alisema “katika
jamii za Afrika mashriki hakuna ushairi,
vina, mizani, hisia, wala chochote cha kukonga”
Katika kutafsiri, mtafsiri anaweza
kupunguza au kuongeza vitu.
- Unapotafsiri ni lazima ujue suala la
utamaduni hivyo utapaswa kutafsiri japokuwa
inakuwa ngumu
katika jamii lengwa.
- Kukosekana
kwa radha na vionjo katika jamii lengwa, hivyo mtafsiri hapaswi kupuuza
vipengele vya lugha bali anapaswa kufany kama inavyostahiri.
Tafsiri ni dhana muhimu katika taaluma
yeyote ila ikiwemo fasihi simulizi lakini kuna changamoto zake
Mwansoko et al (2006) changamoto za kutafsiri:-
i) Tofauti za kiitikadi, kihistoria
na kimazingira kutoka lugha chanzi kwenda lugha
lengwa.
ii) Tofauti za kiisimu, ufasiri wa
matini ya kifasihi huna budi kuwa mahiri wa lugha
zote mbili zinazoshughulikiwa yaani miundo
ya sentensi, maneno, Matamshi pamoja na Isimu kwa ujumla. Kwani vipengele hivi hutofautiana kati ya
jamii moja na nyingine.
iii) Istalahi Mpya / Kuibuka
Inapojitoeza istalahi
mpya katika fasii simulizi kutokana na maendeleo ya Sayansi
na Teknolojia
huleta shida kutafsiri. Mfano: katika TEHAMA.
iv) Tofauti
ya Kiutamaduni,
Utamaduni ni jumla ya
mambo yote yanayotawala katika jamii.
v)
Fasihi Simulizi kama kazi ya
sanaa hasa ushairi wa kiafrika unahitaji kuwa na
vionjo kama vina n.k. lakini kazi hizi
zinapo tafsiri ubora wake hapotea yaani vipengele vyake vya kisanaa hupotea.
Waliofanya tafsiri ni wasomi wa kigeni,
wazungu hivyo vionjo walgusin kwa kiasi kidogo sana hivyo ukiviacha vipengele
vya kisanaa unaifanya tafsiri kuwa pungufu.
vi)
Udhaifu wa Tafsiri uliofanywa
na wageni, walifanya jitihada kubwa lakini
hawakuzijua lugha
chanzi kiasi cha kutosha hivyo hawakufikia viwango.
MKABALA WA KIDHAMIRA KATIKA FASIHI SIMULIZI
YA KISWAHILI
NA YA KIAFRIKA
Tunaangalia
DHAMIRA RADIDI
Kwa kawaida Fasihi Simulizi ina Fani na
Maudhuni na Maudhuri ina hisisha:-
- Mwanzo
- Falsafa
- Historia
- Maisha ya waafrika
Fasihi Simulizi ya waafrika inajengwa na
dhumira. Hiki ni kipengele cha maudhui
na kiutamaduni
- Tunapoangalia dhamira radidi tunarejelea
vipera. Mfano: katika ushairi
Dhina inaweza kuhusu Dini, Mapenzi,
Uwindaji, Michezo ya watoto, Jando na Unyago Shukrani, Kuzaliwa kwa mtoto.
Dhamira radidi / Marudidi lazima uwe
umesoma, umesikiliza na kutazama kazi mbalimbali za fasihi vyakutosha.
Urudidi ni dhana ya kitakwimu Udofao yaani
kujitokeza mara nyingi zaidi kuliko dhamira nyingine(mchomozo) katika Fasihi
Simulizi dhamira zipo nyingi zipo zile ambazo husisitiza maadili, Tabia njema,
Masuala ya uzazi, Umoja na mshikamo Ujasiri, Uganga wachawazi, Uhai na kifo,
Malezi n.k.
Mfano: Katika
Mithali kunaweza kuwa na dhamira kama Wema, Umoja Malezi,
Bidii ya kufanya
kazi, Imani kwa Mungu, kukemea uvivu n.k.
