FASIHI SIMULIZI YA KISWAHILI NA KIAFRIKA
KILONGO MASIMULIZI
/ MATINI SIMULIZI
Inaweza kuwa ya
kipera chochote, tunaangalia Matumizi ya lugha katika muktadha fulani
wa kijamii yaani
Lugha inayotumika kuelezea Miktaha mbalimbali.
Pia katika kilongo
tunaangalia vitu
vinavyoonekana / vionwa au vinanvyotokaa / vionwa au vinavyotokaa
katika kipera kila
Mfano: Maleba yanawasilisha kitu gani,
Lugha, Matendo, Ishara
mbalikbali katika
utendaji wa Fasihi Simulizi zana mbalimbali ambazo huwa tunaziona.
Ili kuelewa kilonzo
simulizi ni lazima uelewe utamaduni wa jamii husika .
SIFA /JIRABAINIFU
NDUNI ZA KIFANI ZA FASIHI SIMULIZI YA
KISWAHILI NA
KIAFRIKA
Fani ni mbinu na
mtindo wa namna ya kuwasilisha mandhui ya kazi ya fasihi
Fani ni ufundi
unaotumiwa na msanii kuwasilisha kazi yake, inajumuisha Mandhari,
Lugha, Mtindo,
MUUNDO
Ni kipengele cha fani, Miundo ya vipera vya
Fasihi Simulizi ipo mingi kulingana na muundo wa kipera husika.
Muundo katika Fasihi Simulizi ni mpango na
mtiririko wa kazi ya Fasihi Simulizi kwa upande wa visa na Matukio. Tunaangali namna mtunzi anavyounganisha wazo
moja na lingine, Motari mmoja na mwingine yaani jinsi kazi ilivyofunywa kazi
nyingi za Fasihi Simulizi muundo wake huwa hauwi mrefu sana bali huwa mfupi,
ingawa hutegemewa fanani anaye simulia.
VIPERA MBALIMBALI NA JINSI M IUNDO YAKE
INAVYOJITOKEZA
Semi
i) Methali
Umbo
lake muundo wake ni wa pande mbili ambao hunyesha hali tendo Masharti na upande
wa pili huonyesha matokeo
Mfano: Mfifha uchi hazai
Methali
nyingi huwa namuundo wa kishairi, yaani Mapigo ya kimuziki, urari wa kimizani,
mpangilio fukani wa vina.
Mfano:Haba
na haba hujaza kibaba
ii) Vitendawili
Huwezi
kuwa katika sentensi neno moja au miundo ya kishairi. Vitendawili huwa na miundo ya kiformula huwezi
kubadilika na mamii husika.
Mfano:Kitendawili
!!! Tegaa !!!
kupata jibu na kama jibu si sahihi unaomba upewe zawadi fulani, kama mji
katika jamii nyingine huweza kupewa mume au
mke na baada ya mtegaji kuridhika anatoa jibu.
iii) Hadithi
/ Ngano
Ni
masimulizi ambayo si ya kishairi, hadhithi nyingi hutumia muundo, rahisi
/sahihi au wa moja kwa moja, utakuwa na Mwisho – kati – Mwisho hivi vyote
vinakuwa nas formula maalumu. Muundo
sahihi husaidia sana hadhiru kufuatilia hadithi husika. Muundo husaidia fanani kuzingatia kusikia kwa
usikivu, muundo huwa moja kwa moja haya hayakatazi kuchomeka vipera vingene ndani
yake kama nyimbo, Methali.
Safari
Hadithi nyingi zinahusu safari
Pia kuna muundo wa ndani ambao
husaidia kuibua maudhiri mbalimbali
Mfano:Falsafa Mila na desturi
Ushairi
i) Shairi
Vipengele
vya kimuundo ni vipande (Shairi la kimapokeo), Misharoro (la kisasa) Beti,
Mizani, Vina, lakini hutegemea shairi linalozungumziwa.
King’ei
& Amata (2001 : 02) Taaluma ya
Ushairi
“Muundo
ni Luray a nje nay a ndani ya dhairi”.
