FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA



UHUSIANO WA FASIHI SIMULIZI NA TAALUMA NYINGINE.
Fasihi Simulizi haipo katika upweke au Ombwe bali inahusiana na taaluma mbali mbali ii ni kutokana na ukongwe wake yaani dhima, sifa zake, utendaji wake n.k. infanya ihusiane na taaluma ningine miongoni mwa taaluma hizo ni mziki, soshologia historia, aksolojia, Isimu na lugha, Ethiolojia hata faihi andishi.
UHUSIANO WA FASIHI SIMULIZI NA MZIKI
i)                   Mziki ni nini?  Au ni vitu gani vinafanya utabue huu ni mziki?
                            Ala za mziki kama vile Zeze, Marimba, Ngoma, Manyanga Fasihi Simulizi  ina husiana na mziki ni katika  (i) utendaji katika fasihi simulizi kwani vipera mbalimbali vya fasihi simulizi vina husisha ala Fulani za muziki.  Mfano:     Majigambo, Tenzi
ii)                 Historia, ni taaluma inayochunga matukio kisayansi ya wakati uliopita na uliopo.
Ni taaluma inayoshughulika na uchunguzi wa maisha ya binadamu ambayo yanatuwezesha kujua maendeleo ya mabadiliko ya binadamu.
Fasihi Simuliziina nafasi kubwa katika historia ya binadamu kwa kupitia baadhi ya vipera vya fasihi simulizi.  Hivyo Fasihi Simulizi inatusaidia kuelewa historia yetu ( ya jamii fulani Mfano:  kupitia nyimbo kama vile za vita.
Mfano :Tenzi baadhi ya tenzi za Kiswahili zinazungumzia mashujaa wa Afrika.  Mfano:  Fumo Liyongo kujua mtazamo wa jamii husika katika kipindi Fulani cha kihistoria .
Wanahistoria pia wamechota baadhi ya mambo yao kutoka katika fasihi simulizi.Data za fasihi simulizi zinassaidia kujenga rekodi za kihistoria .
Vipera mbali mbali kama Tendi visakale ,Tarihi, Shajari n.k. vinatusaidia kuelewa historia ya jamii japo kwa kiasi kidogo kuhusu matukio ya watu au mashujaa katika jamii hiyo.
Suala la utendaji  /hutofauti wa vipera vya fasihi simulizi zamani na sasa vinaweza kutusaidia kuelewa historia ya jamii fulani.
Fasihi Simulizi inasaidia kuhifadhi na kuendeleza historia katika jamii.  Mfano:  Majigambo.
iii)              Sosholojia (elimu jamii) / Athropolojia
Ni tuhuma inayochanganya jamii kisayansi ili kujua mienendo yake na njugu mbali mbali zinazo ongeza jamii hiyo.
Mfano:                  Matabaka
                              Dini   
Kijadi
Vipengele hivi tunavipata katika sosholojia na vinatusaidia kuelewa namna ambayo    vinaweza kuzua mienendo.
Hivyo Fasihi Simulizi tangu hapo mwanzo inatusaidia kujua hiyo mienendo au mifumo mbali mbali ya jamii, kipera kinaweza kuwa chombo cha kutetea utabaka au kuchochea utabaka.
Fasihi Simulizi kilikuwa chombo pekee cha kuwasilisha maadili ya jamii kupitia vipera kama vile kitendawili au nyimbo kupitia fasihi simulizi tunaweza kurithishwa utamaduni, mila na desturi za jamii hiyo.
Taarifa za kisosholojia pia zinaweza upatikana katika kazi za kifasihi.  Mienendo mabadiliko mifumo ya kiuchumi na kijamii inapatikana kwa kurejelea kazi za fasihi simulizi.
iv)               UTAMADUNI ( UHUSIANO A FASIHI SIMULIZI)
Utamaduni unapatikana katika Fasihi Simulizi . Fasihi Simulizi ni chombo kizuri cha kurithisha utamaduni wa jamii husika, huthihirika kupitia utendaji wake katika baadhi ya upengele kama vile :             -           Maleba (mavazi)     
-           Utendaji        
-           Mazingira ya utendaji        
-           Vifaa  
-           Fani husika
Hivyo uhusiano kati ya Fasihi Simulizi na utamaduni pia upo katika lugha kwani       
Fasihi Simulizi hutumia lugha.  Lugha ni nyenzo muhimu wa Fasihi husika hivyo Fasihi Simulizi kama chombo na sehemu ya utamaduni inasaidia mambo kadha wa kadha kama vile.              Inakuuza utamaduni
                                                      Inahifadhi utamaduni        
Kueneza utamaduni
Kueleza utamaduni wa jamii hiyo
Fasihi Simulizi ipo katika kila hatua ya maisha yetu.
v)                 ETHIOLOJIA – KUHUSU DINI
Fasihi Simulizi pia inatumika katika dini kama vile nyimbo na maandiko ya kidini ambayo yanaweza kuwa hadithi, nyimbo ambazo zino katika biblia.
