FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
MODULE 2:
ISTORIA YA FASIHI SIMULIZI YA
KISWAHILI
(a)
Historia
ya ushairi mulizi
(b)
Historia
ya masimulizi
(c)
Historia
ya Thieta.
HISTORIA YA MASIMULIZI
Ili kupata historia ya msimulizi hatuna
budi kuwaangalia wataalamu
mbalimbali. Tafiti zilifanywa Afrika
kama ya 19 na 20 kuhusu maisha ya muafrika,
Na wanazuoni hao walikuja na mitazamo yao
Wazungu / Wageni pia walifanya utafiti
kuhusu utamaduni wa mwafrika.
1.
NADHARIA
YA UBADILIKAJI TARATIBU. (EVOLUTIONS) Hawa wanafanya tafiti mbalimbali
Ulaya na Afrika. Nadharia hii iliasisiwa
na Charles Darwin (Mwingereza) hivyo wataalamu wengine wanatumia mtazamo huo
kuasisi Fasihi Simulizi.
Mtazamo kama huo wa mabadiliko ya
viumbe pia ulitumiwa na wataalamu wa
masuala ya
kiutamaduni
- Pia
metumika katika mamla ya kifasini kwa kuchanganya Chimbuko la
fasihi simulizi ya afrika kwa kulinganisha
na Wataalamu: Edward Burnet Toylor,
James George Frazer ni wafuasi wa mkabala wa mabadiliko ya viumbe hai katika
kuchunguza fasihi simulizi.
- Wanaangalia
binadamu na mazingira yake
- Wanaona
kuna kanuni Fulani muhim zinazochangia maanzi ya binadamu.
Ili kuelelwa utamaduni wa kijadi na jamii
yeyote ile lazima uilinganishe na jamii nyingine.
- Walichunguza mila na desturi za jamii
kwa kina kama vile mivigha, uchawi.
- Walichunguza
katika jamii zao za Ulaya baadaye wakaja Afrika.
John Roscoe
alifanya utafiti katika jamii ya Baganda
Robert Battray alifanya katika
jamii ya Akan huko
Ghana.
- Walichunguza
hadithi, nyimbo, Methali na vipera vingine.
- Katika
uchunguzi wao “Finegan” na “Okpewho” wanasema “Wametafiti Ulaya na Afrika”,
kuna ukoo au jamii moja ambayo imezagaa ulimwenguni kote hivyo kama tuachungua
jamii mbili katika kipindi kila kitu cha ukuaji wa utamaduni matokeo yake ni
kuwa mila na desturi zao zituonyesha kufanana.
Heri chatelaine
alifany uchunguzi kuhusiana na hadith huko Angola na anasema Kimsingi watu wa
Afrika ni kama watu wengine ulimwenguni na hadith au agano za kiafrika ni tawi
toka katika mti mmoja wa kiulimwengu.
- Kazi
yeyote ya kifasihi simulizi ya kiafrika ni masalia au mabaki ya fasihi
iliyotanguli (Ulaya)
NADHARIA YA MSAMBAO (DIFFUSSION)
Pia ni wageni toka Uswisi, Marekani n.k.
pia walitafiti masimulizi hata hadithi, waliangalia maisha ya hadithi Fulani
maalumu.
Mtaalam Stith Thampson aliangalia jinsi
hadith zinavyo fanana kiproti kai ya hadith za Kiafrika na India, Ulaya Arabuni
na sehemu nyingine ambazo watumia toka Afrika walipitia.
- Wanachunguza
asili ya hadithi zinazopatikana Afrika kihistoria na kijiografia.
- Wanachunguza
athari kutoka nje
- Wanahitimisha
kama hadithi mbili kutoka jamii mbili zikionyesha sifa zinazo
fanana ni kwasababu
kuna kipindi Fulani huko nyuma jamii hizi mbili ziliingiliana.
mwingine.
vinavyo fanana
Wataalam:
Jacob Grimm na Wilheton Grimm (wajerumani)
walikusanya kazi
nyingi kutoka India na Ujerumani na wakaja
na kitabu “House hold tolies” 20.
Walisema “kama kuna ufanano wowote kati ya hadithi zinazosimuliwa Afrika
na Ulaya hizo za Afrika ni chpukizi ya hadith Mama ambao ni utamaduni wa India
Ulaya”.
“Kwa kawaida utamaduni huenea toka kwa watu
wengi nguvu (superior) kwenda watu wa chini na si vinginevyo” Thompsona”The
Anasema “ kama kuna ufanano kati ya hadithi za ulaya na Afrika ni kutokana
kwamba wa Ulaya walizileta Afrika kipindi cha biashara ya watumwa”
(3) KIAFRIKA/
UTAIFU
Katika mkabala wa
kiafrika kimsingi, wanapinga mawazo yaliyotolewa na wageni
hawa.
