Wanazuoni wa Kiislamu wajibu hoja ya maaskofu
Dar es Salaam. Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu
Tanzania imejibu hoja zilizotolewa wiki iliyopita na Jukwaa la Wakristo
nchini kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na hali ya
usalama na amani ya nchi.
Machi 10, mwaka huu maaskofu
kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania walitoa tamko na kuwataka waumini
wao kuipigia kura ya hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu
imepatikana kwa njia za hila na kibabe, jambo ambalo sasa limesababisha
mvutano.
Katika tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa,
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu
Tarcicius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania
(CPCT), Askofu Daniel Awet, maaskofu hao walisema uanzishwaji wa
Mahakama ya Kadhi ni uvunjifu wa Katiba na kuwa unahatarisha amani ya
nchi.
Walisisitiza kuwa Serikali ikiruhusu masuala ya
kidini kuingizwa kwenye mfumo wa sheria yatasababisha migongano kati ya
pande pindi zinazotofautiana.
Akizungumza Dar es Salaam
jana, Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni, Sheikh Khamis
Mataka alisema maaskofu wamejisahau kwamba wao ni viongozi wa kiroho na
kuwa wana wajibu wa kumpokea mtu yeyote na kumpa neno la hekima bila
kujali tofauti zao na siyo kushinikiza jambo.
Alisema
Watanzania wapatiwe Katiba Inayopendekezwa, wapate elimu, waisome kwa
makini na kuielewa ili wawe na uwezo na uhuru wa kuamua kupiga kura ya
‘Ndiyo’ au ‘Hapana’ bila shinikizo lolote kutoka kwa viongozi wa dini.
“Maaskofu
wamefanya kosa kubwa kuwachagulia waumini wao aina gani ya kura
wanayopaswa kupiga. Hiyo siyo kazi yao, wao wajikite katika kuhimiza
watu kujitokeza kupiga kura au kutoa elimu, siyo kuwaambia wapige kura
ya ‘Hapana’. Hilo ni suala la mtu binafsi kadri anavyolielewa jambo
husika,” alisema.
Sheikh Mataka alibainisha kuwa
Mahakama ya Kadhi inayolalamikiwa na Jukwaa la Wakristo ni haki ya
Waislamu na haiwahusu wala haihitaji ridhaa ya wasiokuwa Waislamu kama
ambavyo wao hawaingilii baadhi ya mambo ambayo Serikali inawafanyia
Wakristo.
Alisema Mahakama ya Kadhi inatambuliwa katika
sheria za Tanzania kwa sababu ni moja wa vyanzo vya sheria ya Tanzania.
Alisema sheria hizo zimekuwa zikitumika kuhukumu kesi za Waislamu
kuhusu ndoa, talaka na mirathi.
“Tangu mwaka 1963
ilipopitishwa Sheria ya Mahakama za Mahakimu (Magistrate Courts Act
1964), ikifuatiwa na Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ya 1964 na
kuhitimishwa na Sheria ya Ndoa ya 1971, Mahakama ya Kadhi inatambuliwa
kisheria. Si kweli kwamba tutavunja Katiba,” alisema Sheikh Mataka.
Alisisitiza kuwa mahakimu waliokuwa wanasikiliza kesi hizo hawana ujuzi
wa dini ya Kiislamu, hivyo wanachokitaka sasa ni Waislamu wenyewe kuamua
kesi zinazowahusu kwa kuwa wana ujuzi wa masuala hayo. Kiongozi huyo
ameitaka Serikali ipuuzie tamko la maaskofu na iendelee na mchakato wa
Mahakama ya Kadhi. Pia, aliwataka maaskofu wawe watulivu na kuwa
Serikali ni ya Watanzania wote.
“Maaskofu wameamua
kuanzisha utamaduni mpya wa kuyaendea mambo ya kisiasa kwa misingi ya
kiimani. Hilo ni tishio la kuwagawa Watanzania kwa misingi hiyo,”
alisema Sheikh Mataka na kuongeza kuwa madai kwamba Waislamu walipewa
rushwa ni dharau na kutowaheshimu, jambo ambalo lina athari zake.
Sheikh
Mataka aliongeza kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa Taifa ni wajibu wa
kila mwananchi na kuwa si busara kulilaumu Jeshi la Polisi kutokana na
vitendo vya kigaidi na mauaji ya albino yanayotokea nchini.
Alisema mauaji ya albino hayawezi kutokea kama wananchi hawatajenga utamaduni wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Posted Thursday, March 19, 2015 | by- Peter Elias na Emma Kalalu