Mfano:
- Mkataa wengi ni Mchawi,
- Monagana
upwa hali wali mkavu
- Wema ni hakiba
Jando na Unyago. - Kufanya kazi, usafi, malezi
Mfano: - Majigambo
Samweli M ( ) anasema majiga yanaweza kuhusu ushujaa,
namna gani mtu anapendwa
katika wengine, ufanyaji kazi n.k.
Masimulizi
- Hadithi hubeba dhamira mbalimbali
Mfano: Mapenzi
na ndoa , Uzazi chuki, wivu, Ukewenza
FASIHI NA MFUMO WA MAISHA
Hapa tunaangalia Dhima ya Fasihi Simulizi
katika maisha / au kwa jamii yake kwa kurejelea mifano mbalimbali kutoka katika
Fasihi Simulizi.
Mwanadamu amepitia katika mifumo mbalimbali
ya maisha na katika mifumo hiyo Fasihi Simulizi imekiwa ikitenda kazi yake.
Dhima ya Fasihi Simulizi iliweza kua chany au hasi kutegemea mfano
wa maisha japokuwa katika kipindi cha ukoloni. Fasihi Simulizi ilitazamwa kama hasi eti
walisema ni ya kishenzi. Hapa tunapitia
tanzu kama :
i) Ushairi Simulizi
Umefungamana na maisha ya mwanadamu. Mfano Nyimbo zilituiwa na mwanadamu kuchapuza
kazi na kuifanya kazi kuwa rahisi
- Pia nyimbo zilielimisha, onya na
kuhamasisha shughuli mbalimbali. Jamii
nyingi kwa Fasihi
Simulizi ilikuwa nyenzo muhimu katika kutoa maarifa.
- Nyimbo
ziliambatana na shughuli za maendeleo kama :
kazi
- Burudani
- Za kubembeleza watoto
Fasihi Simulizi
ilifungamana na maisha kwani kulikuwa na nyimbo mbali za kazi
kama za Vita,
Uvuvi, Kilimo, Bembesi,
katika Jando na
Unyago Nyimbo zilihimiza
- Kazi
- Usafi
- Malezi
- Kutii
- Kufanya kazi kwa bidii
Za Harusi zilihimiza:-
- Kupendana
- Kuacha Uongo
- Uvumilivu
- Kuwajibika
Za Dini zilihimiza
- Mahusiano
kati ya wanadamu na Mungu au Miungu yao
Za Sifa
- Maudhri
yake ya majigambo
Za Misiba
SEMI
Vitendawili (Dhima yake) kuna fomula maalumu yaani mianzo
na miisho yake.
Dhina ya kujenga udadisi na kurekodi
historia ya maisha ya mwanadamu na husaidia kujenga kumbukumbu.
- Pia
husaidia jamii kutambua mazingira yanayomzunguka.
Methali
Hubeba Maudhiri na
Dhamira.
Dhina zake,
Methali ni uti wa mgongo wa Fasihi Simulizi
kwani hurejelea katika kila jambo linalozungumzia.
- Methali hutia radha katika
mazungumzo.
- Hupamba mawasiliano zina dhima ya
kiujumi yaani uzuri katika sanaa.
- Hutoa
maadili, kama kuonya, kushauri kukejeli, kuadhibu.
- Pia methali zina busara
- Huibua tafakuri
- Huweka msisitizo juu ya jambo fulani
linalozungumziwa
Fasihi Simulizi
Mlokozi (1996) anasea Fasihi Simulizi
inabeba dhima zake ilibeba dhima hizo za kijamii tangu zamani yaani tangu
wakati wa kina Alstotte,
- Huburudisha kuvura hisia za mwili.
- Ilikuwa inajenga tabia ya jamii
- Ilikuwa inastarehesha – kumpumzisha
mtu baada ya kazi nzito.