Finegan:“Wanaubadilikaji na wanamoambao
walishindwa kuona kuwa hadith za kiafrika zimetoka na miktadha yao ya kijamii
na wala sio masalio hivyo anaona kuwa mtazamo huu si sahihi kabisa.
Hivyo mkabala huu wa kiafrika unachochewa na mawazo finyu ya
kimagharibi.
Hivyo mawazo ya waafrika yapo pia kwa
waafrika wengi na wanasema wanazuoni wengi, hawakuelewa vizuri fasihi
yetu. Alexis Kayame (Ruanda) Alifanya
utafiti katika ushairi simulizi wa Rwanda.
Kwabena Nkryis - Alitafiti
Fasihi Simulizi na muziki huko Ghana.
Adebayo Babalola - (Nigeria)
Amadu ba - Mali
T. Y. Sengo - Tanzania
M. M. Mulokozi - Tanzania
P. Mramu - Tanzania
Mfano: Sengo
(1985) anaelezea asili na chanzo cha ngano, alichunguza jamii ya Wazanzibar
- Anasema
“Ipo pale tangu jamii ilipokuwepo pale”
Binadamu alitung ngano ili imfae katika
maisha yake ya kiuchumi, kijamii na kisuikolojia.
- Mazingira
yanayomzunguka binadamu ndiyo yanayojua chanzo cha ngano (fasihi simulizi)
Mfano: Ngure (2003) “Utanzu wa mwanzo kabisa
wa fasihi simulizingano au hadithi”.
Anasema”Ngano hizi zilitokana na Uwoga na
haja ya mtu kuanza kuijiuliza maswali kuhusu vyanzo vya asili ya dunia, binadam
kifo n.k.
HISTORIA YA USHAIRI SIMULIZI
Mulokozi
(1996) anasema “Ushairi simulizi ni utungo wa kinadhumu unaofuata kanuni fulani
za urari wa sauti, mapigo ya lugha na mpangilio wa vipashio vya lugha.Chanzo
cha fasihi hakiwezi kutenganishwa na utamaduni fulani, maisha na lugha yao. Hivyo
asili ya ushairi wowote ni nyimbo. Asili
ya ushairi wa Kiswahili / kiafrika ni nyimbo za wantu pamoja na utamaduni
wao.Ushairi ulianza pale binadamu alipogundua lugha baada ya kuacha hatua ya
uhaywani na kuwa razini, ubunifu wa lugha ulirahisisha mawasiliano.
Pamoja
na kugundua zana mbalimbali za uzalishaji pia alitumia sanaa ili kurahisisha
kazi hizo. Ushairi unaojitokeza katika
nyimba ulitumika kama chombo cha kuzalisha mali. Nyimbo zilimsaidia kuchapuza azi kwani zilimpa
nguvu na kumsahaulisha ugumu wa kazi.
Wimbo wa kazi uliimbwa kwa kufuata mapigo ya zana za kazi.
Kwasababu
kazi zilifanywa kwa umoja (upamoja), kulikuwa na kiongozi aliyeimba wimbo na wngine waliitikia
kwa kufuata milio maalumu ya zana za kazi.
Kazi izo ni kama kilimo, uvuvi, uwindaji n.k.
Ushairi
pia ulianza kutumika katika matambiko ambayo ni ibada za kijadi. Matambiko huwa na sala /maombi maaalumu kwa
mizimu au miungu. Matambiko haya
yalifanywa kwa matukio maalumu na vipindi maalumu.
Mfano:Kumaliza
na kuanza mwaka, kuomba mvua n.k.
Wimbo
ni kazi ya sanaa hivyo lazima uwe na ubunifu wa vinana mizani pamoja na
maudhuni maalum. Kiongozi wa nyimba
anaitwa manju / malenga ambay huwa ni fundi stadi wa kuimba. LAKINI Si kila wakati wote kulikuwa na vina
vya mwanzo, kati na mwisho bali vina vya upande mmoja au mbili vilijitokeza.
Pia
nyimbo zilizingatia idadi ya mistari katika wimbo husika. Na mizani ilizingatiwa. Dhima za nyimbo hizo ziliimbwa kwa lengo
lakutmbiza ambako kuliambatana na kuchapuza kazi.
USAHIRI SIMULIZI ULIANZA LINI?
Si rahisi kueleza kuw aushairi ulianza lini
kwani utanzu huu una historia ndefu na ni mkongwe ukilinganisha na tanzu
zingine.
Wengine
wanasema utanzu huu ulianza kabla ya kama ya 10 kutokana na tungo simulizi za
kibantu hususani nyimbo na ngoma.
