Wanafunzi Wakutwa Wakilawitiana Katika Shamba la Migomba huko Moshi
Wanafunzi wawili wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ongoma iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamekutwa wakilawitiana katika shamba la migomba jirani na shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Jerad Kesi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 5 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Mwalimu Kesi alisema mmoja wa wazazi wa
watoto hao alivamia shuleni hapo na kuwapiga walimu kwa kile alichosema
kuwa walimu hao walikuwa wamemdhalilisha mtoto wake.
“Siku ya tukio, wanafunzi wawili wa darasa la pili na mmoja wa darasa
la kwanza walikutwa na mwalimu wangu wakilawitiana kwenye migomba.
“Walipojua mwalimu amewaona, walikimbia na kuacha nguo zao pamoja na
yule wa darasa la kwanza. Tulipomhoji yule mtoto aliyebaki alikubali
kwamba amekuwa akilawitiwa na kwamba ameshafanyiwa kitendo hicho kama
mara saba hivi,” alisema Mwalimu Kesi.
Baada ya wanafunzi hao kutimua mbio, Mwalimu Kesi alisema walirudi
nyumbani na baadaye mmoja wa wazazi wao alifika shuleni hapo na
kuwashutumu walimu hao kwamba wamemdhalilisha mtoto wake kwa kumvua
nguo.
“Baada ya majibizano kati ya walimu na mzazi huyo, mzazi huyo aliwapiga walimu kwa fimbo na kuwajeruhi.
“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda kutoa taarifa polisi na kupewa
RB namba MJ/RB/988/15 kwa ajili ya kumkamata mzazi huyo,” alisema
mwalimu huyo.
Naye Mwalimu Idda Kilawe ambaye ndiye aliyewakuta wanafunzi hao wakilawitiana, amesema kuwa siku ya tukio
aliwakuta wanafunzi hao wakiwa ndani ya kibanda walichokuwa wamekijenga
kwenye migomba.
“Niliwakuta wakiwa wamejenga kibanda cha miti na kukiezeka kwa matawi
ya miti na ndani yake walikuwa wanafunzi watatu na wawili kati yao
ndiyo walikuwa wakilawitiana.