Mfano:-Utenzi wa Sudiata, Utenzi Rukiza
vi)               Fasihi Andishi
Uhusiano kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi utafiti unaonyesha kuwa tanzu karibu zote za Fasihi Andishi zimetokana na Fasihi Simulizi.
                  Maigizo yanazaa tamthiliya pia uhusiano huu pia unajitokeza katika nafasi ya Fasihi Simulizi katika utanzu wa Fasihi Andishi.  Fasihi Andishi inanufaika kikubwa kutoka katika Fasihi Simulizi kifani na kimadhui kwa kuchota:-
                  -           Vipera
                  -           Matumizi ya lugha
Vitu hivi vinaleta athari kubwa katika
(i)                 Tamthiliya           -           Fomula za Fasihi Simulizi
Mfano:                  -           Lina ubani, jogoo kijijini
(ii)              Riwaya
(iii)            Ushairi
(iv)            Hadith fupi
Pia kuna mianzo maalumu katika tamthiliya kuna fomula za kiadithi
Mfano:                  -           Niendelee nisiendelee
Vile vile matumizi ya wahusika wanyama, ndege, mizimwi, majitu.
                  Katika Fasihi Simulizi kuna wahusika Bapa
                  Mbinu mbali mbali kama vile Taswira Ucheshi n.k.
                  Suala la kuingiliana kwa tanzu (ndani ya Fasihi Andishi kuna kuwa na
Tanzu za Fasihi Simulizi) kama vile Hadithi, ngano, nyimbo, n.k.  Pia katika 
mashairi kuna utambaji, malumbano na vipera vingine.
            SUALA LA UTENDAJI KATIKA FASIHI SIMULIZI
            Katika Fasihi Simulizi utendaji ni utii wa mgonyo yaani ni suala la msingi.
Mulokozi (1996 :24)  Fasihi Simulizi ni tukio na lina fungamana na matukio ya kijamii na hutawaliwa na fanani (msanii au mtendaji)  Fanani, huyu ndiye mwasilishaji na mtunzi wa kipera.  Fani husika kwa hadhira katika muktadha wa tukio fulani, kazi yake yaweza kuwa kichani au atatunza papo kwa papo.
                        Fani inayotendwa (kipera).
                        Hudhiru / wasikilizaji, washiriki, wachangiaji wahakila, watazamaji hawa
huangalia uzuri na ubaya.
Tukio             -           ni shughuli yoyote ya kijamii ambayo ndio muktadha wa utendaji mfano:            Msiba, Ibada, Harusi, Sherehe n.k.
Mahali            -           eneo mahususi ambapo sana hiyo inatendwa
Wakati           -           muda amaalumu au majira maalumu ya utendaji vipera vingi
vina wakati wake
                        Mfano :           Sifa huimbwa wakati wa kuomba mwingiliano huu wa vipengeli hivi
ndiyo unaoamua fani hiyo iwasilishwe vipi.
            OKPEWHO (1992) “anasema”  Utendaji unatofautiana kutokana na sababu mbeli mbali
kama vile
                        Umri wa fanani
Umri wa hadhira
Nguvu ya fanani, baadhi ya vipera vinahitaji fanani awe na nguvu
 mfano Ngoma
Tukio husika mfano Msiba hauwezi fanana na sherehe.
Aina ya madhari – jukwaa la kutdnda, yaani pale inapotendewa
Vifaa ambatani vinavyotumika na fanani katika utendaji.
Idadi ya fanani
Maleba / Mavazi
Pia utendaji unatokana au unatawaliwa na dhima – tukio ya kipera husika.  Muktadha wa uwasilishaji na namna ya uwasilishaji hutegemea dhina ya kipera katika jamii.
(ii)                   Muda na mahali, ni muhimu kuzingatia kwa kipera chochote hutegemea /
husikumwa na muda na mahali.  Mfano – Matambiko yanafanywa muda gani
            (iii)                  Ni muhimu kujua kama kuna kanuni za kifomula zozote zinazotaawala
kipera husika kinachotendwa.
            (iv)                  Mila na Utamaduni, kila jamii ina mila na utamadunii wake na hivyo
huathiri utendaji wa vipera husika.
                                    Mfano   -         Mavazi (maleba, mavazi maalum ya kisanaa) yaani kipera hiki
kinahitaj aina ipi ya maleba                                  
                                    Sifa za wahusika au watendaji wa kipra Fulani wanapaswa wawe akina
nani.
            Swali:Hivyo utendaji  ni  nini?
            Muluka (1999) -Utendaji ni uwasilishaji wa hadhithi  au ngano unaofanywa na msanii kwa hadhira kwa kutumia mdomo na kuumbatana na matendo ya viungo mbali mbali vya mwili na ishara uso.
Hivyo kila kipera kipo kwa ajili ya kutwa
            UTENDAJI KATIKA VIPERA MBALI MBALI
a)            MASIMULIZI
Vipera vyake; ngano, visasili, Tarihi Hadithi / Ngano.