Ni Luray a utungo kama unavyosikika au onekana kutokana na midundo au
mapigo yake. Katika shairi Luray a nje
ya shairi inajidhirisha katika umbo lake, je linatumia kanuni za kiamdhi au la
na muundo wa ndani unaangalia, Lugha, Falsafa, funzo Maudhui. Hivyo basi muundo ni jumla ya fani na
maudhui.
ii) Majigambo
Huweza kutumia formula Fulani ya
kufungulia jigambo hilo,
Mfano:
huanza kwa kujitambulisha, kisha huanza kutama na hitimisho ni
kumshukuru
Mfalme n.k. hivyo yanamtiririko Fulani /
maalum.
SIFA ZA KIMTINDO KATIKA FASIHI SIMULIZI
Ni
jinsi zinavyojitokeza katika utunzi au utendaji wakeDhana ya mtindo ni pana
maana ya Mtindo;
Senkoro
(2001 : 24) Ni upangaji wa fani na
maudhui katika kazi ya fashihi ambayo hudokeza nafsi na hat upekee wa mtungaji
wa kazi hiyo.
Mulokozi
(1996 : 101) Mtindo hujidhihirisha katika vipengele mbali
- Matumizi
ya lugha
- Utenzi
wa maneno
- Mpangilio
wa maneno
- Wizani (urari wa mapigo ya sauti)
- Mpangilio
wa sauti za lugha ili kuleta athari Fulani.
Mtindo
ni upekee wa mtunzi haufundishiki kwa kutegemea uwezo mazoea ufundi, hisia na
unafsi wa mtunzi.
watoto, wazee.
Tamathali mbalimbali za Semi:
Kila
fanani ana upekee wake katika kutunga kazi, kipera kimoja kinaweza kuchomoza zaidi
kuliko kingine.
- Mtindo
wa kimajibizano
- Kimolojia
- Mtindo
wa kimasimulizi
Picha, Ishara,
Tanakali Sauti.
VIPENGELE VYA LUGHA
a)
Ishara
Ni wazo, tendo, au dharia, kitu kimoja
kinachowakilisha dhana au tendo au kitu kingine kuwa ishara za lugha kama
vitendo, lugha, mawazo, Mavazi. Ishara
inaweza kuwa kitu h alisi, kikarejelea kitu ambacho ni cha kidhahama. Matumizi ya Ishara hutegemea ufundi wa
fanani. Ishara hutumika katika vipera mbali
mbali kuna ishara za kiutamaduni Fulani na ishara za kiulimwengu. Ili kuelewa utendaji lazima ujue mbinu za kisanaa kama hadhira na kama fanani.
- Matumizi
ya Ishara utendaji Fasihi Simulizi hutegemea maarifa na utamaduni wa jamii hiyo. Ishara ni mbinu ya kuumba picha ya jambo
katika mawazo ya msikilizaji, msomaji kwa kutumia lugha.
Kuna Taswira mbalimbali
TASWIRA
Ni neno au maelezo ambayo hutumika ili
kuunda / kuchora picha ya kitu Fulani hali dhana au wazo Fulani akilini mwa
msikilizaji au msomaji.
Katika akili unaweza kuona, kuonja
kuchukia, kudharau n.k. na husaidia kushirikisha
ubongo kufanya kazi.
- Husaidia picha kupanda akilini. Mbinu hizi hutuika katika vipera mbalimbali.
TAARUKI
Ni mbinu inayotumiwa sana
- Ni tamathali ambayo inamsimamisha
hadhira, haimfikishi kule mwisho haraka;
kutokana na shauku
ya kutaka kujua mambo yaliyo au yatakayojiri.
- Ni tamathali ambayo inaonesha
kutoonyesha kitu kwa muda fulani au hadi
mwisho. Hutumika
katika kazi za fasihi. Mfano: - Ngano
TAKRIRI
Ni kujjirudia, kujirudia kunaweza kuwa
kiirabu, konsonanti, neno kipandi cha mstari katika shairi, mstari mzima, vina,
wazo muundo.
