FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
MODULE 1: UTANGULIZI
FASIHI SIMULIZI
YA KISWAHILI -Senkoro (1988 : 10 – 11)
Ni ile inayojitambulisha na
kujihusisha na utamaduni wa waswahili popote pale walipo ulimwenguni. Utamaduni wa waswahili ni ule unaohusu
desturi na mila za waswahili, sayansi sanaa zao, uchumi wao na maisha yao kwa
ujumla. Hali kadhalika inawahusika,
Maudhui, fabafa, mawazo, historia n.k. vinavyoenda na na maisha ya waswahili.
Kwa upande wa lugha, fabafa ya
Kiswahili ni ile inayotumia lugha au lahaja ya Kiswahili.
FASIHI
SIMULIZI YA KIAFRIKA
Ni ili inayojitambulisha na
kujihisisha na utamaduni wa Afrika kupitia jamii na lugha zao. Hivyo utamaduni wa waafrika ni ule unaohusu
mila zao, sanaa zao, siasa na uchumi wao kwa ujumla.
Hivyo fasihi simulizi ya kiafrika
ina mawazo, fabafa, wahusika, maudhui , na dhamira zinazoendana na maisha yao. Imefungwa kwa lugha za kiafrika au lahaja za
lugha hizo.
FASIHI SIMULIZI
Mgullu
(2003:16)
Ni
sanaa itoayo maudhui yake kwa lugha ya maneno ambayo hutamkwa ama hutendwa.
Ni
fasihi inayohusu mkusanyiko wa kazi za kisanaa za binadamu zinazowasilishwa kwa
njia ya mazungumzo au utendaji. Siku
hizi fasihi simulizi huhifadhiwa kwa kuandikwa vitabuni, kanda za video, redio
na santuri.
Mlacha (1980 – 16)
Ni
Nyanja ya maisha ya jamii ambayo huchangia sana katika kuendeleza na kudumisha
historia ya jamii husika.
Fasihi
simulizi huchangia katika kuelimisha jamii kuhusu asili yake, chanzo chake na
maendeleo ya utamaduni wake na maisha ya jamii hiyo tangia zamani.
WAMITILA (2003 : 44)
Ni
dhana inayotumika kurejelea kazi ambazo kimsingi hudokeza na kwa njia ya
msimulizi au mdomo. Hutumika katika
jamii kama njia ya kupashana maarifa kama njia a kupashana maarifa yanayohusu
utamaduni Fulani historia ya jamii na matamnio yao.
OKPEWHO (1992 : 3)
Ni
matini bunifu ambazo huvutia fikra zetu, au hisia zetu, kama vile hadithik
mashairi na michezo ya kugiza (matini).
Sio kwa matini za ukweli kama vile ripoti za magazeti au rekodi za
kihistoria, hata hivyo nazo zikiandikwa kwa kuvutia zinaweza kuwa fasihi.
MLOKOZI (1996 : 24)
Ni
fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia
yam domo na vitendo bila kutumia maadishi.
Hivyo
ni tukio linalofungamana na muktadha Fulani ya kijamii na kutawaliwa na
muingiliano wa mambo sita, fanani (msomi).
Hadhira, fani inayotendwa, tukio, mahali na wakati. Fasihi simulizi inaendana na Tukio.
SEMINA:Swali la 1:
Mbali
na jitihada za wataalam mbali mbali katika kufasili fasihi simulizi na fashi
simulizi ya kiafrika mpaka sasa hakuna fasili iliyotoshelevu. Jadili dai hili na pendekezani fasili yenu.
KUFANANA NA
KUTOFAUTIANA KWA FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
i) Zote zinahifadhi mila, desturi na
historia pamoja na lugha za jamii husika.
ii)
Zote zinahitaji utendaji (maleva –
mavazi)
iii)
Vipera na Tanzu vinaingiliana na
kufanana
iv)
Muktadha, maudhui ya lugha maalum
dhana hizi zinajitokeza kote.
UTOFAUTI
a) Fasihi
Simulizi ya kiafrika ni pana lakini Fasihi ya Kiswahili ni finyu kwani fasihi
ya Kiswahili huchota vipengele fulani katika fasihi simulizi ya kiafrika.
b)
Fasihi Simulizi ya kiafrika ni
kongwe
c) Utamaduni
wa Fasihi Simulizi ya kiafrika ni tofauti na ule wa kiafrika
TANZU ZA FASIHI SIMULIZI NA UAINISHAJI WAKE
Tanzu
ni matawi, Matawi ya fasihi simulizi ni mitindo yake. Uainishaji wa Tanzu za Fasihi Simulizi si
jambo rahisi. Wataalamu wengi wamejaribu
kuainisha lakini wamepambana na matatizo kadha wa kadha kwani:-
i) Afrika
ina utajiri mkubwa wa fasihi simlizi.
ii)
Tanzu hizi zinafanana .
iii)
Tanzu hizo zinaingiliana.
Wageni walipokuja kama vile Finegan (1970), Matteru
(1977) Mlokozi (1966) Catheline Jovi & Kitula Kingei (2005) Wajula & C.