Aman
Abeid ( ) katika kitabu kilichoandikwa
na Mathias Mnyampala (1965) “Waadhi wa Ushairi” anasema kabla ya watu hawajajua
kuandika, mashairi yalitungwa na kuimbwa katika jando, unyago, ngoma, harusi
n.k. kwani mashairi si kitu kingine ni nyimbo.
Waliokuwa wanaimba na kutunga nyimbo waliitwa Manju au Malenga.
Mabadiliko
yalianza kujitokeza taratibu hususani walipokuja waarabu waliofundisha kusoma
na kuandika. Ndipo ushairi ukanza
kufungamana na maisha ya binadamu kuanzia kuzaliwa mpaka kufa.
Hivyo
maudhui yalianza kumhusu binasamu na mazingira yake.
Ngure
Alex (2003) anathibitisha kuwa asili ya ushairi ni nyimbo ambazo zilianza
kuimbwa bila kufuata utaratibu maalumu.
Ushairi huo haukuandikwa kwasababu watu hawakujua kusoma na kuandika
bali zilifungwa hovy hovyo bali zilifuata tukio husika.
Wamitila
(2004) Ushairi ulitokana na nyimbo.
Ushairi una vipera vingi
(a)
Nyimbo
(b)
Maghani
(c)
Sifo
(d)
Ngonjera
(e)
Shairi
Katika ushairi kuna tendi ambapo Finnegan
(1970, 2012) anasema ushairi katika bara la Afrika hususani tendi hazikuwepo. Yeye anatoa sifa za jumla za tendi nazo ni:
a)
Utungo
wa kishairi / nudhumu
b)
Lazima
uwe mrefu
c)
Upatanifu
ie visa vinavyoungana kimantiki
d)
Uwe
na maudhui
e)
Husimulia
maisha na tendo la kishujaa kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa
kwake.
Watafiti waliofuata baadaye wakaona
kuwa sifa hizo hazitoshelezi na wakaongeza
a)
Masimulizi
b)
Masimulizi
yatolewe kishairi
c)
Tendi
hufungamana na tukio la kihistoria u kijamii
d)
Zielezee
ushujaa
e)
Tendi
huimbwa / hughanwa
f)
Tendi
hufungwa pao kwa papo
g)
Tendi
huzingatia muktadha wa tukio
HISTORIA YA THIETA NA DRAMA
Wamitila (2008) anasema thieta hitwa “Sanaa
za maonyesho”
Penina Muhando anasema “Sanaa za maonyesho
ni Sanaa ambazo huwasilishwa ana kwa ana, wao kwa hadhira, hutimia usanii
kiutendaji. Anaona kuna aina kuu mbili
za sanaa za maonyesho ambazo ni:-
a)
Sanaa
za Maonesho za jadi
b)
Sanaa
za Maonyesho za Mamboleo.
SANAA ZA MAONYESHO ZA JADI
Ni zile ambazo zimechipuka katika jamii ya
Tanzania kama vile Mivigu, Majigambo, ngoma.
Mivigha-Jando, Unyago, Matambiko
Utambaji hadithi n.k Sanaa hizi zinasaidia sana jamii kuwasiliana
na miungu, mizimu, mapepo n.k. kwa lengo la kuwaeleza matatizo yanayowakabili
jamii kama vile Ukame, njaa, uzazi magonjwa n.k.
Pia huwa na mafunzo ndani yake na heleza
historia ya jamii.
- Kueleza
tabia / tajiliba za jamii husika. Sanaa
hizi zilianza kabla ya ujio wa
wakoloni.
Sanaa hizi huambatana na :- Vitendo kisanaa
a)
Muziki
b)
Kucheza
ngoma
c)
Kutongoa
mashairi
d)
Matendo
ya mwili
e)
Matumizi
ya lugha
Sanaa za Maonyesho (wamagharibi) huwa na
mambo yafuatayo:
(a)
Lazima
uwe ni mchezo
(b)
Uwanja
wa kiutendaji
(c)
Mtendaji
(d)
Watazamaji
Sanaa za maonyesho za jadi zilifungamana na
utamaduni wa jamii na ulizingatia:-
(a)
Dhana
inayotendeka
(b)
Wambaji
/ Hadhira
(c)
Uwanja
wa kutendea
(d)
Watazamaji
SANAA ZA MAONYESHO ZA KIMAMBOLEO
Hizi zimetokana na ujio wa wageni hususani
tamthilya katika Tanzania tamthilia zililetwa na Waingereza kwa lengo la:-
(a)
Kujifurahisha
(b)
Kujikumbusha
maisha ya huko kwao
Drama inauhusiano wa karibu kabisa na
tamthiliya. Tamthiliya za mwanzo ziliiga
tamthiliya za Shakespeare na zilitafsiriwa kutoka kazi za Shakespare ili
kufifisha utamaduni wa mwafrika.