Finegan (1970) “Oral literature in Africa” katika utendaji kuna kanuni maalum, jamii nyingi zina utamaduni wake.  Hadithi ni utanzu muhimu  katika jamii za kiafrika.  Hadithi ni utanzu wa jioni na mtambaji anazungukwa.
Je kwanini hadithi inatambwa jioni?
            Kwa sababu mchana mtambaji anakuwa k atika utafutaji.
Hadithi ina fomula zake za kuanza na kumalizia – mwanzo na miisho malum
Ukitamba hadithi haubanwi kutumia vipera vingine katika utendaji wake.
Katika kutamba hadithi msimuliaji hatakiwi kukalili ila anapaswa alete upya
fulani wa utendaji wa hadithi hiyo.
Tumia sauti vizuri na iendane na utanzu wenyewe.
Kuna wasimuliaji wazuri na wasiowazuri
Msimuliaji awe mbunifu ili unogesha hadithi
Katika utendaji,msimuliaji aoneshe hisia zake.
            Ufalaguzi:
Ni uwezo ambao fanani anao  katika kuunda kutunga kugeuza na kuiwasilisha kazi ya Fasihi Simulizi papo kwa papo bila ya kujifunza na muundo asilia au na muundo uliozoeleka .
Hivyo katika utendaji wa kipera fulani kuna utungaji mpya kutokana na mbinu fulani unazozitumia.
            Hivyo hadith moja inaweza simuliwa tofauti na wasimuliaji tofauti.
            Utendaji wa kipera hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.
SIFA ZA FANANI BORA
Senkoro anasema Funani anatakiwa afanya  kazi ya ualimu  anae mtoa maoni, msanii, mbutudishaji muigizaji.
      Fanani aifanye hadithi ionekane mpya kila mara anapoisimulia.
      Fanani aifurahia na kujivunia fani anayoitenda, kuisimulia ipasavyo
            Fanani awe mbunifu na awe na kumbkumbu.
                        Suala la utamaduni katika utendaji fanani azingatie utamaduni wa kipera
anachotamba.
            Fanani awe tajiri wa lugha yaani ajue kutumia mbinu mbali mbali za lugha kama
vile nahau, semi n.k.
                        Fanani asiwe na aibu katika utendaji (katika kutumia lugha, viungo mbalimbali.
                        Kujua mambo ya kihistoria kwani Fasihi Simulizi inapitia vipindi mbalimbali.
            UTENDAJI WA K IPERA CHA SEMI
1.            METHALI
Ni usemi mfupi wa kimapokeo unadokeza majumbo mazito au fikra zinazotokana na uzoefu wa jamii husika.Katika utendaji unaweza tofautiana na vipera vingine kwani utendaji wa methali lazima unajitegemeza wakati wa kutenda fani nyingine, mfano mkutano, maongezi ya kawaida mjadiliano, hadithi katika kumkanya mtu.Kimsingi watambaji wa methali ni watu wazima (wazee) kutokana na kuishi kwao k atika jamii kwa muda mrefu.
2.            VITENDWILI
Utendaji wake si tegemezi kama methali bali kinasimama chenyewe kwa kufuata kanuni zilizowekwa na jamii husika.
Mfano katika kabila la Wajaluo ukishinda kutegua unaomba upewe mke au
Mme
Katika jamii nyingine unapewa mji

3.            MAJIGAMBO
Jamii ya Wahaya ni jamii ambayo maarufu kwa majigambo huu ni utafiti wa kitaaluma.  Mfano Rubanza (2004), Method jamaa hawa wote wameangalia jinsi ya Wahaya.Katika jamii ya Wahaya majigambo yalikuwa na muktadha wake maalum walikuwa wanatamba mbele ya mtemi kabla ya kwenda vitani, baada ya kurudi toka vitani harusi n.k.
Ø  Kwa Wahaya mjigambi huhigamba mbele ya watu, sherehe ambayo inahudhuriwa na Mtemi na kuna namna ya kuanza (wanajitambulisha kwa kujigamba) pia kuna namna ya umalizaji.
Ø  Unaweza kumaliza kwa kutoa heshima kwa Mtemi au kiongozi aliyepo pale.
Lugha
Ø  Katika majigambo, mjigambi yupo hum kutumia lugha ya kujikweza.
Ø  Kuna maleba yaani mavazi maalumu, mfano katika kujigamba wanavaa kanzu ndefu, pia hushika silaha kama mkuki, panga n. k.
Ø  Pia majigambo huambatana na ngoma yenye mapigo ya pekee, na
maandamano ya namna fulani.
Ø  Katika majigambo kuna zawadi, shujaa aliyeshinda au aliyrudi toka
kuwinda, vitani n.k. hupewa zawadi kama pombe.
Ø  Wale walioenda vitani au kuwinda wakashindwa zawadi yao ilikuwa maji
ya kunywa na kinyesi cha ng’ombe.  Hii ilikuwa inaleta umakini kwani kurudi na kinyesi ilikuwa ni aibu.
Miaka ya 1960 utendaji wa majigambo uliathiriwa sana kutokana  na mabadiliko ya kijamii na kiutawala.
>>>>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>
Powered by Blogger.