Nungo (1993) Liongo (1992), Wajula R. & Kiman Njogu (2007) na wengine
wamefanya jitihada za kuainisha Tanzu za Fasihi Simulizi. Si rahisi kuainisha Tanzu kwani hakuna mipaka
bayana kati ya utanzu mmoja na mwingine
Hadithi, methali, vitendawili na mafumbo vinaweza
kuwekewa katika kundi moja.Wapo wataalamu walioainisha Tanzu za
watoto na tanzu za watu wazima. Mfano
Methali ni tanzu za watu wazima.Pia ni upi utanzu bora kuliko mwingine, wapo
wataalamu waliosema methali ni uti wago wa mazungumzo.
VIGEZO VYA UAINISHAJI WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
Wafulu R. &
Kimani Njogu wanasema ili tuweze kuainisha tanzu za fasihi simulizi lazima tuwe
na vigezo:
Materru
(1983) ameainisha Tanzu za Fasihi Simulizi katika makundi 3:-
1. Nathari - Masimulizi
au mazungumzo ngano, visasili , misendu
KITULA KINGEI & CATHERINE KISOVI
Wametaja
makundi 4 ya tanzu;
2. Hadithi - Ngano / Hekaya
- Visasili
3. Maigizo - Michezo ya kuigiza
4. Ushairi
Nyimbo kama Rege, Chakachu,
Nyimbo za harusi, Mbolezi,
Wawe za kazi , Mkwaju ngoma, Nyimbo za unyago, Bembelezi
MLOKOZI
M. M. (1996)
Ametumia vigezo
Mlokozi ameainisha Tanzu Fasihi Simulizi katika makundi 6
ambayo:-
1. Mazungumzo
2. Masimulizi
3. Maigizo
4. Ushairi
5. Semi
6. Ngomezi
1. MAZUNGUMZO
Utanzu una
vipera 4:
Maapizo
Tabano
2. Masimulizi
Istiara
Mbuzi
Michapo
Mapisi
Tarihi
Dhajari
Kumbukumbu
Visasili
vya ibada na sini
Visasili
vya miungu na mizimu
3. MAIGIZO
- ya watoto, misiba, sherehe, kidini
4. USHAIRI
SIMULIZI VIPERA
-
Tumbuizo Bembea
Mbolezi
Nyiso
Janda
-
Tukuzo Kongozi
Nyimbo
za dini
Nyimbo
za Taifa
-
Chapuzo kazi au kimai Nyimbo
kuthinga
Za
watoto
Za
vitu
-
Tenzi na Tendi
-
Ghani nafsi – kuikomba
-
Ghani Tumbuizi
-
Sifa Vivugo
– Majigambo
Tondozi
-
Maghani simulizi Rara
Tendi
5. SEMI
v
Methali
v
Vitendawili
v
Mafumbo Chemsha bongo
Fumbo
jina
v
Simo / Misimo
v
Kauli Taulia
6. NGOMEZI
MAZUNGUMZO
Ni mazungumzo yenye sanaa
ndani yake yaliyosheheni mbinu za kifani (fani na Maudhuni) Mfano : Tamathali za Semi kama vile Sitiari, Jashibia.
MBAZI
Ni hadithi fupi zenye
lengo la kuonya.
SALUA
Ni hadithe zinazosimulia
matukio ya kihistoria / zamani
VISAKALE
Visa vya kimapokeo vya
mashujaa
MAPISI
Ni historia ya matukio ya
kweli
TARIHI
Ni maelezo au jedwali la
matukio muhimu na tarehe zake
VISASILI-Hadithi
za kale zinazo zungumzia, asili ya kitu au imani ya mtu.
Mfano:Asili ya binadamu
MAIGIZO -Kulielezea matukio ya dunia kwa namna ya
dunia kwa namna ya
kucheza
/ utani
USHAIRI - Ni
utungo wa kinathumu unaozingatia urari wa vina na mizani
MBOLEZI - Nyimbo
za kuliwaza katika msiba
NYISO - Nyimbo
za jando na unyago
WAWE - Nyimbo
za kazi
KONGOZI - Nyimbo
za kuaga mwaka mara nyingi zinaendana / kuambatanana
Matambiko
CHAPUZO - Nyimbo
za kazi
KIMAI - Nyimbo
za wavuvi
TENZI - Ni utungo unaozungumzia tukio fulani
TENDI - Utungo
unaozungumzia tukio la kiuhujaa
SIFO - Ni nyimbo za kusifu
TONDOZI - Tungo
za kusifu watu wanyama n.k.
RARA - Ni maghani ya kusimulia au tukio fulani la kihistoria na
huenda
sambamba
na ala za muziki.
FUMBO
-JINA -Ni mafumbo ya nayotaja majina.
Mfano: Mwamvua alizaliwa
kipindi
cha mvua nyingi
LAKABU - Kupewa
jina kulingana na tabia. Mfano: Mwalimu Nyerere - Baba
wa
Taifa.
KAULI
TAULIA -Ni kauli zenye
mfuatano wa sauti
NGOMEZI - Ni
tango za ngoma au zinazoambatana na ngoma
>>>>>>INAENDELEA >>>>>>>>>>>>>>