Tamthiliya hizi zilisambazwa kwa kutumia
(a)
Elimu
(b)
Dini
ya Kikristo
Dhima zake:
(a)
Kuchekesha
(b)
Kufundisha
kuwatii wakolono
(c)
Kuwapumbaza
wafrika wasifikirie juu ya kupambana na ukoloni.
Baaada ya Ukoloni sanaa hizi zilibadilika
kwani zilianza kusisitiza siasa ya ujamaa na kujitemea ustawi wa maisha ya
mtanzania. Mnamo 1970 zilisisitiza
ujamaa, usawa kwa binadamuk kulinda uhuru, haki za wanawake na watoto n.k.
Drama ni maigizo yenye mambo ya fuatayo:
(a)
Mpangilio
(b)
Wahusika
(c)
Utendaji
Sifa za drama ni uigaji wa uhalisia yaani
kuiga jambo halisi ambalo liko katika maisha yetu ya kila siku.
Wamitila (2004) anasema kuna aina nyingi za
maigizo
(a)
Mivigha
(b)
Ngomezi
(c)
Utumbi
(d)
Michezo
ya jukwani
(e)
Ngonjera
(f)
Utani
(g)
Majigambo
(h)
Vichekesho
(i)
Mazungumzo
Mulokozi (1996) anasema maigizo yanatumia
watendaji ambao juiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine kwa lengo la
kubanidisha au kutoa ujumbe Fulani.
Aina za Maigizo:-
(a) Maigizo
ya watoto
(b) Maigizo
ya msibani
(c) Maigizo
ya Sherehe
(d) Maigizo
ya Kidini
Vipera vya Thieta ni pamoja na Mirvigha,
Dansi, Sarakasi, Masimulizi ya kidrama, Ngoma, Majigambo, Sherehe za jando na
Uyago, Matambiko, Ngomezi Utambaji wa Hadithi n.k.
Thieta ya jadi ilifungamana na kazi za
maisha ya kila siku ya jamii husika, ilijikita katika mila na desturi au
utamaduni wa jamii hizo, zilikuwa na lengo maalumu la kijamii na kiutamaduni
ili kurithisha amani kwa vizazi vya jamii hizo.
Pia zilikuwa kwa ajili ya mawasililano kama vile Ngomezi, Matambiko ni
kuwasiliana na miungu ili kutatua matatizo mbalimbali katika jamii. Wageni walileta vichekesho na Drama ambayo
kwa wao thieta au sanaa za maonyesho zilikuwa na mamba 4 :-
Thieta ya jadi ilihitaji
Sehemu za kutendea zilkuwa tofauti
kulingana na kipera husika.
BUBWI (MIME)
Nikipera kilichoanzia ulaya (Wagiriki na
Warumi)
Ni aina ya utendaji wa kisanaa ambapo
hadithe husimuliwa kwa kutumia matendo ya mwili, Ishara za uso na matendo.
Kwa kutumia vitendo unaweza kuwasilisha
hadithi ikieleweka vizuri. Inahitaji
ujuzi wa viungo vya mwili na kujua utamaduni wa jamii husika. Kipera hiki ni maarufu ulimlwenguni pamoja na
Afrika.
NGOMA:
Ni chombo cha kimuziki, ni Uchezaji ni
sherehe katika kufanikisha vipera mbali
m bali. Ni kifaa cha kimuziki
katika jamii za kiafrika.
Ngongi hutumia ngoma inayoongea katika
jamii za jadi huwezi kuzungumza Thieta bila kutaja ngoma katika Fasihi Simulizi
na utamaduni ni lazima uitaje ngoma katika kutoa taarifa n.k.
Baadhi ya misiba pia kutumia ngoma katika
tawala za kijadi ngoma huweza kutumika:-
Ngoma huambatana na Nyimbo hivyo Nyimbo ni
kipera muhimu cha Thieta
- Hutumika
katika utendaji wa vipera mbalimbali kama vile Matambiko huambatana na nyimbo
Nyimbo ikiambatana
na ngoma huonesha hali ya jamii kama furaha, huzuni
MALEBA
Ni muhimu katika
utendaji ingawa si kila kipera huhitaji mavazi maalum. Baadhi ya
vipera Majigambo,
Ngoma, Jando na Unyago huhitaji mhusika avae Maleba maalum.
- Maleba
hutegemea ubunifu wafanani. Mfano: Nyimbo za uganga, hivyo Maleba huweza
kuambatana na zana mbalimbali katika utendaji kama vile kibuyu. Maleba hayavaliwi kwa kuvutia tu hadhira bali
huwa na dhima mbalimbali
>>>>>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>