Horace
anasema Dhima ya Fasihi Simulizi imekuwa ni sanaa tamu na tumizi. Kama 19 na 20
wahikiki wa kimrx wanasema Dhina
ya Fasihi na Fasihi Simulizi ilibeba maktadha mahususi ulikuwa ni kuburudisha,
kuulimisha, kuhifadhi amali za jamii kuonyesha kweli wa maisha, kuonyesha harakati
za jamii, kuhfadhi lugha.
Kwa ujumla
Wahakiki wa Fasihi na Fasihi Simulizi ni
kama John Ramadhani, Penina Mhando Balisidya, Kahigi, Mulokozi, F. Nkwera Sengo na Kiango, F. E. M Senkoro,
Musokile, Mazrui, hawa wamejadili sana kuhusu fafasi ya Fasihi Simulizi katika
j amii, wamesema Fasihi Simulizi indhima kubwa katika kuelezea utubaka yaani
Masusiano kati ya kundi moj la jamii na kundi jingine.
- Wanadai
kuwa Fasihi Simulizi ina dhima ya Kiitikadi (umwinyi, ubepari ujamii utabaka,
katika jamii kuna wenye nacho na wasio nacho hivyo Fasihi Simulizi hutafuta
usanii.
Itikadi ina mambo
mengi kama:-
- Musuala
ya maslahi kati ya mtu mmoja na mwingine
Mfano - Vitendawili,
misemo
* kuhifadhi
mila za jamii
* kuhifadhi
imani
* Desturi
* Historia
Mfano - Mivigha,
ngoma, ngemezi
Dhima
ya Kisiasa
Mfano - Nyimbo
zinatumika katika siasa.
Mfano - Uchaguzi,
kubadili mifumo mbali nyimbo hutia
hamasa.
FASIHI SIMULIZI NA FALSAFA YA K IAFRIKA
Fasihi Simulizi na Falsafa ya Kiafrika ni
dhana ambazo zina tegemeana na kushikana zinafanana sana. Neno Falsafas “Philesophy” “Philo” LOVE
na Sophia means Wisdom.
:
Philosophy mean study of Love of Wisdom Dhana hizi mbili zinashikamana
kwa vipengele vinavyounda Fasihi Simulizi ni hivyo hivyo huunda falasafa ya
kiafrika.
Mbili (2011) anasema Falsafa ya Kiafrika ni
mtazamo muelekeo na itikadi ya waafrika na wasio waafrika kuhusu mila na
desturi za kiafrika.
Falsafa ya Kiafrika imejikita katika mila
na desturi na vipengele vya Fasihi Simulizi.
Hivyo Falsafa ya kiafrika
inachota vipengele vya Fasihi Simulizi
Matambiko, Uhai na Kifo
Malezi, Jando na Unyago, Dini za kijadi
(matambiko) kuabudu mizimu na wahenga vyote hivyo ni vipengele vinavyounda
fabafa ya Kiafrika.
Vipengele vya Ontolojia ya kibantu inafanna
na ile ya Fasihi Simulizi.
Mfano - Wanaimani dhabiti katika miungu na
hiyo Miungu ipo katika darajia kama Mahoka, Mizimu
(Temples) hata
salamu ya Mwafrika ina hofu ya kifo
* Heshima na Umri
Waafrika wanaheshimu sana umri kuwa mtu
mzima anasadikiwa kuwa anabusara zaidi.
Mfano
- nyumba, vyombo
Katika Fasihi Simulizi dhana hii ya uduara
na ujumi inaooa kuwa vitu bora ni vile vilivyo katika uduara.
Si jambo rahisi kutenganisha Fasihi Simulizi
na Falsafa ya Kiafrika kwani ni dhana zinazotegemea.
Fasihi Simulizi inategemea sana Falsafa ya
Kiafrika kama nyenzo au rasilimali yake pia Falsafa ya Kiafrika inategemea
vipengele vya Fasihi Simulizi.
>>>>>>>>>MWISHO>>>>>>>>>>>