Mfano: Hadith
hadith
TABAINI
Ni tamathali ambayo huundwa na maneo au
mawazo yanayokingana ili kuleta msisitio wa wazo hilo
Mfano: Asiyejua maana haambiwi maana. Chuku, Tashibira, Sitiari, Tashihisi,
Usambamba, Tanakali Sauti
USAMBAMBA
Ni kauli ambazo zinafanana kimuundo au
kimaana na huwekwa pamoja. Miongoni mwa
mifanano hiyo. Pia mbinu nyingine ni
kama wahusika halisi na wasio halisi.
Maudhari inaweza kuwa halisi au ya kufikirika.
MOTIFU
Ni kujirudia kwa dhana fulani au kitu
fulani.
Mfano: Motifu
ya Safari - Hadithi nyingi zina safari
Motifu ya Namba
Katika hadithi namba Fulani inaweza
kujirudia mara kadhaa.
USHAIRI
Lugha ni nyenzo muhimu katika uwasilishaji
wa fasihi simulizi.
Ushairi una uhuru wa kutumia maneno yake na
mipangilio tofauti tofauti ya sentensi.
- Pia
katika ushairi kuna matumizi makubwa ya Ishara, mafumbo ya taswira.
Katika ushairi lugha ya kishairi ina m
iundo ya sentensi na mpangilio wa maneno ambayo ni adimu kupatikana katika
tanzu ngingine za kifasihi hutumia lugha ya
mkato ili kuleta radha.Lugha ya kistari ina utaraibu Fulani jaalumu na
inaleta radhu Fulani ambayo inaweza ikahuzunisha au kukuamsha.
Lugha ya kishairi huwa ni ya mkato
hfupishwa ili kupata mlingano wa silabi.
Mshairi anaaweza kubadili maneno kama anaweza kubadili maneno kama
anvyotaka ili kupata vina, mizani n.k.
BAADHI YA MBINU ZINATOA UHURU WA KUCHEZA NA
MANENO
a) Hujitokeza kwa njia ya kubadili mpangilio
wa maneno
Mfano: Mtoto mzuri - Mzuri
mtoto
b)
Kwa
kutumia Inkthari - kufupisha
maneno
c)
Mzada
Ni kurefusha neno ili kupata mizani
inayohitajika bila kupotosha maana iliyokusudiwa.
d)
Tabiri
Ni kubadili mpangilio wa herufi au vitambwa
katika neno ili kupata vina unavyo vitaka
SEMIOTIKI YA UTENDAJI KATIKA FASIHI SIMULIZI
Semiotiki
Ni taaluma ya mipangilio ya ishara
inayomwezesha binadamu kuona vitu au hali
kama ishara zenye maana. (Wafula na Njogu 2007 : 103)
Wamitilal (2003 : 90 – 91) Semiotiki ni aina ya nadharia ya kimuundo
inayojishughulisha na ishara na maana za ishara hizo katika kazi za fasihi.
Semiotiki ni namna hadhira inayo fasili
ishara mbalimbali kazi ya fasihi inayotendwa.
Ishara hizo huweza kuwa katika neno, vitendo, shamfas, sauti n.k. Katika utendaji kitu chochote kitakuwa
na maana kama utakifasili.
Mfano: Maleba
ya mhusika yanaashiria nini n.k.
Katika Ishara / Semiotiki kuna usimbaji
yaani kuelewa mitindo mbalimbali katika
matini.
Katika Semiotiki kuna Misimbo au kaida
muhimu katika kufasili kazi ya fasihi.
Kuna aina 5 za Misimbo:
1.
Msimbo
wa Matukio
Katika kazi ya fasihi matukio mbalimbali
yanasaidia kuielewa kazi ya fasihi hiyo.
2.
Msimbo
wa Kihemenitiki
Husaidia kupata maana ya neno au maneno
kama yanavyotumika katika kazi hiyo.
3.
Msimbo
wa Kiseme
Huhusisha kuelezea elementi nasibishi za
Kisemantiki. Unasaidia kuwaelewa
wahusika wa kazi ya fasihi kwa kupitia sifa ambayo wahusika wanapewa.
4.
Msimbo wa Kiishara
Unahusisha jinsi ambavyo wasomaji
wanavyosumbua maana za kiishara za kazi za fasihi
5.
Msimbo
wa Kiutamaduni
Hujengwa na viashiria mbalimbali vya
kiutamaduni ili kuweza kujua maana ya viashiria hivyo
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>>>>>