Watuhumiwa 40 wa mauaji ya tembo wakamatwa huku wengine wakiwekwa chini ya uangalizi maalum.
Kikosi
kazi,maalumu kilichoundwa na serikali, kufuatilia mwenendo wa mtandao
wa ujangili nchini kimefanikiwa kuwakamata watuhumumiwa muhimu zaidi
ya 40 na kuwaweka wengine chini ya uangalizi maalum, baada ya kuanza
kwa operesheni hiyo mwaka 2013
Mratibu wa kikosi hicho katika eneo la ikolojia ya
Serengeti,ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha kupambana na ujangili wa
mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro (NCAA)Bw.Robert Mande amewaambia
waandishi wa chama cha wanahabari za maliasili na utalii(TJT) kuwa hayo
ni matokeo ya ushirikiano wa vikosi vya kuzuia ujangili,katika mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro hifadhi ya Serengeti,Manyara na Tarangire.
Bw.Mande amesema tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa
mahakamani na kazi ya kufatilia mtandao huo inaendelea licha ya
kukabiliwa na changamoto nyingi zinazotokana na ukubwa na uzito walinao
watuhumiwa wa mtandao huo.
Uchunguzi ulioshirikisha makundi mbalimbali wakiwemo wananchi
wanaoishi jirani umeonyesha kuwa mtandao huo unajumuisha watu wa ngazi
mbali mbali wakiwemo wataalam kuua tembo na kutoa meno kwa
mudamfupi,madalali,na wamekuwa wakipewa mikopo yamagari, silaha na
mahitaji mengine ya kufanya ujangili ili kufanikisha kazi hizo na kutoa
rushwa kwa baadhi ya watendaji wanaojaribu kukwamisha kazi yao.
Kaimu meneja wa idara ya utalii wa mamlaka ya Ngorongoro
Bw.Asanaeli Merita, amesema changamoto ya ujangili uliokuwa umeshika
kasi hivi karibuni kwa upande mwingine imeongeza chachu ya udhibiti
na umakini kwa kila idara na baadhi ya matokeo yameonekana yakiwemo
kuongezeka kwa mapato.
Kati ya mwaka 2013 na 2014 Tanzania ilikumbwa na wimbi kubwa la
ujangili hasa wa meno ya tembo ambao licha ya kwamba kwa sasa
umedhibitiwa ulitishia uwepo wa wanyama hao na pia uchumi wa tanzania
ambao kwa kiasi kikubwa unategemea sekta ya utaliii.